Uchaguzi 2020 Ahadi na Sera za Tundu Lissu katika Uchaguzi Mkuu 2020
Neno moja tu limebaki,kuwagawana wale wote mafionso wa meko watakaojaribu kuiba kura.uzuri tunaishi nao familia zao tunazijua.
Hakika hapatatosha.ama AFE KIPA AU BEKI.
Huu uchaguzi ni jambia linakata pande zote.
Amigooo
 
CCM mpya inapata tabu sana wakati huu kutokana na kukosa watu makini na wajenga hoja

Hoja hujibiwa kwa hoja, kwa sasa Bashiru na Polepole hawawezi tena kujibu hoja kwani kuna mambo wanayakwepa kuogopa heshima yao kushuka

Tundu lissu anapangua hoja kama yupo kwenye mteremko

Kwa ufupi jamaa ana IQ kubwa sana kuanzia historia ya nchi hii mpaka leo anapangilia mambo sana

Wengi wanajifunza historia ya muungano toka kwa Lissu

Ccm asili ndio yenye uwezo wa hoja lakini wote wamekaa kimya
 
Ujibuji wa hoja uko chini sana sasa angalia mtu kama polepole anajibu habari mara misukule mara lisu sio mwenzetu hizo ni hoja kweli za kuwambia watu wenye akili zao timamu?
 
Nimemshusha hadhi Polepole Leo Sasa alichoongea mpaka mwisho ni mamlaka na vitisho kwa polisi na matusi Kama kichaa, naomba nimsaidie kumwambia hata upinzani wakiongea shombo wanakuwa jukwaani wakiwa wanahuburi lakini wakishuka jukwaani unaona wanaongea vitu vyenye akili vya kujenga Sasa mbele ya waandishi wa habari unaongea kama upo jukwaani? Kweli umeharibu sana.
 
Nimesikiliza Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CHADEMA Mhe. Tundu Lissu kwenye Kampeni zake mkoani Mara Hakika hakamatiki!!
Ili kumshinda Lissu kwenye Sanduku la kura itabidi CCM waibe vile hawajawahi kuiba tangu mfumo wa multipartism uanze.....!!!
 
Nitampigiaje mtu aliyekata mshahara wangu kisa tu nilitangaza nia.
Na bado mmerudishiwa mshahara adhabu hamjapewa. Hujui adhabu inayojadiliwa katika vikao juu yenu. Mnafunguliwa mafile upya mnaanza ajira upya kwa mshahara ya ajira mpya,na michango yenu mliyochangia mifuko ya hifadhi yote inachukuliwa na serikali. Saa hzi wanaitisha barua zenu za kurejeshwa kazini na za vibari. Itunze hii habari baada ya kupita uchaguzi utakuja nikumbuka
 
Lissu ni kama vile ameshashinda uchaguzi huu kwa hoja zake 7 ambazo zimepata nguvu na kuaminiwa na jamii. Na hii inajidhihirisha maeñeo mbalimbali ambayo amepita kufanya kampeni.

Lissu ni kama vile mhubiri wa injili, kila eneo analopita shetani anapoteza nguvu na neno linabaki mioyoni mwa watu. Maeneo ambayo bado hajapita ndio yamebaki kuzungumzia habari za CCM, lakini yatakapofikiwa na habari njema ya injili ya wokovu na ubatizo wa maji mengi na wao wataachana na CCM.

Hoja 7 ambazo Lissu zimemwongezea nguvu toka kwa makundi mbalimbali ambazo CCM wamekosa majibu yake

1. Vitambulisho vya wajasiliamali;

Ni hoja ambayo imepokelwa vizuri na watamzania, kila kona.CCm wameshindwa kujibu hadi sasa, wamebaki tu kudema dema kwenye majibu yao kwamba magufuri anawapenda wamachinga, Mara vitambulisho sio lazima ,wakati wamevitungia na sheria tayari. Lissu shikilia hapo hapo kwa mpaka waeleze ni lini wamachinga walioomba wauziwe vitambulisho visivyo na picha wala jina

2. Maslahi ya watumishi, nyongeza ya mshahara.

Hoja ambayo haijajibiwa hadi Leo, na ccm wamekosa majibu wakaeleweka kwa wananchi. . Nyongeza ya mshahara ni takwa la kisheria na sio takwa la mtu . Alisikika Mara moja akisema hajapandisha mshahara ila edhibiti mfumuko wa bei, na akapata majibu yake toka kwa Lissu kwamba bei ya sukari ya 2015 na Leo 2020 ipo sawa, ? "Wananchi hapana" Lissu " anatuambia nini. Baba shikilia hapo hapo wameshalegea na hawana majibu

3. Suala la pension na kiinua mgongo kwa wastaafu

Watu wengi walikuwa gizani na suala lakini baada ya kulitolea maelezo sasa nalo limepata hamasa miongoni kwa watanzania kwamba kuanzia mwakani wastaafu hawatapata pension zao zote baadala yake watapata nusu. Hilo limeonekana kuwa chuki kwa makundi hayo na CCM wameshindwa kutolea majibu ya kueleweka . Lissu shikilia hapo hapo wamesha nyooka tayari

4. Ujenzi wa uwanja wa ndege Chato na hifadhi ya wanyama

Hoja hapa sio ujenzi ,hoja inayoonekana hapa ni namna mradi unavyotekelezwa kwa ufisadi mkubwa wa kupeana tenda na Ndugu yake Mayanga . Mpaka Leo hoja hiyo Magufuli na CCM yake wameshindwa kuitolea majibu, kwa nini aingilie mchakato wa tender na kuagiza apewe ndugu yake na watu sasa huku wanasema ni kama mtu ameamua kupitishia di kwa ndugu yake. Amenipigia pasi kwa mbele ,na suala la hifadhi pia ndio hawana majibu kabisa .Baba Lissu shikilia hapo hapo wamesha nyong'onyea tayari

5. Suala la ununuzi wa ndege

Hii hoja ilianza kwa kasi mwanzoni kunadiwa na ccm lakini baada ya Lissu kuanza kushughurika Nayo wameshakimbia. Lissu amezungumzia masuala ya Faida na mchakato wa ununuzi wa midege hiyo imegubikwa na ufisadi mkubwa na kwamba anayejua ni Magufuri na mjomba wake Dotto James. CCM mpaka Leo wamepoteana na ajenda ya ndege sio ajenda yao tena kwenye kampeni zao.Lissu wabananishe hapo hapo kwenye kona washindwe pa kutokea.

6: Ukosefu wa Ajira kwa makundi mbalimbali

Eneo hili limepata uungwaji mkono mkubwa toka kwa makundi mbali mbali ya vijana. Tangu 2015 ajira zimetolewa kwa walimu wa sayansi na kada za afya. Kada nyingine hazijaguswa kabisa . Hoja yake hapa magufuri imebaki kuwa ni watu wajiajiri wakati yeye mtoto wake Jesca amemwajiri wizara ya mambo ya nje, mwingine amempa RAS iringa .hao walishindwa kujiajiri hadi awaajiri. Watoto wa wanyonge ndio wanaohimizwa kujiajiri. Hapo napo Lissu shikilia hapo hapo pana tija na kundi kubwa la wahanga

7: Waathirika wa vyeti feki
Hii ni hoja ambayo imepata kusemwa na Lissu, kwamba hao walio wa ajiri ni wao ccm na kinachozungumzwa hapa ni watu kufukuzwa kama mbwa bila kupewa mafao yao, ambayo wamechangia kwa miaka mingi halijulikani lilipo enda. Hao ni watanzania wenzetu na sio wakenya wala wamalawi, wamelitumikia na kutufundishia watoto wetu kwa miaka mingi hadi wengine wamekuwa maprofesa. Michango yao ipo wapi kama hawajapewa, Magufuri na ccm yao iliyojaa roho ya kuumiza watu waseme wamepeleka michango yao ya pension waliyokuwa wanachangia kwenye mifuko ya hifadhi

Nashauri Lissu sasa kwa kuwa kwenye miji yote na vijijini amefanikiwa kuiteka sasa ajikite katika kuwaaminisha watanzania ni namna gani walinde kula zao. CCM wamebaki na mbinu moja tu ya kuwategemea wakurugenzi na NEC, ili wawavushe hapo walipo kwenye tope kwenda nchi kavu. Katika hotuba zake sasa ajikite kuwahimiza wananchi kulinda kura zao, hii ngoma imeshaisha . Wakurugenzi na hawa watendaji kata ambao wamepewa maelekezo marafuku kuwatangaza wapinzani kwenye maeneo yao ndio imekuwa mwiba na Wapinzani wasipo jipanga vizuri mwishoni wataumizwa na hao watu.

Ushauri wangu Lissu sasa ajikite katika kulinda kura. Watendaji wa kata si wa kuchekewa na kuendelea kuachwa kwani kwanza ni watu wa chini mno, lakini ni watu ambao wameshapokea vitisho, hivyo inabidi kazi ya ziada ifanyike. Umati kwa umati Huo Huo wanaojaa kwenye mikutano yao wahimizwe pia wawepo hivyohivyo kwenye kulinda kulinda kura zao kwenye vituo vya kata na ofisi za wakurugenzi. Kwa umati ule wa mwanza wakifanikiwa kukaa kwenye kata na ofisi za wakurugenzi kazi itakuwa imeisha.

Kama una hoja nyingine ambayo unaona bado Lissu bado hajaizungumzia ambayo inaweza kuteka mioyo ya watu iweke hapa ,lakini pia unaweza kupendekeza mbinu sahihi ya kulinda kura

Chaaaaao, tuonane 28 oktoba
Vipi Kuhusu USHOGA unahisi Nalo Litampitisha kwenda Ikulu?
 
Fikra dhaifu kabisa.
1.Hapo awali machinga walikuwa wanalipa ushuru kila siku ambapo kwa makadirio ya kawaida ni zaidi ya 300,000 kwa mwaka, Hivi sasa machinga analipa sh.20,000 tu mwaka na anafanya shughuli zake mahali popote pale nchini, usitegemee machinga huyu akampa kura Tundu Lisu, kura yake atampigia Magufuli
2.Maslahi ya watumishi, nyongeza ya mshahara, elewa hii kuongezeka kwa mshahara hakumfanyi mtumishi maisha yake yawe bora zaidi itamfanya supplier aongeze bei ya bidhaa sokoni kisha mtumishi kuendelea kubaki palepale, Kinachofanyika ili kumlinda na kumheshimisha mtumishi ni mosi kumlipa mshahara wake kwa wakati, pili kumpunguzia kodi ya PAYE na tatu ni kuhakikisha mfumuko wa bei haupandi. Na haya yote Magufuli ameyafana hivyo kura zote za watumishi ni za Magufuli.
3.Suala la pensheni na kiinua mgongo tayari limeshashughulikiwa na ilani ya CCM imepanga kuliboresha zaidi hilo.
4.Ujenzi wa uwanja ndege chato, kwanza nikutoe ushamba Mwanza kuna uwanja wa ndege wa kimataifa na kisheria unahitaji uwe na strategic hydrome ambapo ndo umejengwa wa chato, pili hifadhi ya Taifa imeibuliwa ili kukomesha uhalifu uliokuwa unatokana na pori lililokuwepo hapo awali na tatu Chato nayo ni Tanzania na wanaishi watanzania pia.
5.Ununuzi wa ndege elewa hii, Pato la taifa letu linategemea utalii pia, ulitegemea watalii wakija wapande bajaji mpak kwenye maeneo ya utalii? Pili tunahitaji kufanya exportation ya
several products ulitegemea tutafanya kwa pikipiki. Watanzania wanaelewa na watamchagua Magufuli.
Vyeti feki ulitaka watumishi wasiokuwa na weledi waendelee kuingamiza Tanzania? Hiyo haikubaliki aisee. Tanzania ya sasa Magufuli ndie Rais wetu na tutamchagua tena. Kura yangu nitampa Magufuli
 
Screenshot_20200927-183350.jpeg
 
Back
Top Bottom