MJADALA UNGELITAKIWA UWE KUMUONGEZEA MUDA JPM NA SIO KUOMBANA KURA.
Na Thadei Ole Mushi.
Kuna siku niliwaambia wenzetu huko nje wakiona wamepata kiongozi mwenye maono huwa hawamwachii kwa haraka.
Niliwahi kuwaambia kuwa Urusi wao kwa kutambua Mchango wa Putin waliamu kubadilisha katiba yao badala ya Putin kustaafu 2024 walimuongezea muda mpaka 2036. Bunge la Urusi lilipitisha kipengele hicho Cha kumuongezea muda Putin kwa kishindo. Warusi wanaona kuwa ili maono ya Taifa lao yakamilike lazima pale juu awepo mtu mbishi Kama Putin na asiyeyumbishwa na mataifa Mengine.
China wao mwaka 1990 kwenye katiba yao walipitisha kuwa kila Rais atastaafu baada ya miaka 10 akiwa madarakani. Lakini mwaka juzi waliamua kubadilisha kipengele hicho kwa kuhofia kumpoteza Xi Jinping wameamua kugusa Katiba yao na Sasa atakaa madarakani Hadi Kifo kitakapomchukua. Jinping alikuwa astaafu 2023 kwa mujibu wa katiba kabla hawajaigusa.
Nimekuwa nikiwaleta maajabu ya Serikali ya awamu ya Tano kila Mara leo tuguse kipengele Cha Elimu kwa miaka mitano Nini kimefanyika.
1. Serikali ya awamu ya tano ilipoingia madarakani iliamua kufuta kabisa ada kwa wanafunzi wote wa kuanzia awali Hadi kidato Cha nne. Mpaka kufikia February 2020 Serikali ilikuwa imeshatoa shilingi trilioni 1.01 kugharamia Elimu bure. Ni nchi pekee kwenye ukanda wetu huu iliyoweza kutoa Elimu bure.
2. Serikali ya awamu ya tano imefanikiwa kuongeza shule za primary toka 16,899 zilizokutwa 2015 Hadi kufikia 17,804.
3. Kwa upande wa Shule za Sekondari zimeongezwa Kutoka 4,708 Hadi 5,330.
4. Serikali imefanya Ukarabati wa shule kongwe 73 Kati ya 89. Ukarabati huu kila pembe ya nchi mnauona unavyitafuna mabilioni ya shilingi.
5. Serikali ya awamu ya tano imefanya Ujenzi wa mabweni 253 ya shule za Serikali.
6. Serikali ya awamu ya tano imefanikiwa kufanya Ujenzi wa Maabara 227 katika shule mbalimbali nchini
7. Serikali ya awamu ya tano imetoa vifaa vya Maabara zipatazo 2,956.
7. Madawati JPM aliyokuta yalikuwa 3,024,311. Ameyaongeza Hadi kufikia 8,095,207 sawa na asilimia 200 ya ongezeko.
8. Vyuo vya ualimu 18 vimejarabaitiwa. Vyuo hivi vilielekea kuwa magofu. Hii Ni kazi ya Serikali ya awamu ya tano.
9. Vyuo viwili vimejengwa upya Murutunguru na Kabanga. Kazi hii imefanyika ndani ya miaka mitano.
10.Zimegawanywa computer 1,550 kwenye vyuo 35 vya ualimu nchini.
11. Vyuo vya ufundi VETA vimeongezwa toka 672 mwaka 2015 Hadi 712 mwaka 2020
12.Bajeti ya mikopo ya Elimu ya juu imeongeza toka Bilioni 348 kwa mwaka Hadi Bilioni 450.
Sisi tunaoelewa Nini kimefanyika usituulize kwa nn tunataka JPM aongezewe Muda.
Usituulize kwa nn tunataka JPM achaguliwe Tena.
Narudia Yale mazuri ya Upinzani yatachujuliwa na ikiwezekana wale wenye uwezo mkubwa kichwani wanaweza kuchukuliwa wakalijenge Taifa lao.
Duniani hakuna nchi ambayo imewahi kumaliza Changamoto zake zote. Lakini mnapopata mtu wa kupambana nazo Kama JPM sio wa kumwachia haraka.
Ole Mushi
0712702602.
Sent from my TECNO F3 using
JamiiForums mobile app