Madhehebu yote ya dini wanapewa misamaha ya kodi kiwango fulani, kama wakiomba.
Kama ambavyo watumishi wote wa umma wanapata tax exemption kwenye bidhaa fulani, lakini pia ni mpaka uombe.

Ni juha wa kutupwa tu anayeweza fikiri kuwa kodi hazishughulikiwi na TRA, ila na hao watoa mizigo (TPA & assoc).

Ukisema taasisi za dini zinaogopa kwamba DPW wakija,misamaha ya kodi itakwisha,maana yake ni kuwa hao DPW pia watahusika na ukusanyaji wa mapato na mifumo yote ya utoaji mizigo.

Maana yake kwa mujibu wako wewe Crocodiletooth na wenzako, DPW inawaondoa TRA pale bandarini na kubadilisha sera na sheria zetu za kodi.
 
Ni nini kimekusibu mpaka ukatoa matspishi kiasi hiki?
PS.
Karamagi ni muislamu.
 
Mimi ni mkristo mkatoliki! Natoa maoni yangu kwa mujibu wa Ibara ya 18 ya katiba ya Tanzania.

1.With due respect, sijaona wazo la maana la TEC. There is NO substance in it. Dunia ya leo inajengwa na uwekezaji wa kimataifa(international investments).

Hata China, Russia kuna uwekezaji mkubwa wa makampuni toka nje ya nchi. Tanzania siyo kisiwa. Lazima tuendane na sera za kiuchumi za dunia ya leo. Kuendesha mifumo ya uchumi mkubwa kama bandari, kijamaa tumeshindwa na tutaendelea kushindwa. Hata hii SGR tukisema iendeshwe kwa mifumo ya utumishi wa umma tutashindwa pia. Assets zenye sura ya kibiashara kama hii lazima ziendeshwe na private sector ili zilete faida na tija.

2. Findings za hao TEC ziko based on heresay. Wametumia axiom ya vox populi vox dei, Sauti ya watu ni sauti ya Mungu.Je ni watanzania wangapi wanapinga uwekezaji huu wa DP World? Je kuna wakatoliki wangapi hapa nchini? Je wakatoliki wote wanaupinga mkataba huo? Je wakatoliki waliomo kwenye orodha za wakatoliki bado ni wakatoliki mpaka sasa?(Wengi wameshahamia kwenye ulokole).

Ukijibu maswahi hayo utaona maaskofu wa TEC hawana uhalisia kwenye waraka wao.Ni blah blah tu. No driving facts. It is just FALLACY OF GENERALIZATION. Findings zao hazina supporting data. Wamekurupuka!

3. DINI: Naona ni hofu za masilahi yao ya kidini, wala siyo tatizo la mkataba. Wazungu toka nchi za magharibi walipoingia mikataba ya kuiba madini ya watanzania, maaskofu wa TEC walikaa kimya!!! Leo wakati wa mkataba na waarabu ETI wanajitia kuandika waraka wakijipambanua ETI wazalendo,watetezi wa rasilimali za nchi. UWONGO mtupu!

4. Serikali haina dini na mambo yote ya dini yapo nje ya mifumo ya serikali(Ibara ya 19 ya katiba ya TZ,1977). Huo waraka wao hauna mashiko wala nguvu yoyote mbele ya Jamuhuri. Ni kama makaratasi ya kufungia maandazi tu! Hayo ni maoni yao kama maoni ya mtu yoyote yule.

CONCLUSION: Serikali iendelee na mchakato wa utekelezaji wa mkataba na DP World HARAKA SANA, ili kama taifa tuanze kunufaika na uwekezaji huo HARAKA. Serikali kikatiba ina mizizi mirefu sana na mikubwa sana, isiyumbishwe na kelele za chura ambazo ni nyepesi sana.

Wananchi tuna hitaji pesa ipatikane ili tupate huduma bora za kijamii. Uwekezaji DP world ni LAZIMA ufanyike. Na ufanyike HARAKA iwezekanavyo. Serikali ina legitimacy ya kufanya maamuzi kwa niaba ya wananchi kwa sababu iliingia SOCIAL CONTRACT na wananchi kwa kushinda uchaguzi,2020.
 
Wenzako tang jana wanaruka na kukanyagana humu kiujumla wamepagawa tang tamko la Tec litoke. Yaan wanapaparika kila mmoja anakuja na uzi kila baada ya lisaa 🤣🤣🤣 chezea maslahi kuguswa weye 🤣🤣🤣!! Mtatema ulimi!!
 
Mimi nafikiri hapa hoja kubwa inayo pigiwa kelele ni ubovu wa mkataba ilio ingia Tanganyika na Dubai.
Nimesikia, mkataba mbovu ambao hauna maslahi mapana kwa taifa ndio hasa chanzo na ndipo tatizo lilipo anzia.
Kwahivyo hapa hoja sio kwamba wapingaji hawataki muwekezaji, Lah.
 
........wabongo tulio wengi nadhani tuna shida kidogo, hili ulilosema limerudiwa zaidi ya mara mia lakini sijui kwa nini watu hatuelewi.......
 
Hakuna anaebisha kuwa mkataba wa DP World na Tanzania ni mbovu.

Wanaharakati wameweka bayana na sisi tusio wanasheria tumeelewa. Hilo ni jambo jema.

Shida inakuja pale Taasisi moja ya dini inajiona yenyewe ndio inaweza kuamua na kusemea taasisi zingine. That's stupidity!

Tanzania ni ya wote Christians, Muslims, Jews, Buddhists na hata wasio na dini rasmi za kigeni.

Iweje Taasisi moja idai yenyewe ndio ina mizizi kwenye kila kaya. Kwa hiyo mnatutisha sisi protestants na Waislamu eeh?

Mbona mnamwandama sana Rais na serikali, angekuwa ni muumini wenu mngefanya hivyo?

We are no longer under the yoke of Papacy regime.

Waprotestant tupo wengi tunaweza jisemea. Naomba mkae kwa kutulia.

Mkataba hatuutaki na utumwa wa kidini hatuutaki pia. Nimemaliza.

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…