Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC): Hatuungi mkono Mkataba wa Bandari. Sauti ya Watu ni sauti ya Mungu
6 Hapana hata mmoja aliye kama wewe, Ee Bwana; wewe ndiwe uliye mkuu, na jina lako ni kuu katika uweza.
7 Ni nani asiyekucha wewe, Ee mfalme wa mataifa? Maana hii ni sifa yako wewe; kwa kuwa miongoni mwa wenye hekima wote wa mataifa, na katika hali yao ya enzi yote pia, hapana hata mmoja kama wewe.
... si uweke katika muendelezo mmoja kwenye post ya kwanza mzee?
 
Endapo taasisi ya Urais ingevunjiwa heshima saahizi si wangekuwa lupango wananyea debe[emoji3][emoji3]

Sent from my HUAWEI NMO-L31 using JamiiForums mobile app
Mafisadi na ujanja wenu wote wa kuiba hela za wananchi, na pia kuingia mikataba ya kimangungo! Bado hamna jeuri ya kuwakamata Maaskofu wa Kikatoliki.

Imagine Askofu Mwamakula tu mnamgwaya!! Ndiyo muwe na jeuri ya kumkata Askofu wa Kikatoliki!! Jeuri yenu nyinyi ni kwenye ukamataji wa Masheikh tu kama Ponda Issa Ponda, Masheikh wa Uamsho, nk.
 
Huko shule ulienda kujifunza ujinga?.


Yaan Mahakama yenyewe, kwenye hukumu inaweka wazi madhaifu, Kuna Mahali mahakama yenyewe inashangaaa .


Watanzania wasomi na waso wasomi, wamesema.


TEC imesema, TEC sio kikundi cha waimba taarabu, mule wamejaa wasomi, na Amin usiamin, hata wakati wanaamua kuja na waraka Huu, walishirikiana na Serikali hiyohiyo.



Acha ujinga
 
Mkataba ni mbovu ila haifanyi taasisi ya Urais ivunjiwe heshima.

Sasa wanapodai wana mizizi kila kaya wanamtishia nani sasa?

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app

Wanatetea maslahi ya Taifa wanasema wanawakilisha maoni ya walalahoi, wananchi wa kawaida sababu wanajichanganya na hawa wananchi kila siku tofauti na Rais/serikali ambayo haitaki, haijali, haisikilizi maoni ya wananchi wengi.

Waislamu, Waprotestanti, Wapentokosti, wasio na dini wafanye hivi hivi tupate mkataba mzuri tunusuru vizazi vyetu na pesa zetu.
 
Mimi ni mkristo mkatoliki! Natoa maoni yangu kwa mujibu wa Ibara ya 18 ya katiba ya Tanzania.

1.With due respect, sijaona wazo la maana la TEC. There is NO substance in it. Dunia ya leo inajengwa na uwekezaji wa kimataifa(international investments).

Hata China, Russia kuna uwekezaji mkubwa wa makampuni toka nje ya nchi. Tanzania siyo kisiwa. Lazima tuendane na sera za kiuchumi za dunia ya leo. Kuendesha mifumo ya uchumi mkubwa kama bandari, kijamaa tumeshindwa na tutaendelea kushindwa. Hata hii SGR tukisema iendeshwe kwa mifumo ya utumishi wa umma tutashindwa pia. Assets zenye sura ya kibiashara kama hii lazima ziendeshwe na private sector ili zilete faida na tija.

2. Findings za hao TEC ziko based on heresay. Wametumia axiom ya vox populi vox dei, Sauti ya watu ni sauti ya Mungu.Je ni watanzania wangapi wanapinga uwekezaji huu wa DP World? Je kuna wakatoliki wangapi hapa nchini? Je wakatoliki wote wanaupinga mkataba huo? Je wakatoliki waliomo kwenye orodha za wakatoliki bado ni wakatoliki mpaka sasa?(Wengi wameshahamia kwenye ulokole).

Ukijibu maswahi hayo utaona maaskofu wa TEC hawana uhalisia kwenye waraka wao.Ni blah blah tu. No driving facts. It is just FALLACY OF GENERALIZATION. Findings zao hazina supporting data. Wamekurupuka!

3. DINI: Naona ni hofu za masilahi yao ya kidini, wala siyo tatizo la mkataba. Wazungu toka nchi za magharibi walipoingia mikataba ya kuiba madini ya watanzania, maaskofu wa TEC walikaa kimya!!! Leo wakati wa mkataba na waarabu ETI wanajitia kuandika waraka wakijipambanua ETI wazalendo,watetezi wa rasilimali za nchi. UWONGO mtupu!

4. Serikali haina dini na mambo yote ya dini yapo nje ya mifumo ya serikali(Ibara ya 19 ya katiba ya TZ,1977). Huo waraka wao hauna mashiko wala nguvu yoyote mbele ya Jamuhuri. Ni kama makaratasi ya kufungia maandazi tu! Hayo ni maoni yao kama maoni ya mtu yoyote yule.

CONCLUSION: Serikali iendelee na mchakato wa utekelezaji wa mkataba na DP World HARAKA SANA, ili kama taifa tuanze kunufaika na uwekezaji huo HARAKA. Serikali kikatiba ina mizizi mirefu sana na mikubwa sana, isiyumbishwe na kelele za chura ambazo ni nyepesi sana.

Wananchi tuna hitaji pesa ipatikane ili tupate huduma bora za kijamii. Uwekezaji DP world ni LAZIMA ufanyike. Na ufanyike HARAKA iwezekanavyo. Serikali ina legitimacy ya kufanya maamuzi kwa niaba ya wananchi kwa sababu iliingia SOCIAL CONTRACT na wananchi kwa kushinda uchaguzi,2020.

Ni nani mhandisi wa hii karakana ya uzushi na uongo?
 
Huo NI MTAZAMO wako juu ya TEC na sidhani kama dini nyingine zimezuiwa kutoa tamko tofauti hapo ni kwamba TEC wamechukulia hilo suala serious kwa mustakabali wa Taifa wengine labda wamechukulia poa tu bora liende sasa TEC wasitoe ya moyoni kwa kuogopa kwamba wasabato hawajasema kitu LA HASHA
 
Kuna jamaa mmoja anaitwa Pascal Mayalla ameleta uzi wake na akaupachika kwa jina Mpeni Mungu yaliyo ya Kimungu na Kaisari yaliyo ya Kaisari! Hiki kinachofanywa na Baraza la Maaskofu Katoliki, sio kuchanganya dini na siasa?

Huyu kijana akajinasibu kuwa yeye ni mkatoliki. Kwanza nataka nimwambie tu ukatoliki haupo katia kujitambulisha bali upo katika kufanya kwa vitendo.

Nipo hapa kuujibu uzi wake aliouleta kwa mbwembwe nyingi akitumia andiko moja na akashindwa kuelewa context ya hilo andiko.
Andiko linalosema ya kaisari mpatie kaisari na ya Mungu mpatieni Mungu ni suala la kulipa Kodi na wala siyo issue ya Bandari.

Sasa nitaanza kama ifuatavyo:-

Zab 24:1​

Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya BWANA, Dunia na wote wakaao ndani yake.
Biblia inatueleza kuwa kila kitu kilichopo duniani ni mali ya Bwana. Kama tunaongelea Vitu vya Mungu TEC wamaefanya Utume wa kusimamia Mali za BWana.

Zab 11:3
Kama misingi ikiharibika, Mwenye haki atafanya nini?

Hapa ndipo kwenye akili na Hekima TEC ni watumishi wa Bwana wa Majeshi. Maana yake Mungu wetu ni Mungu mwenye haki na ni Mungu wa vita. Kwa hiyo Misingi ikiharibika mwenye haki lazima achukue hatua na kutimiza wajibu wake.

Mithali 3:19​

Kwa hekima BWANA aliiweka misingi ya nchi; Kwa akili zake akazifanya mbingu imara.

Kwahiyo Kazi waliyoifanya TEC ni kazi ya Bwana.

YEYOTE ANAYETAKA KUWAPINGA WATUMISHI WA BWANA HAKIKA NI MPINGA KRISTO

Rum 1:16-17​

Kwa maana siionei haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia. Kwa maana haki ya Mungu inadhihirishwa ndani yake, toka imani hata imani; kama ilivyoandikwa, Mwenye haki ataishi kwa imani.
 
Hakuna anaebisha kuwa mkataba wa DP World na Tanzania ni move. Wanaharakati wameweka bayana na sisi tusio wanasheria tumeelewa. Hilo ni jambo jema.

Shida inakuja pale Taasisi moja ya dini inajiona yenyewe ndio inaweza kuamua na kusemea taasisi zingine. That's stupidity !

Tanzania ni ya wote Christians, Muslims, Jews, Buddhists na hata wasio na dini rasmi za kigeni.

Iweje Taasisi moja idai yenyewe ndio ina mizizi kwenye kila kaya. Kwa hiyo mnatutisha sisi protestants na Waislamu eeh?

Mbona mnamwandama sana rais na serikali angekuwa ni muumini wenu mngefanya hivyo?

We are no longer under the yoke of Papacy regime.

Waprotestant tupo wengi tumaweza jisemea.
Naomba mkae kwa kutulia.

Mkataba hatuutaki na utumwa wa kidini hatuutaki pia.
Nimemaliza.

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app

1. Hivi unajuwa kuwa TEC ni wakatoliki pekee???

2. Kuna mahali popote kwenye tamko lile wamesema wanawasemea na watu wenye imani nyingine nje ya ukatoliki???
 
Hakuna anaebisha kuwa mkataba wa DP World na Tanzania ni move. Wanaharakati wameweka bayana na sisi tusio wanasheria tumeelewa. Hilo ni jambo jema.

Shida inakuja pale Taasisi moja ya dini inajiona yenyewe ndio inaweza kuamua na kusemea taasisi zingine. That's stupidity !

Tanzania ni ya wote Christians, Muslims, Jews, Buddhists na hata wasio na dini rasmi za kigeni.

Iweje Taasisi moja idai yenyewe ndio ina mizizi kwenye kila kaya. Kwa hiyo mnatutisha sisi protestants na Waislamu eeh?

Mbona mnamwandama sana rais na serikali angekuwa ni muumini wenu mngefanya hivyo?

We are no longer under the yoke of Papacy regime.

Waprotestant tupo wengi tumaweza jisemea.
Naomba mkae kwa kutulia.

Mkataba hatuutaki na utumwa wa kidini hatuutaki pia.
Nimemaliza.

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
Wameanza lini?Unamkumbuka sheikh Mwaipopo?
 
WACHA TUSEME, TANZANIA NI YETU SOTE SIO MALI YA WAKRISTO

Hivi karibuni kumezuka mjadala mkali kuhusu Serikali kuingia kwenye makubaliano ya kuendesha bandari za Tanzania na kampuni ya DP World.

Mjadala huu ulianza na sura ya kisiasa wakati Mwenyekiti wa Chadema Bwana Freeman Mbowe alipotoa shutuma kali kuwa bandari za Tanganyika zinauzwa na Wazanzibari yaani Waziri wa Ujenzi, Mhe Makame Mbarawa na Mhe Rais Samia Suluhu Hassan.

Lakini ghafla mjadala ukahama kwenye Siasa na ukatawaliwa na hisia kali za kidini.

Sote tumeshuhudia namna viongozi wa dini ya Kikristo hasa wakatoliki wakiongozwa na Kadinali Pengo walivyokuwa wakilipigia kelele suala la Bandari.

Hoja zinazotawala mjadala huu ni mbili.

Hoja ya kwanza ni kwamba mkataba ule umesainiwa na Waziri Mzanzibari na Rais Mzanzibari na kwamba Wanzanzibari hawa wawili wanauza mali za Tanganyika. Hoja yao ya pili inadai kuwa mkataba hauna ukomo wa muda, yaani ni mkataba wa milele.

Hii hoja hii ya pili inashabikiwa sana na viongozi wa Kanisa.

Jambo la kushangaza ni kuwa mpaka sasa hakuna hata msemaji mmoja, awe mwanasiasa au kiongozi wa Kanisa aliyetoa hoja za kiuchumi na utendaji za kupinga makubaliano hayo.

Badala yake, viongozi wengine kama vile mama Anna Tibaijuka anadiriki kusema uwongo kuhusu sababu za DP World kukataliwa kuendesha Bandari za Marekani.

Mama Tibaijuka anajua vyema lakini hakutaka kusema kuwa sababu ya kukataliwa kuongoza Bandari za New York na New Jersey ni Uwarabu wao na wala si utendaji wao.

Ni kweli Bunge la Marekani lilikataa DP World wasipewe Bandari hizo lakini walisema wazi kuwa Marekani haiwezi kuwapa Waarabu kuendesha Bandari zao kwa sababu za kiusalama.

Hakuna asiejua msimamo wa Marekani kuhusu Waarabu na Waislamu.

Kwa makusudi kabisa, mama huyu anapotosha watu kwa kufananisha suala la bandari za Marekani na bandari za Dar es Salaam.

Kwenye suala la Dar es Salaam, DP World haikutaka kununua TPA.

Inachopendeza ni kuendesha na si kununua Bandari ya Dar es Salaam.

Suala hili la kuendesha si geni Tanzania.

Kampuni ya TICTS imeendesha Bandari ya Dar es Salaam kwa zaidi ya miaka 20.

Kampuni ya “Swissport” inaendesha Kiwanja cha Ndege cha Dar es Salaam kwa muda mrefu.

Mbona hizi kelele hatukuzisikia?

Wakati wa utawala wa Donald Trump Marekani ilifika hatua ya kupiga marufuku baadhi ya Mataifa ya Arabuni kwa maana Waislamu kuingia Marekani.

Kwa hiyo mama Tibaijuka hakutaka kuwa mkweli kuhusu suala hili.

Ametumia kivuli chake cha kuwa mfanyakazi wa Umoja wa Mataifa kwa wakati ule kuwaaminisha Watanzania kuwa yeye anafahamu zaidi kuhusu ubaya wa DP World.

Mama Tibaijuka amekosa uadilifu (moral authority) wa kuweza kukemea kile alichokiita mkataba mbovu kwa sababu wakati kampuni ya TICTS iliyokuwa inaendesha Bandari ya DSM kwa utendaji wa ovyo huyu mama alikaa kimya hata pale ambapo TICTS walipopewa nyongeza ya mkataba wa miaka 15 bila kufuata sheria za manunuzi.

Lakini jambo la pili, nani asiyejua kuwa mama Anna Tibaijuka alikiri hadharani kuwa alipokea shs 1.6 bilioni ya fedha za rushwa za ESCROW?

Huyu mama ambaye alisema kwa majigambo kuwa shs 1.6 bilioni ni pesa ya mboga ana uchungu gani wa kuwatetea Watanzania masikini?

Bado tunarejea kusema tena kwa kinywa kipana, mpaka sasa hakuna mtu hata mmoja aliyesema kwa kuonesha ushahidi kuwa DP World hawana uwezo kifedha au utendaji wao ni mbovu. Hakuna aliyesema kuwa hizo fedha ambazo tunaahidiwa ni ahadi hewa kwa sababu DP World hawana uwezo wa kuvutia mizigo kupitia Bandari ya Dar es Salaam.

Kwa kuwa mjadala umetawaliwa na CHUKI za kidini na wasemaji wakubwa wamekuwa viongozi wa Kanisa.

Tukumbuke kuwa ni Wakristo hao hao ambao mmoja kati ya viongozi wao waliosema kuwa Rais Samia anafanana na muuza vitumbua!

Makanisa hawakukemea kauli hii ya kumkosea adabu Rais.

Kwa kuwa mjadala wa bandari una chuki za udini, naomba tujikumbushe nafasi ya Makanisa katika nchi hii.

TUKUMBUKE MWAKA 1992
Mwaka 1992, Serikali iliingia Mkataba na Makanisa kupitia Taasisi zao za TEC na CCT.

Chini ya Makubaliano yale, hospitali za Makanisa zitatumika kwa wananchi wote pale ambapo serikali haina hospitali.

Kwa kufanya hivyo, Serikali itakuwa na wajibu wa kuyapa Makanisa fedha za kuendesha hospitali hizo ingawa umiliki wa hospitali utabaki kuwa wa makanisa.

Ifahamike kuwa fedha hizo zinatokana na kodI za Watanzania wote:

Waislamu, Wakristo, Mabaniani, Magoha, Makadiani, na hata wale wasio na dini.

Nini athari za Mkataba huu?

Mkataba huu wa kibaguzi una athari nyingi.

Kwanza:

Serikali inatumia kodi za wananchi kuyapa makanisa kuendesha shughuli zake za kuimarisha Ukristo.

Tunasema hivyo kwa sababu utaratibu unaotumika ni kuwa serikali inatoa fedha kwa makanisa ambayo wao ndio wanapanga matumizi ya fedha zile na sio Serikali.

Pili, kwenye Jamii, makanisa yanaonekana ndio yanatoa huduma za Jamii na hivyo kujenga saikolojia kwa wananchi kuwa Ukristo ndio unajali wananchi.

Athari ya tatu ni kuwa makanisa yananyonya wananchi kwa sababu pamoja ya kuwa hospitali zile zinapata fedha kutoka serikalini, bado wananchi wanalipia huduma.

Nne, Mkataba hauna ukomo, yaani ni wa milele.

(Wakristo wataendelea kupewa hayo mabilioni na Waislamu watanyimwa milele).

Kwa tafsiri nyingine ni kuwa Serikali imejivua kwenye wajibu wa kutoa huduma za Jamii na kuchagua Makanisa kuwa ndio wakala wake.

Tunapenda kuwakumbusha Watanzania kuwa wakati Mkataba huo unasainiwa aliyesaini Mkataba ni Bwana Edward Lowassa aliyekuwa Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu.

Huyu ni Mkristo.

Kwa utaratibu wa Serikali, Lowassa alikuwa Waziri wa Nchi, hivyo basi Waziri mwenye dhamana ni yule mwenye ofisi yake kwa maana ni Waziri Mkuu.

Wakati unatiwa saini Mkataba, huo Waziri Mkuu alikuwa John Samwel Malecela ambaye ni Mkristo.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye ndie aliyeishauri Serikali isaini Mkataba ule ambao kwanza hauna ukomo (mkataba wa maisha) na pili unatumia kodi za wananchi kuimarisha Ukristo alikuwa Damian Lubuva ambaye ni Mkristo.

Kwa upande wa Kanisa mwanasheria wao alikuwa Prof Balozi Costa Mahalu, Mkristo.

Kwa maana hiyo, upande wa Serikali, Mkataba ule umeasisiwa na kusimamimwa na Wakristo watupu. Waziri wa Nchi Mkristo, Waziri Mkuu Mkristo, Mwanasheria Mkuu Mkristo.

Ni Wakristo! Wakristo! Wakristo!

Kama kwenye hoja ya makubaliano ya Bandari ni Wazanzibari wawili (ambao ni Waislamu) wamesaini makubaliano ya kuiuza Tanganyika, Mbona Waislamu hawakulalamika pale Wakristo 3 wazito Serikalini walipobuni mbinu za kutumia kodi za wananchi kuimarisha dini yao Ukristo Tanzania?

Kama hoja ni ukomo wa mkataba, mbona Mkataba huu wa Serikali na Makanisa hauna ukomo?

Ni mkataba wa milele na ndio maana mpaka leo (miaka 30 sasa) bado unaendelea kutumika.

Bado Serikali inaendelea kutekeleza mkataba wa kibaguzi ambapo inatumia kodi za wananchi wote kuimarisha shughuli za Kanisa.

USHAHIDI

Tarehe 23 Januari 2019, Rais Magufuli alikutana na viongozi wa dini zote IKULU.

Kwenye Mkutano ule Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana ambaye pia ni Askofu wa Dayosisi ya Tanga Bwana Maimo Mndolwa alilalamika kwa Rais Magufuli kuwa Serikali inavunja mkataba kwa kujenga hospitali kwenye maeneo ambayo Kanisa imeachiwa kuwa na hosptali ambazo zinapewa fedha na Serikali.

Amelalamika hivyo kwa sababu Mkataba wa Makanisa na Serikali hauna ukomo.

Kila penye hospitali ya Kanisa, Serikali haikutakiwa kujenga hospitali yake.

Badala yake, Serikali inatakiwa kuendelea kutoa fedha za kodi kuwapa Makanisa ili ziendeshe hospitali zao na kuimarisha Ukristo kwa kutumia jasho la Watanzania.

Katika kusisitiza madai yake, Askofu Mkuu alitoa ushahidi wa hospitali zilizojengwa na Serikali katika Wilaya ya Ifakara, Ngara na Muheza ambazo kwa mujibu wa Mkataba wa 1993, Serikali haikutakiwa kujenga hospitali hizo za Wilaya.

Kitendo cha Serikali kujenga hospitali hizo kinatafsiriwa na Kanisa kuwa Serikali imevunja Mkataba kwa sababu sasa inatoa huduma hiyo muhumu kwa wananchi.

Askofu Mkuu alifafanua kua matatizo haya yapo kwenye ngazi ya Wilaya kwa sababu kwenye ngazi za juu, hakuna tatizo kwa kuwa kuna Msimamizi anaesimamia Mkataba huo.

Hapa Askofu Mkuu alikuwa ana maana kuwa hospitali za KCMC ya Moshi, Bugando ya Mwanza na CCBRT ya Dar es Salaam ambazo zote ni mali ya Kanisa bado zinaendelea kupata fedha za kodi huku zikiendelea kuwalipisha wananchi kwa huduma wanazopewa kwenye hospitali hizo.

Rais Samia Suluhu Hassan alifanya Mkutano na Baraza la Maaskofu la Kanisa Katoliki Tanzania uliofanyika Kurasini tarehe 25 Juni 2021.

Katika risala yao, Baraza la Maaskofu limeilaumu Serikali kwa kujenga hospitali zake kinyume cha Mkataba wa 1992, na Makanisa.

Kwenye risala hiyo, Baraza la Maaskofu limeshangaa kuona Serikali inajenga hospitali kwenye Wilaya ambazo Makanisa tayari yana hospitali zao.

Wamehoji kwa nini kuwepo na ushindani wa kutoa huduma hizo?

Kwa maana nyepesi, kwa nini Makanisa yasiachiwe kuendesha hospitali maisha (milele) na kuendelea kupewa ruzuku zinazotokana na kodi za wananchi?

Risala hiyo ni ya chombo cha juu kabisa katika Kanisa Katoliki ambao leo viongozi hao hao wanaohoji na kulalamika kuhusu makubaliano ya Serikali na DP World kuwa hayana ukomo!

Kanisa hilo hilo ambalo linapiga kelele kuhusu mkataba wa Serikali na DP World, ndilo ambalo kiongozi wake Askofu Method Kilaini alipewa shs. 80.9 milioni, Askofu Eusebius Nzigirwa alipewa shs. 40.4 milioni na Mchungaji Alphonce Twimanye Simon alipewa shs 40.4 milioni fedha za Rushwa zilizotokana na kashfa ya akaunti ya Tegeta ESCROW.

Hadi leo Kanisa halijatangaza hadharani hatua za kinidhamu iliyowachukulia viongozi hao.

Ukimya huu tuutafsiri vipi?

Kwa ukimya huu, Kanisa linapata wapi “moral authority” ya kupinga mkataba wa DP World.

Watanzania hawajasahau wakati wa utawala wa Magufuli wameshuhudia mauwaji kule Kibiti na Rufiji ambayo ni Wilaya zenye Waislamu wengi.

Watanzania bado wanakumbuka viroba vyenye miili ya watu vilivyokuwa vinaokotwa Coco Beach kila uchao.

Kanisa lilikuwa wapi wakati Magufuli anatoa roho za watu wasio na hatia?

Masheikh wangapi wamepotea ambao mpaka leo hawajulikani walipo wakati wa utawala wa Magufuli?

Hao waliobahatika wametoka jela wakiwa vilema kama alivyo Sheikh Abdallah Maginga Wambura ambaye kakatwa mguu kutokana na vipigo vya Polisi?

Yuko wapi mwanasiasa Ben Saanane ambaye “kosa” lake ni kuandika kuwa PhD ya Magufuli ni feki?

Yuko wapi mwandishi Azory Gwanda ambaye “kosa” lake lilikuwa kuandika ukweli kuhusu mauwaji ya Kibiti?

Wakati wa utawala wa Magufuli, Mbunge wa Kilwa Kusini Mhe Selemani Bungara maarfu “Bwege” aliwahi kusema Bungeni kuwa raia wake walichukuliwa na askari msikitini na wamepotea mpaka leo hawajulikani walipo.

Kanisa halikuyaona haya?
Kama Kanisa ilifumbia macho udhalimu na ukatili huu, leo wanapata wapi mdomo wa kukemea hicho wanachokiita mkataba usio na maslahi kwa wananchi?

Ni wananchi gani hao ambao leo Kanisa linajifanya kuwatetea?

Sasa Watanzania wanakumbuka kuwa pamoja na ukatili wote wa Magufuli, ni viongozi hao hao wa Kanisa waliokuwa wakimkaribisha kila Jumapili kwenye Makanisa yao na kumpa nafasi ya kuzungumza.

Leo Kanisa linataka kuwadanganya Watanzania kuwa lina maslahi na wananchi?

Kuna kitu kikubwa zaidi ya uhai?
Wakati watu wanatolewa roho zao na Magufuli Kanisa lilikuwa wapi?

KWANINI WAKRISTO WANAPINGA MKATABA WA BANDARI

Mpaka sasa si Makanisa wala wanasiasa ambao wametoa hoja ya kiuchumi.

Tofauti na Wamarekani ambao walisema hadharani kuwa hawawezi kuwapa Waarabu kuendesha Bandari zao, hapa Tanzania sababu haswa ya kupinga Mkataba haisemwi hadharani.

Vinatafutwa visingizio tu. Ukweli ni kuwa Mkataba wa Bandari unapingwa na kuwepo kwa fikra potofu za Kanisa kuwa:

Iwapo DP World watapewa zabuni ya kuendesha Bandari, uwepo wao Tanzania utawanufaisha Waislam kwa namna moja au nyingine.

Kuna wanaohofia kuwa iwapo Bandari itafanikiwa, na endapo itatokea fursa ya miradi mingine mikubwa ya kiuchumi, Dubai watakuwa na nafasi nzuri ya kupewa miradi hiyo. Kwa hiyo kuwepo kwao kutaimarisha Uislamu.

Ikiwa DP World watapata tenda ya Bandari, nchi itapata mafanikio makubwa ya kiuchumi ambayo kwa fikra zao potofu yatakuwa yameletwa na Rais Mwislamu. Kwa maana hiyo, Waislamu wanaweza kuongoza nchi kwa ufanisi.

Tayari kuna watu wanaosema kuwa Samia awe Rais wa mwisho Mwislamu Tanzania

Kuna wanaosema Bandari ikipata mafanikio itaonekana kuwa kumbe wanawake wanaweza kuongoza nchi vizuri
Kuna wasemao kuwa Bandari ikifanikiwa itaonekana Wanzanzibari nao wana uwezo sawa na wa Bara katika kuliongoza taifa letu.

Hoja zote hizo ni za kipuuzi.
Mafanikio yakiletwa na Rais Mwislamu au mwanamke au Mzanzibari wataonufaika ni wananchi wote.

Fedha za Bandari zitawanufaisha WOTE kwani anaepanga matumizi ya fedha ni Bunge letu ambalo lina Wabunge Waislamu, Wakristo na wasiokuwa na dini.

MWISHO
Nchi hii Waislamu wamekuwa wakidai kuwa Tanzania ni NCHI YETU SOTE, Waislamu wamekuwa wakidai kuwa idadi yao ni kubwa

Waislamu wanajigamba kuwa wamesoma lakini hawapewi fursa sawa

Kinachoshangaza ni kuwa tokea Mjadala wa Bandari uanze na hata mijadala mingine inayohusu UDINI huwasikii Waislamu kusema lolote.

Wao ni kimyaaaaaaaaaa.

Mjadala wa Bandari umetawaliwa na viongozi wa dini ya Kikristo, Wasomi Wakristo, Taasisi za Kikristo na hata wanasheria waliofungua kesi Mahakamani ni Wakristo.

Kwenye mjadala wa Bandari kuna mafunzo kwa Waislamu.

Sote tujiulize maswali yafuatayo:

Hao Wasomi Waislamu wanaolalamika hawapati fursa leo wako wapi?

Mbona hawapazi sauti zao?

Au Usomi wao ni wa makaratasi na kutafuta ajira tu?

Hiyo haki wanayoidai inaenda na WAJIBU.

Lazima watimize wajibu wao kwa kutumia taaluma na vipawa vyao kupaza sauti zao.

ZIKOWAPI TAASISI ZA KIISLAMU

Au zinasubiri mwezi wa Ramadhani kuomba msamaha wa kodi za tende?

WAKO WAPI MABARAZA YA ULAMAA

Au wanasubiri mwezi wa Ramadhani kualikwa futari IKULU?

WAKO WAPI VIJANA WA KIISLAMU

Hivi kweli nchi hii hakuna hata Waislamu wa kawaida kwenye magenge na vijiwe wakajibu hoja za Wakristo?

Bwana Mtume SAW Anatufundisha tunapoona uovu tuuondoe kwa mikono yetu. Kama hatuwezi basi tukemee.

Na kama hatuwezi kukumea basi angalau tuchukie ingawa kuchukia ni imani dhaifu.

Leo Waislamu kwa mamilioni yetu tunashindwa hata KUSEMA?

Tumeamua kuwa na imani dhaifu na kuwaacha waseme Wakristo peke yao?

MWENYEZIMUNGU ASHUHUDIE TUMEFIKISHA
Ndo umeyajua leo?

Uliwahi kuona TEC wakisema sauti ya wengi ni sauti ya Mungu pale Maaskofu wa TEC walipolalamikiwa kuhusika kula fedha za wizi za escrow?

Uliwahi kuona Maaskofu wa TEC wakisema turudi kwenye mfumo wa chama kimoja kwa kuwa watanzania wengi wamekataa vyama vingi na sauti ya watu ni sauti ya Mungu?

Hawa watu ni cartels kama zilivyo cartels zingine duniani huko tofauti hawa wanavaa majoho na misalaba tu.

Ndo mana Rwanda walishtakiwa kama kumbikumbi kwa luhamasisha mauaji ya kimbari!
 
CHARLES KITIMA ACHA KUTUMIA KANISA KATOLIKI KUENEZA CHUKI ZA WAZI DHIDI YA RAIS SAMIA SULUHU

Na, Nulphin Charles Heche

Kwa mara nyingine, Kikundi kidogo cha wanachama wa Chadema ambao pia ni viongozi ndani ya Kanisa Katoliki wakiongozwa na Charles Kitima wameamua kuonyesha chuki za wazi kwa kusambaza kipeperushi kinacholenga kujenga chuki kati ya serikali na waumini wa Katoliki nchini.

Charles Kitima ambaye amekuwa akifanya shughuli mbalimbali za Chadema bila kificho amevuka mipaka ya kazi zake kama kiongozi wa kidini akijikita katika kutengeneza na kusambaza chuki dhidi ya serikali kwa madai ya kupinga uwekezaji katika Bandari ya Dar es salaam kama ilivyo ajenda ya chama chake.

Mawasiliano mbalimbali yanayofanywa na Ndg. Charles Kitima na kundi lake kuwashawishi viongozi wengine wa Kanisa Katoliki nchini ili waunge mkono hoja za Chama cha Demokrasia na Maendeleo na kueneza chuki dhidi ya serikali ni kinyume cha taratibu kwani Kanisa Katoliki si la CHADEMA.

Heshima ya Kanisa Katoliki ni kubwa kuliko maslahi ya Charles Kitima na rafiki zake wachache. Kueneza chuki dhidi ya Rais na serikali yake ni ukosefu wa uzalendo na kujisahau. Tanzania ni kubwa kuliko fedha au tija yoyote binafsi. Uwekezaji katika bandari ya Dar es salaam ni kwa maslahi ya umma na si vinginevyo.

Mageuzi yanayoleta tija kwa uchumi wa nchi yetu ni pamoja na kuvutia uwekezaji katika maeneo ya kimkakati kama vile Bandari. Kwa miaka zaidi ya thelathini Bandari yetu imekuwa ikiendeshwa na kampuni ya TICS na Charles Kitima hakuwahi kuhoji juu ya ufanisi hafifu lakini amepata ujasiri wa kueneza chuki dhidi ya serikali katika kipindi hiki muhimu, hili ni jambo la kushangaza na linatia aibu kwa kiongozi huyu anayejaribu kutumia Kanisa kuchafua serikali wazi wazi.
Kanisa limeongea ni Mungu ameongea JUMA JUMA, funga bakuli lako.
IMG-20230818-WA0014.jpg
 
Hata shingo ikiwa kama chuma ila ni Bora kutambua mziki wa TEC na impact hapo baadae tusionane wachawi
Haya mambo yako very complex. Humohumo kuna waumini wakatoliki walioshiriki kuupitisha na kuutetea sasa leo wanasomewa waraka kutoka kwa watu wanaoungama kwao!!!
 
Mkataba ni mbovu ila haifanyi taasisi ya Urais ivunjiwe heshima.

Sasa wanapodai wana mizizi kila kaya wanamtishia nani sasa?

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
1. Sehemu gani ya tamko imevunja heshima kwa taasisi ya urais?
2. Kwamba wana mizizi kila kaya ya kikatoliki, huko ni kutisha au ndo uhalisia?
 
CHARLES KITIMA ACHA KUTUMIA KANISA KATOLIKI KUENEZA CHUKI ZA WAZI DHIDI YA RAIS SAMIA SULUHU

Na, Nulphin Charles Heche

Kwa mara nyingine, Kikundi kidogo cha wanachama wa Chadema ambao pia ni viongozi ndani ya Kanisa Katoliki wakiongozwa na Charles Kitima wameamua kuonyesha chuki za wazi kwa kusambaza kipeperushi kinacholenga kujenga chuki kati ya serikali na waumini wa Katoliki nchini.

Charles Kitima ambaye amekuwa akifanya shughuli mbalimbali za Chadema bila kificho amevuka mipaka ya kazi zake kama kiongozi wa kidini akijikita katika kutengeneza na kusambaza chuki dhidi ya serikali kwa madai ya kupinga uwekezaji katika Bandari ya Dar es salaam kama ilivyo ajenda ya chama chake.

Mawasiliano mbalimbali yanayofanywa na Ndg. Charles Kitima na kundi lake kuwashawishi viongozi wengine wa Kanisa Katoliki nchini ili waunge mkono hoja za Chama cha Demokrasia na Maendeleo na kueneza chuki dhidi ya serikali ni kinyume cha taratibu kwani Kanisa Katoliki si la CHADEMA.

Heshima ya Kanisa Katoliki ni kubwa kuliko maslahi ya Charles Kitima na rafiki zake wachache. Kueneza chuki dhidi ya Rais na serikali yake ni ukosefu wa uzalendo na kujisahau. Tanzania ni kubwa kuliko fedha au tija yoyote binafsi. Uwekezaji katika bandari ya Dar es salaam ni kwa maslahi ya umma na si vinginevyo.

Mageuzi yanayoleta tija kwa uchumi wa nchi yetu ni pamoja na kuvutia uwekezaji katika maeneo ya kimkakati kama vile Bandari. Kwa miaka zaidi ya thelathini Bandari yetu imekuwa ikiendeshwa na kampuni ya TICS na Charles Kitima hakuwahi kuhoji juu ya ufanisi hafifu lakini amepata ujasiri wa kueneza chuki dhidi ya serikali katika kipindi hiki muhimu, hili ni jambo la kushangaza na linatia aibu kwa kiongozi huyu anayejaribu kutumia Kanisa kuchafua serikali wazi wazi.
Jikite kwenye Mkataba. Mlianzisha udini mkidhani utawasaidia?
 
Mafisadi na uja wenu wote wa kuiba hela za wananchi, na pia kuingia mukataba ya kimangungo! Bado hamna jeuri ya kuwakamata Maaskofu wa Kikatoliki.

Imagine Askofu Mwamakula tu mnamgwaya!! Ndiyo muwe na jeuri ya kumkata Askofu wa Kikatoliki!! Jeuri yenu nyinyi ni kwenye ukamataji wa Masheikh tu kama Ponda Issa Ponda, Masheikh wa Uamsho, nk.

Kwenye ule waraka Maaskofu 37 wa Katoliki wamesaini. Wakiwakilisha waumini wao, wazalendo, Watanganyika na Watanzania makini.

Mimi sio Mkatoliki. Ila nasema serikali hii basi iwakamate kuwafungulia kesi za uhaini tuone kitakacho tokea.

Badala ya kurekebisha mkataba wanahangaika na wazalendo
 
Back
Top Bottom