Umepeleka kisamvu cha kopo usipandishe mabega bure,upinde ndiyo mlivyo. Eti mwanasheria nguli,wanasheria nguli hawasemi bali kazi zao ndiyo zinawasemea. Wewe kutwa kucha uko humu kuishabikia DP World ndiyo unguli wako huo?
 
Nyie mnasubiri nini kutoa Tamko. Au kuna mtu KAWAZUIA
 
Kwenye uchumi wa bandari kuna masuala mengi sana na kwa bahati mbaya wengi wetu hatuyajui na tunaishia kupotoshana tu kila kukicha.

Uchumi wa bandari au kwa kingereza PORT ECONOMICS ni mnyambuliko mzima wa ukuaji wa sekta nzima ya bandari. Zipo hatua kadhaa za kufuata katika uchumi mzima wa bandari.

Kwanza kabisa inaanza kuwepo bandari ya kutoa huduma yaani SERVICE PORT ndio hii kama ya kwetu inayojishughulisha na upakuaji pamoja na upakiaji wa makasha ya wateja mbalimbali. Sisi Tanzania kwa sasa tupo katika hatua hii ya mchakato, bado sana teknolojia yetu ni ya chini na pato la ujumla linalopatikana ni la chini pia.

Ikishaanza kukua bandari inatoka katika hatua ya huduma na kuingia kwenye hatua inayojulikana kama TOOL PORT kwa maana ya bandari inayotoa huduma lakini yenye wigo mpana wa wateja wanaohudumiwa. Ikiwa Service Port inahudumia meli elfu hamsini kwa mwaka, hii Tool Port inahudumia meli laki mbili kwa mwaka.

Hatua ya tatu wa bandari ni ile inayoitwa LANDLORD PORT, ni ile ambayo mamlaka inayoendesha inafanya shughuli mbili kwa wakati mmoja, kupangisha watoa huduma na kuwa msimamizi mkuu mwendeshaji.

Nafahamu kwamba awamu ya sita imekuwa ikitamani sana kutoka hatua hizo za kwanza za uendeshaji mpaka kufikia hatua hii ya Landrord. Kwamba tunakuwa na watoa huduma wanaopangishwa moja kwa moja na TPA.

Juu kabisa kuna hatua ya kuwa na bandari mwekezaji yaani INVESTOR PORT ndio hawa kina DP World, wanayo bandari kule Jebel Ali lakini wanamiliki utoaji wa huduma katika bandari nyingi duniani. Hiyo ni hatua kubwa sana na kwa nchi zetu zenye kusikiliza wapiga miluzi wengi hakuna uwezekano wa kufikia kirahisi hatua ya kutoka hapa Tanzania na kwenda kufanya shughuli za shipping kule Port Harcout Nigeria au Beira Msumbiji.

Wanaopinga uwekezaji pale bandarini wanayajua haya masuala ya uchumi wa bandari wa karne hii tuliyopo na namna serikali inavyotaka kutuvusha kiuchumi kupitia sekta hii ya uchukuzi?. Wapo wanaokuja na hoja za wazawa kuendesha uchumi wa nchi ikiwemo bandari, vipi hao wazawa wanao uwezo wa kiteknolojia katika dunia yenye ushindani mpana wa bandari kisasa?.

Haya ni masuala ya kiuchumi na ya kimkakati. Ili uweze kupinga uwekezaji wa DPW inabidi uziongelee kwa kina hizo hatua za ufanisi za utekelezaji wa bandari nilizozitaja kwa ufupi sana hapo juu. Sio kwamba mwekezaji huyu amekuja kibahati bahati tu , hapana, ni katika michakato ya kukuza uwezo wetu wenyewe wa kuendesha bandari zetu ndio serikali ikaona umuhimu wa kuwa na kampuni pale bandarini yenye uwezo kiteknolojia. Kampuni inayotoka kwenye nchi iliyoshavuka hatua za kuwa na Service Ports mpaka kuwa na Investor Ports.

Samaki mkubwa ni lazima atamla mdogo na hii sio baharini tu hata huku kwenye maisha ya kawaida ya kibinadamu, kwa uwezo wa bandari yetu kutoka kuwa Servide Port mpaka kufikia hatua ya kuwa Investor Port ni safari ya kumwaga jasho jingi na kuwa na nidhamu pana ya kazi pamoja na ubunifu unaopewa uhuru.

Tukumbuke kuwa gati namba sifuri mpaka namba mbili ni mali ya Serikali yetu. Magati namba tatu mpaka nane yanamsubiri mwekezaji na gati namba tisa mpaka kumi na mbili yatachukuliwa na mwekezaji mwingine atakayetangazwa sambamba na mwekezaji wa bandari ya Bagamoyo.

Kusambaza waraka kuna hatari moja kubwa sana, wapo mashekhe wapole kwa hulka na wana uwezo wa kusema haya ni masuala ya muda tu na kesho kesho kutwa yameshapita. Wapo mashekhe wenye hulka hizo.

Lakini wapo mashekhe wenye misimamo mikali kina Ponda watakaokuja na mikutano wa waandishi wa habari wakihoji inakuwaje kanisa katoliki liusambaze waraka huo makanisani na serikali iyachukue maoni yao moja kwa moja!.

Mungu ni mwema naamini tutaivuka salama hii patashika inayoonekana kutaka kutokea hapa Tanzania.
 
Ni kweli madhehebu almost Yote yana exemptions, lakini wenzetu kuna na mengine nyuma ya pazia elewa hili,watu siyo wajinga kivile!
Basi serikali na vyombo vyake vya ulinzi na usalama vimeshindwa majukumu yake.

Tuwape "dipiiwedi" serikali na vyombo vyake waviendeshe ili kuleta ufanisi.
 
Binafsi sijafurahishwa na Tamko la TEC na kujivisha ukuu fulani as if wao ndio final say wa hili taifa, Hilo hatukubali kabisa, Mkataba wa DP ni Mbovu sana na haufai kabisa Kupitishwa ila kitendo cha TEC kujivisha Ukuu ile hali Taifa hili lina Rais ambae amebeba dhamana ya Wananchi wote hio swala halivumiliki kabisa.
 
Daaaah!!
Kuna watu mna guts za ajabu kweli.
Unawezaje kuhoji hayo kwa kanisa,tena Roman Catholic!!??

Hapa kuna mawili,mosi inawezekana wewe ni zero brain na uelewa wako ni wa kujua kusoma na kuandika pekee.
Pili,inawezekana unajitoa ufahamu kwa sababi fulani fulani za kimaslahi.

Vyovyote iwavyo,kanisa lina wasomi wa kila namna na kwa kila sekta tena walio wabobevu.
 
Kuwa na wasomi haimaanishi kuwa hakuna makosa yanayoweza kufanyika, kibinadamu tu.
 
TANZANIA NI KUBWA KULIKO TEC .


DP WORLD WATAENDESHA BANDARI HATA KAMA TEC WATACHUKIA.


TEC WATALIPA KODI/USHURU KWA MWARABU HAPO BANDARINI.


MIZIGO HARAMU YA TEC ITAKUWA NDO MWISHO KUPITA HAPO BANDARINI BILA USHURU NA KUTOKAGULIWA.


MUNGU IBARIKI DP wORLD [emoji289]
 
Hawana elimu kabisaπŸ˜…πŸ˜…hata walikuw hawajui kwamba TICTS alikuwa pale.

Elimu za kupewa baada ya kusujudia wazungu ndo tatizo..
 
TANZANIA NI KUBWA KULIKO TEC .


DP WORLD WATAENDESHA BANDARI HATA KAMA TEC WATACHUKIA.


TEC WATALIPA KODI/USHURU KWA MWARABU HAPO BANDARINI.


MIZIGO HARAMU YA TEC ITAKUWA NDO MWISHO KUPITA HAPO BANDARINI BILA USHURU NA KUTOKAGULIWA.


MUNGU IBARIKI DP wORLD [emoji289]
 
Ukiona wanavyojigamba Sasa na waumini wao humu jf unawedha dhani wao ndio hutuchagulia Rais au Wana hati miliki ya Nchi.

Hawa wakichekewa wanaweza amsha hisia Kali za Kidini,wakemewe
Toka lini mdini akamkemea mdini mwenzake?
Ili ukemee udini lazima uonekane NEUTRAL na watu wakujue kuwa wewe ni NEUTRAL kwa matendo yako na maisha yako kwa ujumla.
KIFUPI: Viongozi wa SERIKALI wasilazimishe mambo yenye utata katika nchi, haya mambo yenye utata ndio yanayosaidia kuwagawa WATANZANIA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…