Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC): Hatuungi mkono Mkataba wa Bandari. Sauti ya Watu ni sauti ya Mungu
Wajumbe wa Kanisa moja Takatuifu la mitume ndio hawa

leo tarehe 20 Agosti 2023

TUJIKUMBUSHE UFISADI WA KANISA NA MAASKOFU NA WACHUNGAJI



WEDNESDAY, NOVEMBER 26, 2014

HAYA NDIO MAJINA YA MAFISADI WALIOKULA FEDHA ZA ESCROW

Mh Zitto Kabwe akisoma ripoti ya ESCROW Bungeni jioni ya leo

HAYA NDIO MAJINA YA WALIOKULA FEDHA ZA AKAUNTI YA ESCROW KATIKA RIPOTI YA PAC INAYOSOMWA SASA BUNGENI.




Zitto:

Upande wa viongozi wa kisiasa ambao waliingiziwa fedha katika akaunti zao binafsi ni;

1. Mhe.
Andrew Chenge (Mb)
Zitto: Andrew Chenge aliingiziwa shilingi bilioni 1.6.


2. Mhe. Anna Tibaijuka (Mb) na Waziri wa 62
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi shilingi bilioni 1.6.


3. Mhe.William Ngeleja (Mb) na ambaye alikuwa Waziri wa Nishati na Madini alipewa shilingi milioni 40.4


4. Ndg. Daniel N. Yona ambaye alikuwa pia Waziri wa Nishati na Madini alipewa shilingi milioni 40.4.


5. Ndg. Paul Kimiti ambaye ni Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Sumbawanga
alipewa shilingi milioni 40.4

6. Dr. Enos S. Bukuku ambaye alikuwa Mjumbe wa Bodi ya TANESCO aliingiziwa shilingi milioni 161.7.


Zitto : Upande wa Majaji Prof.


7. Eudes Ruhangisa, aliingiziwa milioni 404.25 na

8. J.A.K Mujulizi aliingiziwa shilingi milioni 40.4


Zitto: kwa upande wa Watumishi wa umma

9.,Ndg. Philip Saliboko ambaye alikuwa mtumishi wa RITA aliingiziwa
shilingi milioni 40.4

10 Ndg. Emmanuel Daniel Ole Naiko ambaye
alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa (TIC) aliingiziwa shilingi milioni 40.4

11. Ndg. Lucy L. Appollo ambaye ni Mtumishi wa TRA aliingiziwa shilingi milioni 80.8.


Zitto:

Viongozi wa Madhehebu
yaDini

walioingiziwa fedha na Benki ya Mkombozi ni Askofu 63

12.Methodius Kilaini shilingi 80.9


13. Askofu Eusebius Nzigirwa shilingi milioni 40.4 na

14. Mchungaji Alphonce Twimann Ye Simon shilingi milioni 40.4.



Zitto: Watu walienda kugawana fedha kwenye Benki tajwa wakiwa na mifuko ya rambo, sandarusi,
mabox, magunia na lumbesa TegetaEscrow
Zitto: Bilioni 73.5
zilitolewa na kugawanywa kwa watu mbalimbali kinyume cha
Sheria ya Benki Kuu na Taasisi za Fedha ya 2006
Zitto: Taarifa
ya benki (bank statements) yenye majina na akaunti zote
zilizoingiziwa fedha zimeambatishwa
Mwambie akutajie waligawana za kwenye Sandarusi 😂😂

Zitto alinyimwa mgao na Rugemalira ndio akatengeneza Zengwe kwa kumshirikisha Tumbiri
 
Tatizo mnajibu hoja bila hata ya kusoma na kuelewa kilichoandikwa.

Kwanza ufute maneno yako kuwa eti wananchi wote wanawakilishwa na wabunge. Hoja yako ingekuwa sahihi kama hao wanaoitwa wabunge kama kweli wangekuwa walichaguliwa na wananchi. Hawa wanaoitwa wabunge, ni majizi ya kura, na wengine hawakuchaguliwa wala hata kuwa na kura hata moja ya mtu yeyote, tena miongoni mwao akiwemo Waziri Mkuu. Kiuhalisia wananchi hawana mwakilishi yeyote.

Jambo la pili unatakiwa kufahamu kuwa, hata kama tungekuwa na bunge, bado kuna taasisi mbalimbali ambazo kupitia kwazo, watu wa makundi mbalimbali wanawakilishwa. Taasisi hizo ni pamoja na taasisi za kidini, taasisi za kiweledi (kama vile vyama vya madaktari, wahasibu, wanasheria, wahandisi, wakulima), vyama vya makundi maalum, vyama vya wafanyakazi, n.k. Hizi taasisi zote ni taasisi ambazo zipo karibu zaidi na wanachama wao kuliko hata mbunge. Ndiyo maana taasisi hizi, zina uwezo wa kushauri, kutetea, kuonya, kukosoa na hata kupinga, japo hawana mamlaka ya kufanya maamuzi ambayo serikali inalazimika kutimiza.

Tumeona, wakati wa utawala wa Mwinyi, kupitia BAKWATA, waislam waliitaka Serikali iwaruhusu wanafunzi wasichana kuvaa mashuleni mavazi yanayoendana na imani yao. Baadaye Serikali ikaridhia. Kama kungekuwa na wajinga, wanaofikiria kwa namna kama yako, wangesema kuwa BAKWATA haina mamlaka ya kufanya maamuzi na kisha kupeleka matakwa ya waislam Serikalini.

TEC wamesema wazi kuwa wana mfumo wao wa kupata maoni ya waumini wao toka ngazi ya kaya mpaka Taifa, na kwa utafiti wao, wananchi walio wengi hawataki huo mkataba wa hovyo uliosainiwa na Serikali na kisha kupitishwa na bunge haramu. Nasema ni bunge haramu kwa sababu ni zao la uovu.

UTAMBUE
Wananchi wote, mmoja mmoja au kwa kupitia taasisi zao wana haki ya kukosoa, kupinga, kukataa, kushauri au hata kulaani au kupongeza maamuzi ya Serikali. Ambaye halijui hili, ni dhahiri itakuwa ni kwa sababu ya ujinga wake.
ibara ya 8, 16, 18 21, 26, na 27 ya Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania, ya 1977 inawapa nguvu ambazo pia wewe unazo kama mwananchi mkuu, kupia ibara hizo tajwa.
 
Nakushaur tu jambo.. jaribu kutafuta CV ya kila askofu angalau kwa uchache tu nadhan utarud hapa na kubadili msimamo wako!! Wale jamaa wana elimu ya vyuo vikuu faculty tofaut tofaut!!
Hata Profesa Shivji mliamini kumpinga ni sawa na kutenda dhambi, akaja kukosolewa mbele ya kamera za waandishi wa habari. Usitishwe na CV za watu, kuna masuala hawayajui.
 
Labda akiwaona walivyovaa yale mavazi yao ya Misa anaona wanachojua ni Biblia tu. Sijui analichukuliaje Kanisa.
Mimi ni mkatoliki ambaye wazazi wangu wote wawili ni wale wakatoliki waliojitolea kulea mapadre wawili miaka ya nyuma. Nimekulia kwenye nyumba yenye ukatoliki kindakindaki.
 
Kaka unajua wengi wameahamia ulikole, je unajua wangapi wamejiunga na roman Catholic kutoka ulokole?

Tuache ufala hii sio Mali ya msonga gang ni Mali ya tz
 
Hivi huko Shule I ,Huwa mnaenda KUFUNDISHWA Ujinga .


Bandari inajieleza, mchango wake kiuchumi unajieleza.

DP W tunaijua, Uwezo wake tunaujua.



Watanzania Tunapinga AINA YA MKATABA, MKATABA UMEPINGWA NA KILA KUNDI .



kwan Nchi hii hamna wawekezaji??.
 
Wao ndio waelimishaji sasa ulitaka waelimishwe na nani, na wewe ama?
Usitishwe na hizi PHD au hawa maprofesa ukadhani wana akili nyingi sana, wana uelewa na ufahamu kwenye baadhi tu ya masuala haswa yale wanayosomea lakini kwingine ni watupu tu.
 
Tena na JPM alishasema muhimili wake ndo umeenda mbali sana. Jiulize, nani anateuwa jaji?
JPM alishawahi kuwabeza vibaya sana waandika waraka, Akaudharau waraka wao na waandika waraka pia. JPM alikuwa anafahamu wakoloni wanalitumia kabisa vibaya kwa kazi zao kwenye nchi husika.
 
Hujaelewa hata swali. Nadhani uwezo wako ni duni sana.

Nikusaidie tu:

Escrow au Escrow akaunti, ni akaunti ambayo hufunguliwa na upande unaodaiwa pale unapotakiwa kuulipa upande wa pili, lakinj mlipaji haafiki juu ya kiwango cha malipo anayodaiwa. Hivyo hufunguliwa ili anayedaiwa aendelee kulipa wakati uamuzi wa uhalali wa malipo unasubiriwa. Na Escrow akaunti kwa hapa kwetu ilikuwa inasimamiwa na BOT. Je, ni nani aliyeruhusu malipo yafanyike kama madai hayakuwa halali?

Pesa ya Escrow ilikuwa ni halali yao waliokuwa wanadai na ndiyo maana walilipwa, na mpaka leo hakuna aliyehukumiwa kwa kosa lolote. Waliopewa pesa na Rugemarila, baadhi yao, kosa pekee walilokutwa nalo ilikuwa ni kutokulipia kodi. Sheria zetu zinasema kuwa hata ukipewa zawadi, uende ukalipie kodi. Je, ni wangapi huwa wanatekeleza sheria hiyo?
Uwe unasoma page zote za uzi kabla ya ku comment. Ilo jibu lilishstolewa na ameulizwa maswali amekimbia
 
Mimi ni mkatoliki ambaye wazazi wangu wote wawili ni wale wakatoliki waliojitolea kulea mapadre wawili miaka ya nyuma. Nimekulia kwenye nyumba yenye ukatoliki kindakindaki.
Samahani mkuu, huna UNALOJUA kuhusu UKATOLIKI. Hili ni moja.

Pili, sababu ya mkataba au makubaliano kuwa kwenye maandishi, ni kuhakikisha kila mtu atakayesoma aelewe, maana ile iliyokusudiwa! Uwezo wa uelewa wa mtu na mtu hutofautiana na hivyo TAALUMA kadhaa huusishwa kuleta maana moja ya mkataba husika.

Taaluma ya sheria ina fanana sana na maandiko ya biblia, ndio maana wanataaluma tofauti wana tafsiri tofauti, kama ilivyo kwa wanazuoni!

Maaskofu wa catholic, wamegonga kona zote kabla ya kutoa tamko, wameshaotea moves zote zitakazojitokeza baada ya tamko, wameshaanda jinsi ya kufanya kwa kila move kwa kuzingatia impact halisi.

Sasa, tunachofanya ni kucheza kwenye muziki wao!

Mwisho, akili ni kile kinachobaki baada ya kuondoa madarasa uliyonayo kichwani!
 
Hivi huko Shule I ,Huwa mnaenda KUFUNDISHWA Ujinga .


Bandari inajieleza, mchango wake kiuchumi unajieleza.

DP W tunaijua, Uwezo wake tunaujua.



Watanzania Tunapinga AINA YA MKATABA, MKATABA UMEPINGWA NA KILA KUNDI .



kwan Nchi hii hamna wawekezaji??.
Kupingwa na kila kundi kunategemea na uelewa wetu wa jumla na namna tunavyoelimishwa.

Wajuzi wa sheria wameuelezea huo mkataba kila kipengele chake kina maana gani.
 
Back
Top Bottom