Hapo unajaribu kufananisha vitu ambavyo haviendani kabisa, ngono na umasikini ni vitu viwili tofauti, ngono ni tendo na umasikini ni hali
Na ili ngono ifanyike lazima ihusishe jinsia mbili, wakati umasikini ni kitu individual, ambacho hakisababishwi na jinsia
Sasa inapotokea tendo ambalo linahusisha jinsia mbili, halafu moja inasifiwa nyingine inapondwa kana kwamba hilo tendo kila jinsia inafanya na viumbe wengine tofauti, inakuwa haimake sense yani
Unapomuambia mwanamke ajitunze automatically unamaanisha na mwanaume naye ajitunze, maana wanawake wakiamua kujitunza wanaume watakosa wanawake wa kufanya nao, hivyo nao watajikuta wanalizimika kujitunza vile vile
Lakini unapomuambia mwanamke ajitunze halafu mwanaume asijitunze, maana yake unamuambia mwanaume yeye kuendelea kutongoza na kubadilisha wanawake ni sawa tu, lakini unasahau kwamba hao wanawake atakaowatongoza na kuwabadilisha ndio hao hao unaowaambia wajitunze tena