PreGE2025 Lissu: Uchaguzi hautafanyika wananchi mkakubaliana na msimamo wetu mkaandamana siku ya uchaguzi

PreGE2025 Lissu: Uchaguzi hautafanyika wananchi mkakubaliana na msimamo wetu mkaandamana siku ya uchaguzi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Mitaa ipi hiyo kuna wanachama wengi wa Chadema?? Uchaguzi wa mwaka jana ulikuwepo TZ au uko nje ya TZ mkuu?
Hawa wameshajua watashindwa kwenye sanduku la kura,sasa,wanatapa tapa.Umzuie mtu na haki yake,wafikiri atakuachia hivi hivi.
 
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu amesema siku ya uchaguzi mkuu utakaofanyika baadaye mwaka huu, chama hicho kitaitisha maandamano ya kuuzuia uchaguzi usifanyike.

View attachment 3296017
Kauli hiyo ya Lissu, inajibu swali kuhusu mbinu ambayo chama hicho itaitumia kuzuia uchaguzi kuendana na ajenda yake ya 'No Reforms, No Election' (bila mabadiliko, hakuna uchaguzi).

Lissu amesema hayo leo, Jumatatu Aprili 7, 2025 wakati akihutubia mkutano wa hadhara Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara katika ziara ya kutoa elimu kuhusu 'No Reforms, No Election.'

View attachment 3296018Amesema iwapo Serikali haitafanya mabadiliko ya sheria na kanuni za uchaguzi, chama hicho kitawahamasisha wananchi kuandamana kuuzuia uchaguzi usifanyike.

"Hatutaenda kupiga kura, hatutaenda kujiandikisha, siku ya kupiga kura tutaandamana, watatufunga wote? Kuna sheria ya Tanzania inayosema lazima tushiriki kwenye chaguzi za kijinga?" amehoji.

Chanzo: Mwananchi
We huyo kibaraka amkalete mkewe na watoto wake kutoka Marekani halafu waandamane hakuna mtanzania mwenye akili ataandamana. Asimjaribu mama yetu atulize hayo makalio yake atafanywa kitu kibaya sana
 
Eti na ukilema wake huo!
Ukilema siyo shida kwasababu amepewa na watu makatili wasio na maana

Shida ni kwamba anaongea sana na kutenda kiduchu

Sanasana atakwenda Belgium Kwa mabwana zake
 
Wataandamana katika kila mji au kila kitongoji? Na maandamano yatazuiaje uchaguzi wakati kabla ya maandamano wanatakiwa kutoa route na sababu kwa Tanpol? Na je CDM itawakatalia watia nia kama yeye kujaza na kurudisha fomu za uteuzi?

Amandla...
 
Maandano hayawezekani, hii nchi ni ya wanawake tupu
Kweli?

Kwahiyo wanawake mna sperms na mnazalishana kutwa kucha sio?

Acha kujdhalilisha

Hakuna maandamano vecause hakuna hoja… domokaya mwenyewe ni rainbow national
 
Kushindwa kwenye sanduku la kura ndio huku
Hawa wameshajua watashindwa kwenye sanduku la kura,sasa,wanatapa tapa.Umzuie mtu na haki yake,wafikiri atakuachia hivi hivi.
 

Attachments

  • 6021057-0f909c697d438e92943259338c363da.mp4
    7.7 MB
  • 6021056-bf15b8f6f927c72fa16d6bb328a5e41.mp4
    14.1 MB
  • 6021175-479b15392d489294edae554034bf610.mp4
    579.6 KB
  • 6016899-46d1e509592bd73d8313972ca4ec270.mp4
    805.6 KB
  • 5833465-c90487a0a3c9f670172c401e803cbac.mp4
    3.5 MB
  • 5810727-156c33252d331784831e630b50148de.mp4
    2 MB
Maandano hayawezekani, hii nchi ni ya wanawake tupu
Sio wanawake
wao wenyewe familia zao zipo nje, uje uniambie nikaandamane na nikusikilize,utakua mzima kichwani kweli wewe?

Haiingii akilini hii
 
polisi wasimzuie wamwache aandamane kuzuia nasie tuandamane kumzuia asituzuie, ila aturudishie kwanza passport yetu asijetutoroka
shida ni kwamba hyo kampeni ya no reform no election ni hoja ya chadema peke yao.sio vyama vya upinzani.mzozo unakuja hapo.wewe kama hautaki uchaguzi acha usishiriki ila usiseme nitazuia.mana wapo wenzio wanaoutaka
 
Wakati chadema ikiendelea kuandamana siku ya uchaguzi mkuu,CCM ,itakuwa inaendelea,kuhesabu kura halali na za wizi.
Matokeo yake, chadema itakosa wabunge nchi nzima na Madiwani Nchi nzima!
Ukitangaza maandamano siku ya kupiga kura maana yake siku hiyo wengi hawatatokea kupiga kura kuogopa vurugu.Polisi badala ya kulinda vituo vya kura watakua busy kupambana na waaandamanaji. Automatically uchaguzi hautafanyika.Sijui kama kuna mwenye akili TIMAMU ataenda kupanga foleni katikati ya vurugu eti awachague CCM.
 
Back
Top Bottom