Mdogo wangu Eeh! Kuoa mwanamke ambaye familia yake imekuzidi kila kitu ni mtihani sana. Usithubutu!

Pole na hii changamoto Mkuu, Kuna Mshikaji wangu naye aliowa mwanamke Familia inajiweza (Mwanamke familia yake ina undugu na Mama Salma Kikwete) na mbaya zaidi jamaa alitoka kwao akahamia ukweni, Jamaa alianza kulipishwa mpaka kodi ya Chumba anacholala na Mke wake, hakutoboa miezi 10 tu jamaa akanyoosha mikono.
 
Kuna mmoja juzi kati sijui FB au humu alileta nyuzi akapendekeza vijana wa kiume wajitahidi kuji-attach kwenye familia za Kitajiri kama alivyofanya Isaya ili watoke kimaisha. Sasa na wewe leo umekuja na lingine. Mbona mnatuchanganya!
 
Milioni 8 na laki na hamsini ilipungua laki wakataka kuturudisha tulikotoka bila busara za wale wazee wangu ndoa isingekuwepo
Kwa jinsi ninavyojifahamu ningempa akaunti namba aingize huo mpunga. Ningeondoka zangu.
Zingepita siku tatu hajaweka mpunga namrukia hewani kudai.

Wanaume hatudharauliani, wanaume tunashauriana.

Ikishafika kwenye suala la ndoa, sisi wote ni wanaume na mwanamke inabidi amtii mumewe.
 
Focus kuelewana na kuiweka vizuri familia (mke na watoto wako) hao wengine achana nao, kama wanakudharau acha kwenda kwenye shughuli zao na uwe more independent,heshima itarudi
 
NImegundua kati ya wanaume 100 waliooa wanawake ambao wanatoka familia za kitajiri ni wanaume wachache sana wanaoishi kwa furaha waliobaki huwa mandondocha
Hakuna ata mmoja. Ata kama mwanamke akikupenda na akawa anakupa mshahara wake. Kuna vikao vya kifamilia ukialikwa ukwen utagundua wewe ni useless..... Na watoto wako watakuwa na mapenzi na ukweni si unajua Generation Alpha haitaki shida. Kwenye urahisi ndio wanapopenda.
 
Kuna tofauti kati ya Mke/Mume wa kujitafutia mwenyewe na Mke/ Mume wa kupewa na Mungu.

Ukijitafutia mwenyewe jiandae kwa lolote wakati wowote!
 
Kuna tofauti kati ya Mke/Mume wa kujitafutia mwenyewe na Mke/ Mume wa kupewa na Mungu.

Ukijitafutia mwenyewe jiandae kwa lolote wakati wowote!
 
Kijana izo ishu mbona ni ndogo sana!
Ndoa ume sema ina miaka 4 je mmesha zaa?
Kama mna kaa week/Mwezi hupewi unyumba usipaniki usiombe mpaka aombe yeye
Tafuta mchepuko punguza upwiru anza kupiga tungi kula uko uko bar ukirudi Lala
Usiulize habari ya msosi Wala usi hangaike nae ata jirekebisha tu mwenyewe.
 
Si uwaambie warudishe mali au mali kaeni nazo na mtoto wenu kaeni naye, mbona wanawake wako chungu nzima, hizo dharau mimi nisingesubiri hata kuja kuomba ushauri, zaidi zaidi labda ningeutoa tu taarifa.

Maisha ni mafupi sana hakuna haja ya kuishi kwa stress ya namna hiyo, dharau za wazi wazi zipinge Mkuu. Usikute hapo hata mtoto wao ana support huo ujinga na hapo hapo anataka aendelee kuishi na wewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…