Mm nadhani angejikita kwenye tozo za mafuta na kuachana na za benk ama kupunguza kdg zile mabenk ila kwenye mafuta wangepunguza kbsa au kufuta kbsa maisha yaendelee mnk Bei ya mafuta ipo juu imepelekea bidha kupanda sokoniVipi tozo kwenye mafuta imeondolewa? Maana hiyo ndo inapandisha kila kitu
Tengeneza tatizo kisha litatue uonekane msikivu. Watu wanalipa kodi, hizo tozo ni za kazi gani?KAZI nzuri ya CCM. Imesikia kilio hiki. Tozo sio tatizo lakini shida Ilikuwa ni kiwango Cha tozo.
Hakuna nchi duniani inaweza kuhudumia watu wake bila kulipa Kodi na tozo zinazostahili. Hata kama ni chadema(japo waameishiwa hoja) wakibahatika kupata serikali labda kuanzia miaka ya 2150 watatoza tozo.
Nimpongeze sana bwana nchemba Kwa kusikia kilio hiki na maelekezo ya CCM.
Huyu jamaa ana tuona sisi Watanzania kama ni wajinga, nyumbu! Au ana tuonaje? Hizi tozo anazo sema amezifuta sidhani kama ndizo zilizo lalamikiwa. Maana hizi hazija futwa bado zipo. Nafikiri kuna haja ya huyu jamaa kujiuzulu.Akizungumza leo bungeni, Waziri wa Fedha na Mipango Mwigulu Nchemba amesema uongezwaji wa wigo wa kukusanya mapato kupitia tozo uliibua malalamiko kwenye jamii, hivyo Kamati kuu ya Chama cha Mapinduzi iliagiza upitiwaji upya wa tozo hizi na kuzingatia maoni ya wananchi.
Marekebisho yafuatayo yamefikiwa-
Kufuta tozo ya kuhamisha fedha kutoka benki kwenda mitandao ya simu kwa pande zote. Kufuta tozo ya kuhamisha fedha ndani ya benki moja na kutoka benki moja kwenda benki nyingine. Kutowahusisha wafanya biashara wadogo (merchants) kama ilivyokuwa kweye kanuni ya sasa. Kusamehe tozo ya miamala kwenye utoaji wa fedha taslimu kupitia wakala wa benki yaani ATM kwenye miamala yenye thamani ya chini ya tsh 30,000/= Kupunguza gharama ya miamala kwa asilimia 10-50 kutokana na makundi ya miamala
Marekebisho haya yataanza kufanya kazi Octoba 1, 2022. Aidha Serikali itafuta utaratibu wa kodi ya zuio ya pango inayotaka kukusanywa na mpangaji, hivyo kwa sasa itapaswa kulipwa na mmiliki wa nyumba na siyo mpangaji.
Kwa kuwa pesa hizi zitaipunguzia mapato serikali, Waziri ameelekeza Serikali ianze kubana matumizi yake mfano kwenye vikao, mafunzo ya semina, warsha, safai za ndani na nje, misafara, kukagua miradi n.k
Wataalamu wa wizara ya fedha na mipango ndiyo wamefanya mapitio haya wakiwa ofisini kwa kuwa ni sehemu ya majukumu yao. Taarifa za kuwa kuna tume iliundwa kutoka nje ya wizara ni uzushi.
Pumbavu kabisa!KAZI nzuri ya CCM. Imesikia kilio hiki. Tozo sio tatizo lakini shida Ilikuwa ni kiwango Cha tozo.
Hakuna nchi duniani inaweza kuhudumia watu wake bila kulipa Kodi na tozo zinazostahili. Hata kama ni chadema(japo waameishiwa hoja) wakibahatika kupata serikali labda kuanzia miaka ya 2150 watatoza tozo.
Nimpongeze sana bwana nchemba Kwa kusikia kilio hiki na maelekezo ya CCM.
Wangapi wanalipa Kodi. Tozo ndio suluhu Kwa wakwepa Kodi. Ni sawa na Simba kumvizia nyumbu kwenye bwawa la maji. Nchi zingine watu hujisikia fahari kulipa Kodi.Tengeneza tatizo kisha litatue uonekane msikivu. Watu wanalipa kodi, hizo tozo ni za kazi gani?
Sasa wewe ndugu nakuuliza msimamo wako haswa ni upi, tozo zilipwe au ziondolewe? Hebu jifikirie unataka na unapenda nini kuhusu tozo???Unajua wangapi wanalipa Kodi kati ya wanaostahili kulipa?. Je njia rahisi ni ipi ya kuwafanya walipe pia?
Tozo zilipwe na tozo ziwe rafiki na Ili mzigo wa Kodi usiwaelemee wafanyakazi tuSasa wewe ndugu nakuuliza msimamo wako haswa ni upi, tozo zilipwe au ziondolewe? Hebu jifikirie unataka na unapenda nini kuhusu tozo???
Sasa kwanini unampongeza Mwigulu kwa kuziondoa?Tozo zilipwe na tozo ziwe rafiki na Ili mzigo wa Kodi usiwaelemee wafanyakazi tu
Akijiuzuru kuna ugali utakuja kwako?Ajuizulu tu. Bogus kabisa.
Umeaisahau JYT (Jamhuri ya Twitter)JF inastahili pongezi kwenye hili.. Huu ni ushindi wa mwanzo tuu tuje sasa kwenye tozo za miamala ya simu
Hakuna sababu ya Rais kuandamana na watu wengi wasio na maana. Ulinzi mkubwa usio na maana wakati bajeti zetu bado za mikopo na misaadaWazungu wameshatowa somo namna ya kubana matumizi, hizo V8 ziuzwe Mara moja.