Mwigulu Nchemba: Tumefuta baadhi ya tozo, nyingine tumepunguza kwa asilimia 10-50
Vipi tozo kwenye mafuta imeondolewa? Maana hiyo ndo inapandisha kila kitu
Mm nadhani angejikita kwenye tozo za mafuta na kuachana na za benk ama kupunguza kdg zile mabenk ila kwenye mafuta wangepunguza kbsa au kufuta kbsa maisha yaendelee mnk Bei ya mafuta ipo juu imepelekea bidha kupanda sokoni

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
KAZI nzuri ya CCM. Imesikia kilio hiki. Tozo sio tatizo lakini shida Ilikuwa ni kiwango Cha tozo.

Hakuna nchi duniani inaweza kuhudumia watu wake bila kulipa Kodi na tozo zinazostahili. Hata kama ni chadema(japo waameishiwa hoja) wakibahatika kupata serikali labda kuanzia miaka ya 2150 watatoza tozo.

Nimpongeze sana bwana nchemba Kwa kusikia kilio hiki na maelekezo ya CCM.
Tengeneza tatizo kisha litatue uonekane msikivu. Watu wanalipa kodi, hizo tozo ni za kazi gani?
 
1. Maeneo mengi nchini machinga wamerudi kwa speed Kali kwenye maeneo ya zamani Mf. Buhongwa Mwanza. Bado viongozi wanasikilizia mitandao inashauri wafanyeje.

2. Leo unaweka tozo za hovyo hovyo, unasikiliza reaction mitandaoni,kesho unaziondoa kwa mbwembwe.
 


Akizungumza leo bungeni, Waziri wa Fedha na Mipango Mwigulu Nchemba amesema uongezwaji wa wigo wa kukusanya mapato kupitia tozo uliibua malalamiko kwenye jamii, hivyo Kamati kuu ya Chama cha Mapinduzi iliagiza upitiwaji upya wa tozo hizi na kuzingatia maoni ya wananchi.

Marekebisho yafuatayo yamefikiwa-
  • Kufuta tozo ya kuhamisha fedha kutoka benki kwenda mitandao ya simu kwa pande zote.​
  • Kufuta tozo ya kuhamisha fedha ndani ya benki moja na kutoka benki moja kwenda benki nyingine.​
  • Kutowahusisha wafanya biashara wadogo (merchants) kama ilivyokuwa kweye kanuni ya sasa.​
  • Kusamehe tozo ya miamala kwenye utoaji wa fedha taslimu kupitia wakala wa benki yaani ATM kwenye miamala yenye thamani ya chini ya tsh 30,000/=​
  • Kupunguza gharama ya miamala kwa asilimia 10-50 kutokana na makundi ya miamala​

Marekebisho haya yataanza kufanya kazi Octoba 1, 2022. Aidha Serikali itafuta utaratibu wa kodi ya zuio ya pango inayotaka kukusanywa na mpangaji, hivyo kwa sasa itapaswa kulipwa na mmiliki wa nyumba na siyo mpangaji.

Kwa kuwa pesa hizi zitaipunguzia mapato serikali, Waziri ameelekeza Serikali ianze kubana matumizi yake mfano kwenye vikao, mafunzo ya semina, warsha, safai za ndani na nje, misafara, kukagua miradi n.k

Wataalamu wa wizara ya fedha na mipango ndiyo wamefanya mapitio haya wakiwa ofisini kwa kuwa ni sehemu ya majukumu yao. Taarifa za kuwa kuna tume iliundwa kutoka nje ya wizara ni uzushi.
Huyu jamaa ana tuona sisi Watanzania kama ni wajinga, nyumbu! Au ana tuonaje? Hizi tozo anazo sema amezifuta sidhani kama ndizo zilizo lalamikiwa. Maana hizi hazija futwa bado zipo. Nafikiri kuna haja ya huyu jamaa kujiuzulu.

Au mamlaka ya uteuzi umtoe.
Ana jaribu kucheza na akili za Watanzania. Ana mharibia Mh Rais na serikali yake. Amekataa kutii maagizo ya chama chake. Bado wabunge wa kubebwa hawaja ona hilo changa la macho wana mpigia makofi!

Shame shame shame on youu!!!
 
KAZI nzuri ya CCM. Imesikia kilio hiki. Tozo sio tatizo lakini shida Ilikuwa ni kiwango Cha tozo.

Hakuna nchi duniani inaweza kuhudumia watu wake bila kulipa Kodi na tozo zinazostahili. Hata kama ni chadema(japo waameishiwa hoja) wakibahatika kupata serikali labda kuanzia miaka ya 2150 watatoza tozo.

Nimpongeze sana bwana nchemba Kwa kusikia kilio hiki na maelekezo ya CCM.
Pumbavu kabisa!
 
Tengeneza tatizo kisha litatue uonekane msikivu. Watu wanalipa kodi, hizo tozo ni za kazi gani?
Wangapi wanalipa Kodi. Tozo ndio suluhu Kwa wakwepa Kodi. Ni sawa na Simba kumvizia nyumbu kwenye bwawa la maji. Nchi zingine watu hujisikia fahari kulipa Kodi.

Tofauti na watu wa ufipa. Wafanyakazi wanakatwa Kodi lakini utakuta jitu kubwa Zima Lina mihela na majumba Kila mtaa lakini tin number halina
 
Unajua wangapi wanalipa Kodi kati ya wanaostahili kulipa?. Je njia rahisi ni ipi ya kuwafanya walipe pia?
Sasa wewe ndugu nakuuliza msimamo wako haswa ni upi, tozo zilipwe au ziondolewe? Hebu jifikirie unataka na unapenda nini kuhusu tozo???
 
Serikali sikivu ya Rais Samia Suluhu Hassan ilisikiliza maoni ya wananchi kuusu suala la Tozo na imefanyia kazi maoni ya wananchi kwa kufuta na kupunguza tozo.

Waziri wa fedha Dr Mwiguru Nchemba amesema leo bungeni kwamba hizi ni baadhi ya sehemu zilizofanyiwa kazi;

-Kufuta tozo ya kuhamisha kutoka benk kwenda mitandao ya simu (pande zote).

-Tozo ya kuhamisha fedha ndani ya benki moja.

-Kufuta tozo ya kuhamisha fedha kutoka benk moja kwenda nyingine.

-Wafanyabiashara (merchats) hawatahusishwa kama ilivyo kwenye kanunu za sasa.

-Kusamehe tozo ya miamala kwenye utoaji wa fedha taslimu kupitia wakala wa benk na ATM kwa miamala yenye thamani isiyozidi shilingi 30,000.

-Kupunguza gharama ya miamala kwa asilimia 10 hadi asilimia 50 kufuatana na kundi la miamala. ikumbukwe kuwa tozo hizo ambapo viwango vya tozo vilishushwa kwa asilimia 30 kutoka kiwango cha juu cha shilingi 10,000 hadi kiwango cha juu cha shilingi 7,000 viwango ambavyo vilianza kutumika tarehe 7 September 2021.
Mheshimiwa Rais Samia Suluhu alisisitiza kupunguzwa zaidi tozo ambapo wizara ya fedha ilipunguza tozo zaidi kwa kushusha tena kiwango cha juu kutoka 7,000 hadi 4,000.

Rais Samia Suluhu alisema lengo lake ni "KUMUINUA MWANANCHI NA SIO KUMDIDIMIZA" mwenyezi Mungu aendelee kumuongoza
 
Sasa wewe ndugu nakuuliza msimamo wako haswa ni upi, tozo zilipwe au ziondolewe? Hebu jifikirie unataka na unapenda nini kuhusu tozo???
Tozo zilipwe na tozo ziwe rafiki na Ili mzigo wa Kodi usiwaelemee wafanyakazi tu
 
Serikali iachane na VX, ianze nunua Prado zinawatosha...
Misafara ipunguzwe

Ujenzi wa maofisi dodoma usitishwe kwa muda
 
Wazungu wameshatowa somo namna ya kubana matumizi, hizo V8 ziuzwe Mara moja.
Hakuna sababu ya Rais kuandamana na watu wengi wasio na maana. Ulinzi mkubwa usio na maana wakati bajeti zetu bado za mikopo na misaada
 
Back
Top Bottom