Rais Samia apandishwa Basi huko London kwenye Msiba wa Malkia Elizabeth II
Punguzeni chuki, kule kama hujachanja huingii.
Mara nyingi nimekuambia HUNA AKILI, Mama Samia atavaa barakoa kulingana na jinsi siku hiyo ilivyo. Na sio sababu uingereza wote wamechanja. Hapa nyumbani tu mara nyingi havaagi, au napo wote tumechanja??
Picha chini ni juzi alipokua kwenye kongamano JNICC
20220919_140358.jpg
 
Kwa hiyo uklitaka apande nini? Kama Ruto tu na upya wake anapanda Bus yeye ni nani mpaka asipande bus? Sukuma Gang bado mna mhaho!
Yeye ni Raisi wa nchi tajiri Magufuli alisema tutembee kifua mbele nchi yetu Tajiri.
 
Biden tu ndio yuko exempt kwa usalama maana maadui ni wengi

Hii Habari aliitoa waziri kuwa ili kupunguza msongamano hata Heathrow haikutumika kwa kupokea wageni mashuhuri
Na pia waliambiwa waje wachache sana yaani kama ni Rais na mke/mume tu na wachache sana
Wote wametua Luton na Stansted na helicopter marufuku

Kupandishwa bus ni sawa tu kupunguza msongamano
La sivyo barabarani tusingepita
Ila na humo kama kuna adui yako ni nkonzi tu haha
 
Afrika bhn Sasa Kila rais angepewa usafir Wake binafsi ingekuwa fujo na kazi zisingefanyika maana idadi ya polisi haitoshi wamechuka sehemu tofauti Ila nimependa
Uache uongo, Wala kusingekua na fujo yoyote na inawezekana kabisa kila raisi kupewa usafiri wake maana hata kwenye mikutano ya UN hufanyika hivyo

Japo sioni issue wakipanda bus ikiwa wenye msimba wameamuaa utaratibu uwe hivyo
 
Wakati watu kama akina magufuli wanapambana kutahiri fikra zetu,mbuzi kadhaa wakawa wanambeza,mbaya zaidi wengine wanatunzwa na hawa hawa wanaotudharau.

Anyaway as long as wote wamewekwa ktk bus,nadhani watakuwa wametumia wasaa huo kutafakari kwa pamoja juu ya namna wanavyochukuliwa na hao watu.
Mbona ndege wanapanda??? Jamani sie wamatumbi fikra zetu ndio shida kuna viongozi zaidi ya 500 unataka kila mtu apande gari lake na walinzi wake lukuki na wasio na tija.
Hili ni somo atakaporudi nyumbani ile misafara ya V8 zaidi ya 50 aachane nao gari 2 latatu basi mkaramo.
 
Back
Top Bottom