Rais Samia apandishwa Basi huko London kwenye Msiba wa Malkia Elizabeth II
Hili ni swali la msingi
..watolee ufafanuzi kwanini Rsisi akisafiri huagwa na kupokewa uwanja wa ndege na utitiri wa viongozi wanaoendeshwa kwenye ma-V8.

.. Kwanini viongozi hao wasipande basi maalum kwenda kumuaga au kumpokea Raisi uwanja wa ndege?
 
Hili jambo wala halihitaji ufafanuzi, wengi wanaolishupalia exposure hakuna.

Viongozi wa nchi zengine mf. China, France, Germany, Brazil, etc. wamepanda mabasi na wala haijawa issue kabisa, ila bongo imekuwa big topic.

Tukiendelea na hizi mentality, hawa mafisi wa kijani watatutawala mapaka Yesu au mtume arudi
Weka kapicha basi mkuu
 
Huyu mwamba angekuwepo angeingia kabebwa,sijui kwa nini tulimtoa?

EOrBXayWkAAQMtn.jpg
 
Hii mada mbona ni ya kitoto sana kiasi cha serikali kuitolea maelezo. Hapo kuna rais wa Kenya pembeni, ina maana na wao serikali itatoa maelezo?.

UK ni ndogo na ratiba ni ngumu siku zote muda hautoshi, hivyo wakaamua wapunguze msongamano kwa kuwapandisha mabasi kwa ajili ya kuwasafirisha baadhi ya wageni.
Hata parking hakuna
 
Watu mna kiherehere shida iko wapi, marais wengi tu wamepanda bus maalum, isipokuwa Biden na PM wa Israel, aibu ni ipi hapo?
Kwenda huko umeona kiongozi gn wa G7 kapanda hizo daladala?
 
Wewe ndiyo usiyekuwa na ufahamu kuhusu kitu kinaitwa "Power Relations" kwenye nyanja mbalimbali na hasa linapokuja kati ya taifa na taifa na athari zake.

Kuna siku Obama alienda Saudi Arabia halafu akajiinamisha chini ya mfalme wa Saudia, wamarekani waling'aka hapana mfano.

Kuna stori (sijui kama ni kweli maana sikuwepo) kwamba Malkia wa Uingereza alimsalimia Nyerere huku mikono yake kavaa gloves, Nyerere kuona hivyo naye akareciprocate kwa kumgea kifimbo chake.

Hizi folklore zote zinatengeneza jambo moja la msingi: kutawaliwa kimwili na kiuchumi kunaanza kwa mtu kutawaliwa akili na roho. Msipende kuchukulia vitu poa kudunishwa kwa Rais wa nchi. Ripple effect yake kwa watu wa taifa analoliwakilisha ina nguvu sana.

Kwangu binafsi Rais Samia haniwakilishi mimi huko alikokwenda sijui kuhudhuria msiba wa nani vile. Hilo basi alilopandishwa kapandishwa yeye kama Samia na wala hawajapandishwa watu wa taifa analoliongoza. Watanzania tuna legacy ya taifa kubwa lililowahi kuongozwa na Nyerere na Magufuli na hatuna uduni uduni wa dizaini hizo. Tunaweza kuwa hatuna uchumi mkubwa wa vitu lakini tuna hazina kubwa ya akili na ufahamu na hatukubali uduni wa akili wa wanasiasa walioangukiwa na bahati nasibu ya kutuongoza.
Loud and clear,big up
 
Back
Top Bottom