Rais Samia apandishwa Basi huko London kwenye Msiba wa Malkia Elizabeth II
Ubaguzi hautaisha hapa Duniani. Mabasi ya marais weusi peke yao!

Hayati Magufuli angemtuma balozi tu amuwakilishe.
View attachment 2361528
soma thread hii,
 
Tuwe na akili. Ile nchi imefurika. So ili kupunguza foleni solution wameona ni mabasi.
Unavosema ya kwamba wakijaga kwetu huwa tunawakarimu na escort je huwa wanakuwa marais na wakubwa wakiwa kwa idadi kubwa kama ya kwenye huu msafara.

Pull up your socks
 
Hili jambo wala halihitaji ufafanuzi, wengi wanaolishupalia exposure hakuna.

Viongozi wa nchi zengine mf. China, France, Germany, Brazil, etc. wamepanda mabasi na wala haijawa issue kabisa, ila bongo imekuwa big topic.

Tukiendelea na hizi mentality, hawa mafisi wa kijani watatutawala mapaka Yesu au mtume arudi

Leta picha hapa ya kiongozi wa china au france na German wakiwa kwenye basi moja!
 
Wewe ndiyo usiyekuwa na ufahamu kuhusu kitu kinaitwa "Power Relations" kwenye nyanja mbalimbali na hasa linapokuja kati ya taifa na taifa na athari zake.

Kuna siku Obama alienda Saudi Arabia halafu akajiinamisha chini ya mfalme wa Saudia, wamarekani waling'aka hapana mfano.

Kuna stori (sijui kama ni kweli maana sikuwepo) kwamba Malkia wa Uingereza alimsalimia Nyerere huku mikono yake kavaa gloves, Nyerere kuona hivyo naye akareciprocate kwa kumgea kifimbo chake.

Hizi folklore zote zinatengeneza jambo moja la msingi: kutawaliwa kimwili na kiuchumi kunaanza kwa mtu kutawaliwa akili na roho. Msipende kuchukulia vitu poa kudunishwa kwa Rais wa nchi. Ripple effect yake kwa watu wa taifa analoliwakilisha ina nguvu sana.

Kwangu binafsi Rais Samia haniwakilishi mimi huko alikokwenda sijui kuhudhuria msiba wa nani vile. Hilo basi alilopandishwa kapandishwa yeye kama Samia na wala hawajapandishwa watu wa taifa analoliongoza. Watanzania tuna legacy ya taifa kubwa lililowahi kuongozwa na Nyerere na Magufuli na hatuna uduni uduni wa dizaini hizo. Tunaweza kuwa hatuna uchumi mkubwa wa vitu lakini tuna hazina kubwa ya akili na ufahamu na hatukubali uduni wa akili wa wanasiasa walioangukiwa na bahati nasibu ya kutuongoza.
Nime like paras za kwanza...Hizo mbili za mwisho, naheshimu maoni yako lakini siyakubali
 
Ni hivi waliopangiwa kuingia na magari mpaka kanisani ilikuwa King Charles na mkewe, senior royals wa U.K. tena wachache na US president pekee.

Hakuna mwingine alitakiwa kuingia na gari lake.

Halafu sio kwamba wametolewa huko mahotelini na buses. Wote wamekwenda na misafara yao ya ulinzi isipokuwa wameshuka hako ka sehemu kadogo tu kama mile moja au mbili na kuingia kwa mabasi kwa pamoja.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Unajitetea sana... samia kaaibika sana maskinii

Amejikunyata dirishani kwa hofu anatamani kujificha [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Kwa hiyo serikali itakuja kufafanua jinsi ambavyo Rais alipandishwa chakito ya Uk nasio Ngorika?

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
IMG_0037.jpg
 
Back
Top Bottom