Una hoja murua kabisa na yenye mashiko: kujimudu au kujitegemea wenyewe katika kujijengea uwezo wa kuendesha, kusimamia na kudhibiti rasilimali zetu wenyewe.
 
Ukitaka twende huko, ninapaweza sana.
Kwa hiyo sasa ninakwambia kwamba huna kitu kichawni. Wewe ni wakala tu unayetumwa kuja hapa kutafuta wapumbavu wenzako. Nilitaka tumalizane hapa, sasa nimeamua nikomae nawe hadi tutakapofikia.
Nashauri achana naye tu. Asiyetaka kukuelewa mwachie aendelee na uelewa wake. Usipoteze muda na akili yako kufundisha asiyefundishika kwako.
 
Wanasheria wa serikali wanazunguka huko kuipa jamii uelewa wa nini kinachotaka kufanyika. Ni kazi ya kizalendo itakayokuja kueleweka umuhimu wake siku moja.
Huu mstari huu, umenifikirisha kidogo, na kupata picha linavyochezwa.

Ninakuomba jaribu sana "kufikiri kidogo nje ya boksi". Sasa hivi naona kama umejitwisha boksi zito sana. Nimekwishaligusia hili hapo juu. Ni juu yako kunielewa au la!.
 
Hapo kaongea kwa hisia bila facts
Wewe jamaa vipi tena? Kaongea Kwa hisia!!!??

"Kuongea kwa hisia" maana yake ni kuongea kwa kudhani au bila kuwa na uhakika..

Lakini Je, ndivyo ilivyo kweli Kwa Tundu Lissu jana?

Jibu ni HAPANA kubwa!!

Kwa sasa yeye na hata wewe unahitaji ushahidi wa fact gani tena wakati alikuwa na facts zote mkononi mwake ambao ni mkataba (makubaliano ya maandishi) yaliyosainiwa na waziri wake Prof. Mbarawa (Mzanzibari) kwa yeye mwenyewe Rais Samia Suluhu Hassan (Mzanzibari pia) kumpa kumpa "full authority" kuuza mali zetu watanganyika ?

Please, try to think twice and carefully about this..

Rais Samia Suluhu Hassan kwa hili, katukosea sana Watanganyika...!!
 
Hayo maandishi ya habari yaliyopewa hongo yanajisikiaje nchi yao inauzwa kwa waarabu? Njaa zingine ni za kuedekeza
 
Sasa kama hao wazanzibar wameamua kwa makusudi kuuza mali za tanganyika mnajuaje kama wanalipa kisasi kwa tanganyika kung'ang'ania visiwa vyao? Hii ishu itatikisa muungano kwa style ambayo haikutegemewa. Watanganyika wamechachamaa hawataki bandari yao iuzwe kwa mwarabu bila mkataba wa kueleweka
 
waarabu wataondokaje kama tayari wamesaini mkataba usio na ukomo kumiliki bandari?
 
Kuna mambo ya kujiuliza.., kwa nn Mwarabu tu. Maana nasikia yuko pia TANESCO, POSTA, TPDC daaah kazi ipo.
nani alileta sera ya uwekezaji? Matokeo yake ndiyo hayo. Eti uwekezaji, mara ubia! Haya sasa ngoma ndiyo imenoga. Bado wachina nao watataka sehemu za kuwekeza kwa hoja ya kuleta ufanisi. Wanasiasa wenyewe ndio hawa, watawekezwa na wao
 
Hapa Ccm Wanapita Wanasonya Tu Na Kutema Mate Mbali Huku Wanapatwa Kiungulia Maeneo Ya Kifuani
ccm inavulia mambo ya ajabu sana, sio kama haiwahusu ila ni nani atamfunga paka kengele? Itabidi wakubaliane tu na serikali yao inavyoamua kufanya wanapitisha wote huku wanaona si vema. Ni unafiki tu huko mbeleni wataanza kusema ubaya wake
 
Mwarabu Ametapakaa Ghafla Tanzania Nzima
tuseme ukweli tu, huu ni ukoloni kutawaliwa kiuchumi, kiutamaduni tayari imebaki kisiasa, soon wakikamata uchumi wa nchi wanaibukia siasani na huenda tayari wana vibaraka wao wanaofanikisha malengo yao
 
Hao waandishi wa habari waliopata milioni sita kutetea mauzo ya sehemu ya nchi yao ni hasara na laana kubwa kwao na vizazi vyao vijavyo.
njaa mbaya sana, esau akauza urithi wake ili tu atulize njaa yake. Umasikini nao ni mbaya, nchi itajaa wawekezaji na wabia wa aina hii wengi tu. Kuna wengine wako kwenye migodi, wengine kwenye wanyama, wengine watataka ardhi walime mazao yao, kama zamani ukoloni wa zama mpya unaibuka, kuja kuwatoa wakoloni waliosaini mikataba ya milele ni shughuli pevu kwa vizazi vyetu
 
Bahati nzuri waandishi wa habari wanaotumika ni walewale tu, tangu mgogoro wa Loliondo mpaka leo, jambo lolote linalopingwa wanatengeneza agenda kubwa na kufanya promo....hizi media houses za Bongo uozo mtupu
hizi media zina njaa kali sana, hazioni hasara kufanya promo mikataba ya ajabu na wawekezaji
 
Mkuu naona yupo makini, na anasema anao huo Mkataba huo. Lisu ni Mwana Sheria Msomi anaelewa na ana uhakika na kile anasema.
 
Kwako mwanasiasa Tundu Lissu!

Ukiwa kama mwanasiasa na mwanasheria mzoefu hebu punguza kulialia kwenye media na kuja na hoja dhaifu za kuwagawa Watanzania katika mapande mawili ya U-tanganyika na U-zanzibar linapokuja suala la maslahi mapana ya Taifa.

Umesema kuwa mkataba unao na ukiwa kama mwanasheria hebu tumia fursa hii kurekodi walau video mtandaoni ambazo zitaelezea hivyo vipengele vya mkataba wa DP world ambavyo unaona havina maslahi kwa Taifa la Tanzania.

Hoja ya kuwa nchi imeuzwa kwa waarabu haisaidii mbona husemi nchi yetu imeuzwa kwa wazungu pindi wanapochangia sehemu kubwa ya bajeti yetu kila mwaka.?

Punguza kulialia ,njoo na suluhisho nini kirekebishwe ili kuhakikisha huu mkataba unakuwa na usawa !

Asante.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…