Zaidi ya kulalamika na kulialia hakuna hoja yoyote ya maana uliyoandika. Historia ya kina Chenge na wanasheria ya miaka ya nyuma haina uhusiano wowote na suala la DP World.
 
Zaidi ya kulalamika na kulialia hakuna hoja yoyote ya maana uliyoandika. Historia ya kina Chenge na wanasheria ya miaka ya nyuma haina uhusiano wowote na suala la DP World.
Loooh!
Mimi nimejibu uliyoandika wewe kuwahusu hao 'madaktari', unaotaka tuamini wao ni tofauti na mafisadi wengine, bado huoni pointi hiyo?
Kwani akina Chenge na wengi wengine waliosimamia mikataba mibovu hawakuwa wanasheria? Unanishangaza kama huoni pointi yoyote kama unavyodai.

Sawa, acha tulie lie, kama tulivyolialia siku zote na hii mikataba mibovu mnayotuletea nyinyi madaktari. Kulia lia kwetu juu ya uhujumu wa nchi yetu hakuwezi kutufanya tuone aibu kulialia. Tutaendelea kulialia. Nyinyi faidini.
 
Tatizo unakariri kina Chenge na kuwalinganisha na kina Hamza Johari. Pia ipo tabia ya kudhani kuwa wanaopewa kazi za kuwasaidia viongozi wa juu na wao ni wezi au mafisadi.

Umenaswa kwenye mtego ule ule wa hukumu za jumla jumla, hukumu za hisia zaidi bila ya kujua ukweli wenyewe upo vipi.

Kusema nyinyi faidini ndio ushahidi wenyewe wa kuwa na fikra za kudhani kila anayemsaidia Rais ni mwizi, hizi ni fikra potofu sana.
 
Sasa unanilazimisha nikudharau, kwa sababu naona huna kitu chochote cha ziada unachoweza kunieleza kuhusu mkataba huu wa Bandari.

Chukua muda, pumzisha akili. Njoo na hoja za maana tunazoweza kuzijadili hapa.

Umenishawishi sana sasa nikuone kuwa kumbe huna tofauti yoyote na hawa wengi wanaotafuta tu fursa za kujinufaisha wenyewe kwa mgongo wa wananchi wa nchi hii.
 
Mkataba unapotoshwa na wenye malengo binafsi machafu. Wanashindwa kugundua kwamba Kagame kajenga Dry Port kwao na yupo tayari kwa ajili ya DPW halafu sisi wenye bandari tunakuja na visa vya kuchekesha vya eti mwarabu aliua babu zetu.

Tunaleta hadithi za darasa la pili na la tatu katika dunia ya kibepari, dunia ya utandawazi isiyomsubiri mtu aamke.
 
Nihatari tukiaminishwa kwamba tunaibiwa na viongozi
 
Sasa hoja hapa ni ipi hasa?

Tulazimishe mkataba wa hovyo kwa vile akina Kagame wamejenga bandari huko kwao?

Umesoma mkataba waliowekeana Kagame na hao wawekezaji ukajua masharti yao ndiyo hayo hayo tunayoingia sisi?

Huyo DP World anaingia mikataba inayofanana na nchi zote anazoshirikiana nazo?
Kama bado huoni ufinyu wa fikra zako kwa mawazo kama haya, sijui unataka uelezwe vipi? Unazidi kujionyesha uwezo hafifu sana juu ya haya maswala.

Ngoja niendelee kukuvumilia kidogo labda mwishowe nitaona la maana unaloamini.
 
Muhunibtu Huyu, anatimiliza agenda yake ya kisiasa lakini anajua vizuri kuwa mkataba hauna shida hizo anazozisema ( kwa maana ya hivyo asemacho).
 
wenye bandari tunakuja na visa vya kuchekesha vya eti mwarabu aliua babu zetu.

Tunaleta hadithi za darasa la pili na la tatu katika dunia ya kibepari, dunia ya utandawazi isiyomsubiri mtu aamke
Hii hadithi yako inanirudisha kule kule kwa mwanzo nilipoanza kukusoma humu JF. Niliachana na fikra niliyoipata katika maandishi yako ya mwanzo kwamba ungekuwa na mlengo ule, baada ya mabandiko yako yaliyofuata baadae. Sasa unanirudisha kule kule kwa mwanzo tena mkuu "Steven"?

Nikueleweje?
 
Mkataba gani hauna muda kwamba unaanza lini na kuisha lini
Cholera! Wewe sijui Chotera .... wewe mkataba wako na umasikini mliingia wa miaka mingapi! Mbona yeye na mbowe waliiuza Chadema kwa Lowasa 2020!!!
 
Umesahau kuweka no zako mkuu
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mjomba mtu kapewa lango la mbele la kuuingia mji.
Kibaya zaidi mji aliopewa lango ni wa nyumba aliopangishwa dadake.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cha kushangaza mpaka leo mwanasheria mkuu wa serikali hajawahi kujitokeza popote kuutetea mkataba wake, hii ni dhahili huu mkataba umeandaliwa na mpangaji na sio mwenye nyumba.
 
Kwangu ubinafsishaji ni sawa ila lugha inayotumika na kulitumia Kisiasa sio sawa, vipengele vinavyoleta shida viangaliwe ila sitaki kabisa Bandari ibaki Kwa Wabongo maana wanaitumia kama shamba la bibi na wanapitisha mizigo Kwa vimemo
Watu wote wenye akiri timamu tunataka hivyo lkn waliosani hayo hawayataki kuyasikia.
 
Bora ukalale kumchafua Lissu sio kazi nyepesi ni sawa nakutaka kumchafua Nyerere.Go Lissu
 
Kitila Mkumbo ameshafafanua,mkataba hauna shida kabisa
 
Napinga tafsiri potofu sana za uwekezaji kwa kumhusisha mwekezaji na historia ya miaka ya 1880 huko, mambo yaliyotokea miaka zaidi ya 120 iliyopita.

Vipi kuhusu Mjerumani aliyeua wanamibia zaidi ya milioni mbili, ana ubinadamu kumzidi mwarabu?. mbona anatoa misaada dunia nzima mpaka kesho?.

Tuje na hoja za kumshindanisha hiyo DPW na makampuni mengine yanayofanya shughuli kama yake sio kurudi kwenye akili za kipuuzi za kujadili masuala ya enzi za utumwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…