Ni uwekezaji mkubwa wenye kulenga uboreshaji wa utoaji huduma bandarini.

Ingizo la teknolojia linakwenda kuongeza tija zaidi ya mara mbili ya hii ya sasa.

Rasilimali muda katika dunia ya sasa ni nyeti sana, na kwa kuimarika huduma kwa maana ya wingi wa meli zitakafanyiwa kazi na bandari inamaanisha utabakia muda mwingi wa kushughulika na masuala mengine. Msemo wa time is money unakwenda kutimizwa kwa vitendo.

Pesa nyingi inayopatikana ikiwa ni faida ya mradi inakwenda kugusa sekta nyingi ambazo kwa muda huu zinashindwa kukwamuliwa na zinaonekana zimelala.
 

Mbona hakuna points hapa kasema nini? Sbb naona kelele tupu..

Bunge lilishapendekeza kipengele cha muda wa Mkataba urekebishwe, pia ni bandari ya Dar tu gati 8 hadi 11 tu na si bandari yote ya Dar au bandari zote za Tanzania kuwa DPW watachukua, Tundu Lissu aache kupotosha.
 
Suala la bandari ni vita ya kiuchumi na mkuu Kalamu kaamua kuisaliti nchi yake kwa vipande thelathini vya fedha kama Yuda.

Lakini mwisho wa usaliti unakaribia. Tutaibuka washindi katika vita hii iliyojaa maadui tunaokula nao chakula meza moja.
Na umejiunga hapa JF juzi tu, kwa maksudi maalum; kwa jina la bandia!

Leo hii wewe ndiyo unajitangaza 'mzalendo', kumbe uwepo wako humu jukwaani ni kwa kazi maalum uliyopangiwa kuifanya!

Hopeless Kabisa.
 
Ni nani asiyeyajua haya uliyotaja hapa juu, na bado huelewi swali unaloulizwa, na kwa kuwa upo hapa kupotosha, unakimbilia kueleza mambo yanayofahamika na yeyote.

Tueleze uzuri wa makubaliano uliomo kwenye Mkataba. Hlo ndilo swali. Achana na haya tunayoyataka sisi sote.
 
Kuna muda natamani bora tuamke Kesho Asubuhi tusikie Malaika Israeli kafanya yake kwa wahusika!
Kutoka moyoni mwangu
Natamani sana watangulie hata usiku huu!
Muungano wa nini hasa ikiwa wao wanaona kuwa vya kwao vina thamani na vinufaishe watu wao?
Muungano tuukatae
udhurumaji huu
 
Ningependa sana kuamini ulichoandika hapa, lakini huna ushahidi wowote unaosimamia maneno yako haya.
Hao hao walioleta taarifa toka mwanzo wamekuwa wakichanganya mambo mbalimbali na kama wanaficha baadhi ya mambo yasifahamike, toka mwanzo kabisa.
Kiufupi ni kwamba hawaaminiki tena kwa kila jambo walisemalo.

Sasa nawe hapa unaleta habari zile zile walizokwishazichanganya na madudu chungu nzima!

Tueleze IGA ina masharti gani. Ubovu unaanzia huko, hata kabla hujafika kwenye hayo uliyoeleza wewe hapa.

TICTS alikuwa akifanya kazi hiyo hiyo, hata kama alikuwa haifanyi kwa ufanisi zaidi. Je, yeye IGA yake iliyopitishwa Bungeni ipo?

Na hizo habari za Bandari mbalimbali kuhusika, zilitokea wapi, kama siyo huko huko kwenye IGA hii iliyopelekwa Bungeni.

Kama sasa panafanyika masahihisho, baada ya kelele nyingi, tunataka hayo masahihisho yafanyike kwa uwazi, na siyo kwa ujanja ujanja mwingi kama ule ulioletwa kupitia IGA mara ya kwanza.
 
Uzuri au ubaya wa makubaliano unatafsirika kwa vitendo baada ya mkataba kuanza kutekelezwa. Vifungu vya kisheria hukosa maana kama havitekelezeki.
 
Na umejiunga hapa JF juzi tu, kwa maksudi maalum; kwa jina la bandia!

Leo hii wewe ndiyo unajitangaza 'mzalendo', kumbe uwepo wako humu jukwaani ni kwa kazi maalum uliyopangiwa kuifanya!

Hopeless Kabisa.
Hopeless ni nyinyi msioitakia TZ mema mkiwa mmetumwa na nchi jirani ili muihujumu nchi yenu wenyewe.
 
Baada ya kiki ya kuzurura Mikoani kubuma Sasa chadema wanatembea na kiki ya Bandari

Chama Cha matukio 😁😁
Prof Tibaijuka ni CDM?

Kardinari Pengo ni CDM?

Mimi ni CDM?

Nashauri SA100 atoke aitishe PRESS atoe ufafanuzi.

Jambo hili halileti AFYA Kwa utangamano wa Nchi yetu hata kdg.
 
Mawazo hafifu sana haya.
 
Uzuri au ubaya wa makubaliano unatafsirika kwa vitendo baada ya mkataba kuanza kutekelezwa. Vifungu vya kisheria hukosa maana kama havitekelezeki.
IGA ikisema Bandari zote Tanganyika ziwe chini ya himaya ya Kampuni ya nchi husika, na kama matatizo yakitokea mbele ya safari kwenye utekelezaji huna njia ya kuondokana na masharti hayo; hili nalo unaliona ni jambo linalosubiri utekelezaji wa mikataba mbalimbali?
Huoni kuwa umekwishapigwa kabali hata kabla hujapiga hatua moja kwenda mbele?

Makubaliano ya IGA yasiyokuwa na muda maalum, wewe hayakupi shida hata kidogo kwamba hata huko kwenye utekelezaji pakitokea matatizo tayari umekwishafungwa na masharti yaliyomo ndani ya IGA?

Haya makubaliano ya IGA yana maana gani kwako?
 
ishu ya bandari ccm waangalie sana inaweza kuwang'oa
 
Prof Tibaijuka ni CDM?

Kardinari Pengo ni CDM?

Mimi ni CDM?

Nashauri SA100 atoke aitishe PRESS atoe ufafanuzi.

Jambo hili halileti AFYA Kwa utangamano wa Nchi yetu hata kdg.
Hana uwezo wa kutoa ufafanuzi. Badala yake ndio atavuruga kabisa. Ndiyo maana kamwachia Mbarawa.

Lakini nikubaliane nawe, kwenye jambo lenye hisia nyingi kama hili, ilitakiwa ajitokeze aeleze ukweli wenyewe uliopo nyuma ya jambo hili.
Hata lilivyoshughulikiwa tokea mwanzo, kunatia mashaka sana.

Rais mzima kaenda kuwekwa ndani na kufundwa jinsi ya kuendesha maswala ya nchi yake?
Karibu wiki nzima alipotea, kumbe kafichwa mahala kwa siri kubwa akiamua mambo ya nchi yake na viongozi wa nchi nyingine.
 
Hopeless ni nyinyi msioitakia TZ mema mkiwa mmetumwa na nchi jirani ili muihujumu nchi yenu wenyewe.
Huu ni upumbavu unaokusumbua mpuuzi wewe.

Kwa vilewewe ni mgeni sana humu, hata hujui historia zetu kuhusu maswala yanayoihusu nchi hiyo, halafu unakuja hapa kuropoka tu kama kichwani huna kitu.
 
Wapi huko ndugu Kalamu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…