Ummy Mwalimu: Kuanzia sasa matibabu ya Joseph Haule(Prof. Jay) yatagharamiwa na Serikali
Mimi hata sielewi maana huyu ni Mbunge mtaafu, vile vile ni Msaani maarufu Tanzania na E.Africa zaidi ya miaka 25 iliyopita prof Jay alikua akirindima katika midia mbali mbali hapa Nchini,Je hakufanya uwekezaji katika advantage alizojizoeleza katika jamii ya kitanzania?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na Watanzania wengine walio wagonjwa watagharamiwa na nani?

Kwanza kwa nini agharamiwe na serikali? Ni mtumishi wa serikali kwani?

Ni bora tu wangeacha watu wamchangie na wao kama wanataka kumsaidia, basi wangechanga tu kama watu binafsi.
Hapana.ni bora hio michango achukue mkewe.Pesa haikosi matumizi.
 
Mhh !!!!

Haya ni Majibu mepesi kwa Maswali Magumu..., Hakikisheni gharama za Matibabu ni rafiki kwa kila kiumbe na sio kutoa Charity everytime you see Fit..... (which most of the time you don't)

Hayupo pale kuchague nani alipe na nani asilipe bali kuhakikisha Healthcare is Reachable and Affordable for All....
Well said
 
Ukiishi kwenye jamii pana na akili yako ukaiweka huru utajua kwanini mdau ameandika hivyo,kuna siku niliingia pharmacy moja Kariakoo nikamkuta yupo jamaa ameingia mule kuomba dawa (sikumbuki zilikuwa za maradhi gani maana siyo Dr) ila yeye akizitaka kwa msaada na wakati huo ilionekana kinachomsumbua ndiyo kilikuwa kimekaza kuuma na hela mfukoni hana na mule ndani wote hawajui wafanyeje!

Hizo dawa zilikuwa zina-cost Tsh 7,000/= tu so fikiria ni wangapi wanateseka na maradhi ktk umaskini wao na wakuwaokoa hawana?issue siyo Jay kutibiwa na serikali the issue ni serikali kwa ujumla kuweka mazingira bora ili kila mtu ktk hangaiko lake apate pakujishikiza,kama akawa mwanasiasa sijui msanii wote ni haki yao kupata tiba kwa unafuu wowote unaowezekana.
Well said!!
 
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema kuanzia sasa Serikali itagharamia matibabu ya aliyekuwa Mbunge wa Mikumi Joseph Haule Profesa J anayetibiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili hadi hapo atakaporuhusiwa kurudi nyumbani.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu alipofika Muhimbili leo kumjulia hali Msanii huyo.



Pia soma:
Tumuombee sana Profesa J
Mke wa Profesa Jay afunguka, familia yaomba msaada wa matibabu
god bless u wiziri wa Afya
 
Na hapo ndipo shida ilipo kama nachangia Kila mwezi lakin nikipata ugonjwa mzito kama huu sisaidiwi hiyo bima ni ya nini?
Ya kutibu malaria? Nini tofauti Kati ya mtu mwenye bima na asiyenayo kama mambo yako hivi? Ni nini kinaangaliwa ili magonjwa mengine yaondolew kwenye bima? Nini mchango wa serikali kwenye kufanya huu mfuko ushindw kuhudumiwa wanachama?
Bima inasaidia kwenye dialysis
 
Na Watanzania wengine walio wagonjwa watagharamiwa na nani?

Kwanza kwa nini agharamiwe na serikali? Ni mtumishi wa serikali kwani?

Ni bora tu wangeacha watu wamchangie na wao kama wanataka kumsaidia, basi wangechanga tu kama watu binafsi.
we umechangia tsh ngapi ndugu? unahos watanzania wote hali zetu zinafanana? wengine hata uwezo wa kumchangia 100 tu hatuna kwaiyo mtu afe? we unahis watanzania wangapi wangemchangia? na wewe umemchangia tsh ngapi mpaka unasema waache tu watu wachange? kama tuna moyo huo bas tuchangie wengine waliolazwa uko ma hospital
 
Tha haves and the have nots...

Tunamuombea apone insha'Allah!!
 
Kama hujui issue bora kukaa kimya.
Pesa zimechangwa na zinaingia kwenye simu n aakaunti ya Jey.
Ccm kuona hayo wameblock accounts za Jey na kukimbila Muhimbili kutoa tamko.. Huku mashahidi wana singizia kuugua baada ya kushindwa kujieleza.
Asante sana Lesiriamu, kwa uvunjaji ukimya huu,
Pande mbili sasa timamu, tumejua ya chama 'chetuu',
Chama kitie ngumu, kama chafanyiwa hila juu kwa juu,
Afya ya Prof Jey muhimu, katu himaya ya siasa kuwa utabibuu.
 
Ni bora tu wangeacha watu wamchangie na wao kama wanataka kumsaidia, basi wangechanga tu kama watu binafsi.
Ccm wana wasiwasi na nguvu ya chadema. Wamechukua uamuzi wa kumgharamia matibabu Prof J ili michango ya watanzania na wanavhadema isiendelee kuchangwa.

Wamehofia kampeni kubwa ambayo ingepigwa na chadema nchi nzima.
 
Shangaa mkuu!

Pr J alikuwa msanii anaeingiza hela kutokana na umaarufu wake!
Akaenda bungeni ambako kwa miaka 5 amevuna zaidi ya nusu bilioni,
Leo hii anachangiwa matibabu na selikali ambapo wala si mtumishi wa selikali,

Sijui mtz wa kule sitimbi atatibiwaje?
Ukijumlisha mishahara posho gratuity ni Zaid ya billion na nusu Mzee..
 
Na Watanzania wengine walio wagonjwa watagharamiwa na nani?

Kwanza kwa nini agharamiwe na serikali? Ni mtumishi wa serikali kwani?

Ni bora tu wangeacha watu wamchangie na wao kama wanataka kumsaidia, basi wangechanga tu kama watu binafsi.
Mhh !!!!

Haya ni Majibu mepesi kwa Maswali Magumu..., Hakikisheni gharama za Matibabu ni rafiki kwa kila kiumbe na sio kutoa Charity everytime you see Fit..... (which most of the time you don't)

Hayupo pale kuchague nani alipe na nani asilipe bali kuhakikisha Healthcare is Reachable and Affordable for All....
'I second you'...mpo sahihi kabisa....lazima bima ya afya kwa wote iwe kipaumbele.
 
Ikiwa mbunge mstaafu ambae alikuwa akipata marupurupu tele alipokuwa bungeni, na anaendelea kupata malipo mazuri ya serikalini kila mwezi anashindwa kujilipia matibabu, serikali haoini kuwa kuna haja ya kumfikiria mlala hoi juu ya malipo ya matibabu? Na kama sio kama hawezi kujilipia je ni kwa nini serikali imlipie na imuwache mlala hoi afe kwa kukosa pesa ya matibabu?
 
Safi sana kwa Serikali kutambua mchango wa Prof Jay kwenye music wa Tanzania
Ni unafiki tu hakuna chochote huyo wasanii na wanasiasa wenzako wako tayari kumtibu tunataka serikali itowe matibabu kwa watu wote bila ya kuangalia wasfu wa mtu tunataka universal health care kuanzia maradhi madogo mpaka makubwa.
 
Habari kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili zinasema Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema serikali itagharimia matibabu ya mwanamziki maarufu wa kizazi kipya ambaye pia alikuwa Mbunge wa Mikumi Joseph Haule, a.k.a Prof. J aliyelazwa katika Hospitali hiyo. Hayo yameandikwa katika mtandao wa jamii wa Twitter.

Pongezi kwa serikali kwa kuwaenzi viongozi wetu.
Acha kushabikia dhulma hatukatai serikali kumtibu pro.j lakini wajibu wa serikali ni kuwatibu raia wake wote bila ubaguzi wa aina yoyote vile.
 
Back
Top Bottom