- Thread starter
- #261
Hao jamaa nao wana risk sana maisha yao. Imagine dogo angeamua liwalo na liwe akaamua kuwagonga hao waliokuwa barabarani?
Kukosa nidhamu, weledi, maadili hasa kwa watumishi kama hawa ni janga kwa taifa.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hao jamaa nao wana risk sana maisha yao. Imagine dogo angeamua liwalo na liwe akaamua kuwagonga hao waliokuwa barabarani?
Hawakugongana, ilikua ni kuchomekeana.No excuse brother, ulitakiwa kusimama palepale eneo la tukio. We ulitegemea ataenda kutoa maelezo gani na gali si lake na lina damage?
Kwa mara nyingine,tuonyesheni umoja na mshikamano katka hili hata kama wengine halituhusu ila ifike MAHALI Jamii Forum iogopwe.
Tupaze sauti,Hili tukio lifike linapostahili kufika na wenye connection watuletee mrejesho,mimi kazi yangu nikutia NUKTA uzi upande hewani kila nitakapohisi umepooza.
Huna cha ku comment tia NUKTA uzi upae hewani hadi hao waliohusika hapo kila mtu apewe stahiki zake na iwe mwanzo na mwisho huu uonevu,Tukiamua wananchi sisi kwa sisi inawezekana.
Hamna cha katiba mpya hapa Maamuzi ni yetu wenyewe tuamueni TU.
Sikubishii mkuu wangu.Usibishe. Iliwahi kunitokea. Mi nimesimama kwenye taa nyekundu. Nasubiri ya kijani. Nyuma kuna roli. Dereva hana mpango wa kusimama. Alivyofika tu kwenye taa, zikabadilika zikawa kijani. Na mimi nikaondoa gari. Najua mimi ndio wa kwanza mbele kwa wale tuliokuwa kwenye mstari wa kusibiri taa za kijani. Alipopita taa, akabadili njia. Akatoka kushoto kwake akaja kwangu kulia, akanibana kabisa nikakosa njia. Nikasisima ghafla. Matairi ya nyuma ya roli lake yakanikosasa. Akaendelea kama vile hajafanya kitu chochote. Ningekuwa na bunduki na mimi siku hiyo ningeua mtu.
Makosa yanaweza kutokea pande zote hao ndugu zetu katika medani ila hata huyo bwana na ist yake ni wale wale tu,pale aliposema mjomba wangu mbunge atanitoa nikaona baasi huyu ni aina ya wale watu wasumbufu hadi mtaani kisa tu anajuana na fulani kisa tu yeye fulani kisa tu ana watu fulani ikumbukwe kuna wakati mpaka uwapate hao watu wa kukusaidia ushachakaa vibaya mno huyo bwana ist nae wale wale
Ana udhibitisho gani?Utaratibu unatakiwa uende ukaripoti kwa mkuu wa kambi kwamba umeharasiwa na huyo jamaa hatua za kinidhamu maana uthibitishi unao hapo
Kwa nani sasa?Hii ni ukosefu wa nidhamu wa hali ya juu. Hii ni kukosa professionalism.
Aibu sana. Halafu haraka zao watumia barabara wanazijuaje?
Unajuaje kama dogo aliwatukana?Nani kasema nchi hii ni ya wana usalama peke yao?
Kama huu unaoufanya hapa! Kutetea upumbavu nayo ni upumbavu+Wamefanya upumbavu gani?
Dogo anapiga picha/video sehemu isiyoruhusiwa.Napajua...
Masihara haya! Alikuwa anashinda klabu ya msichoke hapo makorongoni akigongea komoni Kwa wale kina mama!Najua pale mwembetogwa ulikua mtukutu na mtoro wa shule ila nafasi ya kujifunza ustaarab ilikuwepo unajisahaulisha tu.
Unajuaje kama dogo aliwatukana?
Kuna uwezekano mzozo haujaanzia kwenye kuchomekeana tu
Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Kuna pumbavu mwingine alikuja kwenye mgahawa mmoja nilikuwa nimeachiwa pale karibu na Makumbusho. Amemaliza kula akataka kukimbia, mfanyakazi mmoja akamtia pini pale. Akaanza kusema kuna mtu nilikuwa nataka nimcheck hapo pembeni, akaambiwa lipa uende; mara huyo jamaa ndio ana hela ya kulipia. Akataitiwa pale, kidogo kaanza mimi usalama wa taifa... hapo ndio akatuchefua zaidi. Tukamwambie ofisini kwenu sio mbali, twende kwa bosi wako akalipe! Akabaki anatoa macho. Mwisho wake aliacha simu pale, baada ya wiki alikuja kulipa.Kuna fala mmoja huwa anajifanya au sijui ndio security wa Taifa kweli!!!? Nilikuwa nasikia sana tabia zake za kuwa akikutaa bar unakunywa na yeye anaagiza kama uvyokunywa wewe kisha anasema utalipa wewe,.
Bahati nzuri mimi sinywi ila nikasema hasirogwe kuingia katika anga zangu za aina yoyote hile.
Siku moja nikaenda bar na rafiki yangu mmoja alikuwa ananywa zake bia mimi nikiwa nakunywa sparletar yangu mara jamaa kaja na kama kawaida yake siku hiyo akafikia kwenye point yetu. Akatusalimia akaenda counter kaagiza na yeye bia zake kama za jamaa yangu na kumwambia counter kuwa watalipa wale pale akituonesha sisi.
Baada ya sisi kumaliza yetu tukaomba bill ilipoletwa tukaona bill imekuja mara dufu, nilipooliza tukajibiwa kuwa na pombe zile pale. Mimi nikamwambia sisi hatumfahamu alipe mwenyewe, baada ya hapo jamaa si akaja akatuuliza kwa nini hatutaki kunilipia?
Nikamuuliza tukulipie wewe una tatizo gani? Nae akatuuliza kwani nyinyi hamnifahamu, na Mimi nikamuuliza "sisi unatufahamu?" Nikamwambia ondoka kabla sijakushia dhahama, wakati huo watu wametunguka wakisilizia. Naona kaondoka uku akisema "mtanijua tu"
Juzi nimekutanae barabarani nashangaa kanisalimia bro za ziku?
Nikajifanya sikumsikia.
Mbona vijana mnakuwa wapumbavu na wajinga kiasi hiki cha lami? Do we read kweli sheria?Unyanyasaji huu wa vyombo vya dola haukubaliki.
View attachment 2182373
Kwanini sheria za nchi zilizopo hazifuatwi?
Kwa hakika tuungane kuukataa ubazazi wa namna hii.
Mwendelezo wake hatujui ulivyo.Dogo hapo hapajui na picha kaanzia barabarani akiendesha gari