Uchaguzi 2020 Ahadi na Sera za Tundu Lissu katika Uchaguzi Mkuu 2020
Jana mh Lissu alivyokuwa tabora alisema anatamani nasisi tupate huduma nzuri ya afya kama aliyopata yeye Ubelgiji, kwa kweli ni jambo jema sana. Kasema alivyofika huko aliuliza sasa gharama itakuwaje? akaambiwa alipie Euro 275 tu na atatibiwa kwa mwaka mzima, kwa exchange rate ya leo euro moja ni sawa na Tshs 2748.07, kwa maana nyingine alilipia Tshs 756,000/=. Hiyo ndio bima ya watu wa kawaida wa Ubelgiji.

Lakini juzi Mh Lissu alivyokuwa Shinyanga alilalamika JPM kumnyima hela ya kutibiwa kwa maana nyingine alinyimwa Euro 275. Sitaki kuamini hayo alifanyiwa. Hoja yangu ni kama kila mtanzania atalipa euro 275 naamini huduma zetu zitakuwa bora sana ikiwezekana zaidi ya huko Ubelgiji lakini watanzania wangapi wenye huo uwezo wa kulipa euro 275?

Je, hii ndio bima nafuu anayo tuhabarisha huyu mheshimiwa? Wazo lake ni jema tatizo uwezo wa watanzania kumudu ndio shaka ilipo? Na ukiwa huna maana yake ufe, au? kwa sasa kama hauna bima kumwona daktari ni bure na matibabu ni bure katika zahanati za umma na vituo vya afya.
Ukimchukia mtu zuri huwa baya na baya la unayempenda huwa zuri, nenda NHIF na laki nane urudi na bima! Kabla ya kulikataa jambo chunguza kwako likoje.
 
Hapa bima NHF ni 650,000 sawa na hiyo ya ubelgiji kwa maana hiyo maneno mengi ni burudani za kapeni tu
Maneno mengi utekelezaji 0 ili mradi mtaji wa kura umepatikana
NHIF uko huu zaidi ya hiyo na uzuri wake haupati baadhi ya tiba na kila mara huduma hubadilishwa, hivyo hapa kwetu iko kimapato zaidi.
 
Wasiojiweza watalipiwa na kodi zetu na mifumo ikitengenezwa isiyo ya kufisadi na kufikisha pesa itakuwa rahisi kwa mtanzania na tutapata bima wote tayari wapo ambao wana bima na by the way CCM wepesi sana kwa sasa magu kaharibu kila sehemu hadi anaona aibu kutuomba kura, hivi zile 50m za kila kijiji jpm amezigawa?
Mkuu ukikuta wapumbavu wanaongea upumbavu wao ukitia mambo ya akili hawawezi kukuelewa maana wao huamini katika upumbavu wao.
Izingatiwe tu kwamba "ulofa na upumbavu si tusi ni sifa kama ulivyo unyonge!!"
 
Ukimchukia mtu zuri huwa baya na baya la unayempenda huwa zuri, nenda NHIF na laki nane urudi na bima! Kabla ya kulikataa jambo chunguza kwako likoje.
Ni milioni na ushei wao wanataka kutuambia ni 54,000!!!
 
Sidhani kama bima ya afya huko ulaya kwa mgeni tena liyeingia kwa VIZA ya matibabu kama inaweza kuwa chini kiasi hicho
 
Mwongo,alitibiwa kama mkimbizi new comer,hiyo hela kalipia registate fees matibabu ni bure labda euro 2 kumwona daktari na dawa akikuandikia utalipia,
Bima ya afya unapewa bure as long ni mfanyakazi
 
Jana mh Lissu alivyokuwa tabora alisema anatamani nasisi tupate huduma nzuri ya afya kama aliyopata yeye Ubelgiji, kwa kweli ni jambo jema sana. Kasema alivyofika huko aliuliza sasa gharama itakuwaje? akaambiwa alipie Euro 275 tu na atatibiwa kwa mwaka mzima, kwa exchange rate ya leo euro moja ni sawa na Tshs 2748.07, kwa maana nyingine alilipia Tshs 756,000/=. Hiyo ndio bima ya watu wa kawaida wa Ubelgiji.

Lakini juzi Mh Lissu alivyokuwa Shinyanga alilalamika JPM kumnyima hela ya kutibiwa kwa maana nyingine alinyimwa Euro 275. Sitaki kuamini hayo alifanyiwa. Hoja yangu ni kama kila mtanzania atalipa euro 275 naamini huduma zetu zitakuwa bora sana ikiwezekana zaidi ya huko Ubelgiji lakini watanzania wangapi wenye huo uwezo wa kulipa euro 275?

Je, hii ndio bima nafuu anayo tuhabarisha huyu mheshimiwa? Wazo lake ni jema tatizo uwezo wa watanzania kumudu ndio shaka ilipo? Na ukiwa huna maana yake ufe, au? kwa sasa kama hauna bima kumwona daktari ni bure na matibabu ni bure katika zahanati za umma na vituo vya afya.
Kama unamwamini Lissu ujue una matatizo fulani ya akili. Huwezi kwenda hospitali unaumwa ndipo ukate bima kusudi utibiwe, inatakiwa uwe na bima kabla hujaugua. Mambo mengine ni vizuri kutoyasema tu
 
Umeonyesha rangi yako halisi ya utanzania,uvivu.bibi yangu ambaye hakuliona darasa hana hata wasaa wa kuuliza swali.je wewe mvivu ambaye uliuona mwanga kidogo unashindwa pia kupitia ilani ya chama na iko humu.kimsingi Lissu ameshaeleza yote sera yao ya elimu,bima ya afya kwa wananchi wote,kupitia kodi na tozo mbalimbali,soko huru la mazao linalomnufaisha mkulima mkulima hatakopwa.alishaeleza kuhusu utalii,madini.nk.ACHA UFINYU WA MAWAZO MKUU.na leo saa 3 usiku ITV DAKIKA 45 Lissu atakuwa hewani.kaangalie uondoe tongotongo za ujinga unaokusumbua.Badilisha namna yako ya kufikiri.
Hawa wagombea sanasana atakupa muhtasari wa yale mambo muhimu zaidi.usitarajie MAGUFULI akuonyeshe etie Ilani aliiandaa yeye so amemeza kurassa zote .
Pia kusema waliandikiwa ilani ni kuonyesha upeo mdogo wa kufikiri.kila chama cha siasa kina mambo ya msingi kinayoyasimamia,ikiwa ni sera ,imani nk. Na si katka uchaguzi tu.Mara nyingi hizi ilani zinarekebishwa na kufanyiwa maboresho tu kuendana na mda na wakati.
Sera haina kitu boss! Ni kama wimbo wa taifa. Kila wimbo unamsifu Mungu lakini kweli wanafuata ya Mungu?.
Ilan ni kitabu tu! Je, uonavyo ktk kundi la juu la CHDEMA kuna mtu wa kujua maana ya maendeleo? Lissu?, Mbowe?, Mnyika?, Mwalimu? Yani hayo madarasa kweli ndo yatuvushe? Noooo!
 
Nimejaribu kupekua mafaili yote ya wizi na ufisadi ndani ya Nchi hii yaliyojaa kila ofisi lakini sikufanikiwa kuona andiko hata liliofutika linaloeleza kashfa ya Mgombea Urais wa Chadema ambaye pia ni Rais Mtarajiwa wa Tanzania Mh Tundu Lissu.

Huyu mtu ni msafi kama theluji , hajawahi kudokoa , kudhulumu chochote popote , hajawahi kudhulumu nyumba ya Serikali wala ya mtu yeyote , hajawahi kuiba mtumbwi wa mtu, hajawahi kudhulumu boti ya uvuvi pale feri wala hajawahi kuiba Meli yoyote , ni mtu asiye na makandokando yoyote .

Tunaamini kwamba ameletwa na Mungu Mwenyewe kuja kuleta Uhuru kamili ndani ya nchi hii na amekuja kuleta furaha iliyotoweka kwa zaidi ya miaka mitano
View attachment 1558038

Ukifuatilia sera yake ya Elimu utagundua kwamba ameletwa maalum kuboresha elimu ya nchi hii ambayo mara zote imeshindwa kumkomboa mwanafunzi
View attachment 1558041

Wananchi wote wamemkubali na wameapa kumpa kura zao ili awaondolee dhiki kwa kuleta maendeleo ya kweli ya watu wa nchi hii
View attachment 1558044

Njia pekee ya kumdhibiti mtu huyu kutwaa Urais wa Tanzania ilikuwa ile ya risasi 38 iliyofeli baada ya Mungu aliye hai kuikataa , na sasa tunahesabu masiku machache kabla ya Tanzania kujitwalia Uhuru kamili .

Mungu mbariki Tundu Lissu
Hugo Tundu Lissu ameishapeleka bank statement ya akaunti yake kwa Mwenyekiti Mbowe? Kama bado anaogopa nini?
 
KWA sababu Ccm mmeshindwa kuisimamia democrasia ,haki na maendeleo ya watu naomba kura yako umpe Lissu

Watu wengii Ni waoga Ni wanafiki na kujipendekeza kwingi machoni wanacheka moyoni wanalia Hili kundi Ni kubwa wapo wafanyakazi wa umma, Wafanyabiashara ,wanafunzi na wengine wengi hawasemi tu ,hawaonekani kwenye mikutano ya kampeni lakini miyoyo yao Ina uchungu

Mimi Ni mmoja wao,uwezi kunikuta naongelea siasa mahali popote ,Sina kadi yeyote Ila KURA YANGU NITAMPA LISSU hata asipopita upande wa pili Kuna kitu watajifunza

Usikosee
 
Kiukweli kabisa jamaa ameweza kutuconvince kwa yale anayotaka kuwafanyia watz. Amejibu maswali vizuri bila muhemuko na kwa point. Uongozi ni kipaji na kweli tunaona anacho.
 
Ninyi kweli "weupe", badala ya kumuhimiza Lissu afafanue ilani yake kinaga ubaga watu waelewe Chadema inaweza kufanya nini tofauti na kilichokwisha fanywa na kinatachotarajiwa kufanywa CCM, bado mnabaki kupiga kelele ambazo watu hawana taimu nazo. Mwambie Lissu aWaeleze wananchi ninamna gani ataifumua TRA na kisha kuleta mbadala wake utakao fanya kazi bora zaidi ya TRA ya sasa. Pia aeleza namna atakavyolipa fidia kutoka " mfukoni mwake"!
Atafafanua huko mbele. Vision kwanza, mission baadae.
 
Lissu niseme wazi leo umegusa maisha ya Watanzania walio wengi.

- Bima ya afya kwa Watanzania wote.

- Hakuna tena kuibia wafanyabiashara maskini kwa kuwatoa elfu ishirini kila mwaka.

- Hakuna tena kukatwa asilimia 15 kisa mkopo. Tutakatwa asilimia tatu tu.

- Elimu ya maarifa, kubadili kabisa falsafa ya Elimu. Elimu ya kutatua matatizo ya maisha yao. Big point here Baba.

In General leo sasa umeongea kama Rais.

Viva Lissu, Viva Tanzania yenye Uhuru, haki na maendeleo ya watu.

====
We better vote for TAL
 
Back
Top Bottom