Nimejaribu kupekua mafaili yote ya wizi na ufisadi ndani ya Nchi hii yaliyojaa kila ofisi lakini sikufanikiwa kuona andiko hata liliofutika linaloeleza kashfa ya Mgombea Urais wa Chadema ambaye pia ni Rais Mtarajiwa wa Tanzania Mh Tundu Lissu.
Huyu mtu ni msafi kama theluji , hajawahi kudokoa , kudhulumu chochote popote , hajawahi kudhulumu nyumba ya Serikali wala ya mtu yeyote , hajawahi kuiba mtumbwi wa mtu, hajawahi kudhulumu boti ya uvuvi pale feri wala hajawahi kuiba Meli yoyote , ni mtu asiye na makandokando yoyote .
Tunaamini kwamba ameletwa na Mungu Mwenyewe kuja kuleta Uhuru kamili ndani ya nchi hii na amekuja kuleta furaha iliyotoweka kwa zaidi ya miaka mitano
View attachment 1558038
Ukifuatilia sera yake ya Elimu utagundua kwamba ameletwa maalum kuboresha elimu ya nchi hii ambayo mara zote imeshindwa kumkomboa mwanafunzi
View attachment 1558041
Wananchi wote wamemkubali na wameapa kumpa kura zao ili awaondolee dhiki kwa kuleta maendeleo ya kweli ya watu wa nchi hii
View attachment 1558044
Njia pekee ya kumdhibiti mtu huyu kutwaa Urais wa Tanzania ilikuwa ile ya risasi 38 iliyofeli baada ya Mungu aliye hai kuikataa , na sasa tunahesabu masiku machache kabla ya Tanzania kujitwalia Uhuru kamili .
Mungu mbariki Tundu Lissu