Yaani mradi wa JNHPP hauna manufaa kwa taifa letu? Ndio sindano hizo unaita.
Lisu aende Rufiji tu pale ulipo mradi awaambie wananchi hauna faida halafu aombe kura aone kitakachofuata akitoka akutane na wenye viwanda awaambie miradi ya umeme ya Magufuli ni ujinga mtupu aendeleze watu aache kuhangaika na Stigler Gorge aone kitakachomkuta akitoka aende chato akawaambie mradi wa uwanja wao wa ndege hauna faida aombe kura aone muziki wake akitoka hapo aende kwa wasukuma akawaambie ndege hazina faida kwa mtu wa kawaida aone muziki wake

Lisu ana tatizo kichwani miradi kama anasema mibaya akaongee ilipo kama yeye kidume kweli akaiponde ilipo

Lisu hana agenda serious yenye hoja mbabaushaji tu
 
Ditto Bulendo ana maswali mazuri sana yanayoonyesha si tu anajua kazi yake,bali ni mfuatiliaji mzuri wa namna nchi inavyoendeshwa

Kabisa huyo jamaa ni mwanahabari mzuri sana, ndio nimekuwa nikipendekeza hata kukiwa na mdahalo wa urais, yeye ndio hasa anafaa kuwa muongoza mdahalo.
 
Mwambieni Lisu Kama Miradi yaaliyotekekeza mibaya akaiongelee pale ilipo Kama Ni zahanati akaongee ilipo Kama Ni barabara akaongelee ilipo Kama ni hospital akaongelee ilipo nk aache kuongelea sijui reli akiwa bagamoyo sijui stigler gorge akiwa ikungi kijijini Kwao kwa watumia vibatali !! Kama yeye kidume Kweli
 
Jibu hoja. Kama haumwelewi Lissu basi wewe ni mbumbumbu. Lugha rahisi sana. Lissu ni zaidi ya mwalimu. Kama hautaki kuelewa hauwezi kulazimishwa kuelewa. Kama umesikiliza ujumbe umeupata.
Wanaelewa Kisukuma tu labda kidogo Kitutsi lakini Kiswahili hata wenye PhD wa kule kinawapiga chenga. Tungoje wafike Bukoba wakamwage sera kwa Kisukuma wataelewana tu lakini Ruangwa wajiandae kufukizwa.
 
☝️
Mkuu unaonekana una ushabiki wa kindezi sana.
Hebu andika hapa, lini uliambiwa au kusikia, kusoma pesa ya ujenzi wa miradi hiyo?

NB: Inaonekana wengi hamjasikiliza hii interview, wadau wameukimbia uzi, ila alichoongea Lissu kina jambo lenye mashiko pamoja na wabeba mabango ya siasa kuponda.

Lissu ana jambo kubwa sana dhidi ya chama kizee kilichowalea watanzani.
 
Hizo hoja wanapaswa waziongee wabunge sio mgombea uraisi. Hiyo point ya mishahara Hana uwezo nalo ila kwenye maongezi yake alitie nyama nyama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…