Uchaguzi 2020 Ahadi na Sera za Tundu Lissu katika Uchaguzi Mkuu 2020
Kumbe matibabu ukiwa nje ya nchi ulaya ni bima tu ?

Ulipii pango ulipii Kodi ulipii chochote unaishi miaka 3 ulaya?

Unakula kwa bima unaishi kwa bima unasafiri kwa bima .

Uliza Kwanza ndungai alitibiwa vipi kwa Bilion 12 India.?
 
Yaani hapa umenena ukweli mtupu! Haya mambo yanawagusa moja kwa moja hata ndugu ,jamaa na watoto wao! Ni mwendawazimu tu ndiye atapinga hayo yote lakini wajuwe kile wanachoita kuisoma namba hakichagui itikati, jinsia wala kabila! Nina imani kubwa hata mamilioni ya wanaCCM kura zitaenda kwa Lissu, fanyeni hivyo mjikomboe!
 
Kumbe matibabu ukiwa nje ya nchi ulaya ni bima tu ?

Ulipii pango ulipii Kodi ulipii chochote unaishi miaka 3 ulaya?

Unakula kwa bima unaishi kwa bima unasafiri kwa bima .

Uliza Kwanza ndungai alitibiwa vipi kwa Bilion 12 India.?
Jibu hoja ya msingi watanzania wote wanaweza kugharamia Euro 275? Acha kuruka viunzi.
 
Tupeane ratiba basi jamani 😜😜😜😜 Spunda ndio mpango mzima
 

Attachments

  • image.jpeg
    image.jpeg
    7.4 KB · Views: 1
Mimi binafsi nitamchagua Tundu Lissu maana anagusa maisha yangu moja kwa moja kwa kusisitiza maendelea ya watu na sio vitu..

Miaka 60 ya Uhuru tunajisifia barabara? Na madaraja?

Miaka 60 ya Uhuru tunajisifia kujenga shule na zahanati tulikuwa wapi siku zote wakati watawala ni wale wale?

Miaka 60 CCM wanajisifia kupeleka umeme vijijini tulikuwa wapi miaka yote ?

Huu ni udhaifu wa CCM na Serikali yake miaka yote walikuwa wapi?.

Maji, Umeme, barabara sio masuala ya kutuletea hapa Kama mapya kwani kila siku tutajenga na tutaendelea kujenga kwa sababu tunalipa Kodi kwa kazi hizo.

Tunataka sera mpya zinazogusa maendeleo ya watu na sio vitu.

Lissu kaja na Dawa yake Bima ya afya kwa kila mtanzania

Kuifumua TRA ambayo Ni joka la mdimu kwa Taifa ili

Kuzifumua mifuko za hifadhi za jamii

Kutowakopa wakulima mazao yao

Mimi Ni Nani staki mabadiriko haya kwenye haya maisha mafupi kiasi hiki?

Labda mpumbabu tu ndiye atakataa hizi hoja na sera za Lissu.
Kwani maendeleo ya watu yakoje? Maana hata nyumba bora ni maendeleo lakini ni kitu. Muwe mnatumia ubongo kabla ya kusapoti mambo. Kujenga hospital,sio maendeleo ya watu?
 
Nimejaribu kupekua mafaili yote ya wizi na ufisadi ndani ya Nchi hii yaliyojaa kila ofisi lakini sikufanikiwa kuona andiko hata liliofutika linaloeleza kashfa ya Mgombea Urais wa Chadema ambaye pia ni Rais Mtarajiwa wa Tanzania Mh Tundu Lissu.

Huyu mtu ni msafi kama theluji , hajawahi kudokoa , kudhulumu chochote popote , hajawahi kudhulumu nyumba ya Serikali wala ya mtu yeyote , hajawahi kuiba mtumbwi wa mtu, hajawahi kudhulumu boti ya uvuvi pale feri wala hajawahi kuiba Meli yoyote , ni mtu asiye na makandokando yoyote .

Tunaamini kwamba ameletwa na Mungu Mwenyewe kuja kuleta Uhuru kamili ndani ya nchi hii na amekuja kuleta furaha iliyotoweka kwa zaidi ya miaka mitano
View attachment 1558038

Ukifuatilia sera yake ya Elimu utagundua kwamba ameletwa maalum kuboresha elimu ya nchi hii ambayo mara zote imeshindwa kumkomboa mwanafunzi
View attachment 1558041

Wananchi wote wamemkubali na wameapa kumpa kura zao ili awaondolee dhiki kwa kuleta maendeleo ya kweli ya watu wa nchi hii
View attachment 1558044

Njia pekee ya kumdhibiti mtu huyu kutwaa Urais wa Tanzania ilikuwa ile ya risasi 38 iliyofeli baada ya Mungu aliye hai kuikataa , na sasa tunahesabu masiku machache kabla ya Tanzania kujitwalia Uhuru kamili .

Mungu mbariki Tundu Lissu
JamiiForums1323532925.jpg


Jr[emoji769]
 
Jana mh Lissu alivyokuwa tabora alisema anatamani nasisi tupate huduma nzuri ya afya kama aliyopata yeye Ubelgiji, kwa kweli ni jambo jema sana. Kasema alivyofika huko aliuliza sasa gharama itakuwaje? akaambiwa alipie Euro 275 tu na atatibiwa kwa mwaka mzima, kwa exchange rate ya leo euro moja ni sawa na Tshs 2748.07, kwa maana nyingine alilipia Tshs 756,000/=. Hiyo ndio bima ya watu wa kawaida wa Ubelgiji.

Lakini juzi Mh Lissu alivyokuwa Shinyanga alilalamika JPM kumnyima hela ya kutibiwa kwa maana nyingine alinyimwa Euro 275. Sitaki kuamini hayo alifanyiwa. Hoja yangu ni kama kila mtanzania atalipa euro 275 naamini huduma zetu zitakuwa bora sana ikiwezekana zaidi ya huko Ubelgiji lakini watanzania wangapi wenye huo uwezo wa kulipa euro 275?

Je, hii ndio bima nafuu anayo tuhabarisha huyu mheshimiwa? Wazo lake ni jema tatizo uwezo wa watanzania kumudu ndio shaka ilipo? Na ukiwa huna maana yake ufe, au? kwa sasa kama hauna bima kumwona daktari ni bure na matibabu ni bure katika zahanati za umma na vituo vya afya.
Itakuwa chini ya kiwango hicho kwasababu selikali yetu ya awamu ya sita chini ya kamanda lissu itasubsdize 20% kwa kila mtu.

Tutatumia mfumo wa PPP public private partnership kujenga miundombinu na kuweka tozo nafuu Kama daraja la NSSF kigamboni

ili fedha nyingi ya Kodi na mapato isaidie ustawi wa watu.
 
Nyumba inajengwaje wakati mtu hauna pesa mfukoni

Tukiwaita wapumbavu mnalialia

Pumbavu kabisa.
Ndio maana serikali inajenga hospital kwa kutumia pesa ili wananchi watibiwe. Hoja hapo ni kuwa nyumba inajengwa ili itumiwe na watu. Ndio maana ya maendeleo ya watu. Serikali inaboresha miundo mbinu,afya na elimu ili watu wanufaike. Tumia akili kabla ya kuandika upuuzi.
 
Back
Top Bottom