Jana mh Lissu alivyokuwa tabora alisema anatamani nasisi tupate huduma nzuri ya afya kama aliyopata yeye Ubelgiji, kwa kweli ni jambo jema sana. Kasema alivyofika huko aliuliza sasa gharama itakuwaje? akaambiwa alipie Euro 275 tu na atatibiwa kwa mwaka mzima, kwa exchange rate ya leo euro moja ni sawa na Tshs 2748.07, kwa maana nyingine alilipia Tshs 756,000/=. Hiyo ndio bima ya watu wa kawaida wa Ubelgiji.
Lakini juzi Mh Lissu alivyokuwa Shinyanga alilalamika JPM kumnyima hela ya kutibiwa kwa maana nyingine alinyimwa Euro 275. Sitaki kuamini hayo alifanyiwa. Hoja yangu ni kama kila mtanzania atalipa euro 275 naamini huduma zetu zitakuwa bora sana ikiwezekana zaidi ya huko Ubelgiji lakini watanzania wangapi wenye huo uwezo wa kulipa euro 275?
Je, hii ndio bima nafuu anayo tuhabarisha huyu mheshimiwa? Wazo lake ni jema tatizo uwezo wa watanzania kumudu ndio shaka ilipo? Na ukiwa huna maana yake ufe, au? kwa sasa kama hauna bima kumwona daktari ni bure na matibabu ni bure katika zahanati za umma na vituo vya afya.