Wasalaam
Mgombea mwenza wa chadema Ndugu Salum Mwalimu mwenye Phd ya mambo ya usafiri ameendelea kuzunguka huko moshi akikinadi chama na kuendelea kuwashangaza walio wengi kwani baadhi ya matamshi yake yanawachanganya watu na kushindwa kujua upi ni msimamo wa chama?
Salum Mwalimu leo amekaririwa akisema watanzania wote kuanzia watoto na kila rika watapatiwa pass port bure(hati ya kusafiria) lakini hili jambo limefanya wanao msikiliza wajiulize nini msimamo wa chama?
Watu bado wanajiuliza hizo hati za kusafiria watanzania watakwenda nazo wapi na kwakutumia usafiri upi ikiwa chadema na mgombea wao bwana Lissu wanapinga uwepo wa ndege? hizo pass port tutakwenda nazo morogoro? pass port tutakuwa tunazitumia kwenda nazo singida? au tutazitumia kwenda machame?
Bado watu wanajiuliuza tutapanda nazo bajaji au baiskeli ukizingatia chama na mgombea wake wanapinga uwepo wa ndege na kuna uwezekano wakiingia tuu watauza ndge zote? au tutazitumia kufanya nini?
Wasalaam