Najikita kwenye hoja ya VITAMBULISHO
Ngoja nijikite kwenye "UONGO" na UZUSHI wa kwanza juu ya vitambulisho vya wajasiriamali. Ni hivi - ni vizuri watu msiwe wasahaurifu wa mambo yaliyokuwa yakitukuta sisi wajasiriamali. Ni nani asiyejua adha, manyanyaso na usumbufu tuliokuwa tukipewa na mgambo na viongozi mbalimbali katika sehemu zetu za kazi kama huko kwenye masoko, kwenye site mbalimbali au huko mabarabarani tulikokuwa tukipanga vitu, bidhaa au biashara zetu. Kweli mmeshasau mateso hayo ya kuporwa au kumwagiwa bidhaa zetu na hata wakati mwingine kukamatwa na kupelekwa mbele ya PILATO na kuhukumiwa faini za ajabu ajabu ajabu na hata VIFUNGO? Kweli mmesahau kiasi ambacho mnasimama na kusikiliza UONGO NA UZUSHI wa Lissu eti VITAMBULISHO VYETU hivi ni sawa na KODI YA KICHWA? Uongo gani huu?
Haya hilo moja. Je mmesahau USHURU tuliokuwa tukitozwa huko sokoni au barabarani au kwenye vibanda vyetu humu mitaani kwetu? Je mmesahau ule USHURU wa shilingi 500/= hadi 1000/= au 1500/= kwa siku moja kwa kupanga na kuuza vifungu vichache vya nyanya au vitumbua au vitunguu au USHURU wa kiasi hicho kwa kutembeza suruali 5 au 10 za mitumba au kwa viguo 10 vya watoto, MMESAHAU au mnadanganywa na kupotoshwa kwa UONGO na UZUSHI huu wa Lissu!?
Ngoja nimalize kwa kuwapa hesabu ndogo tu ili kuonyesha unafuu wa hizo shilingi 20000/= kwetu sisi wajasiriamali. Shilingi 20000/= ni tozo KWA SIKU 365 AU MWAKA MMOJA! Maana yake ni kwamba tunahitajika kulipa USHURU wa SHILINGI 54/= yaani shilingi HAMSINI NA NNE kwa siku badala ya zile shilingi 500/= au 1000/= au 1500/=. Ni unafuu ulioje! Halafu anaibuka mtu mmoja asiyejua na kufahamu UKWELI kwa vile alikuwa nje ya nchi kwa muda mrefu kiasi cha kusikiliza kila UPOTOFU aambiawo na wapambe wake. Jamani shilingi 54/= kwa siku ndiyo KODI YA KICHWA YA LISSU. Hii ni AJABU NA KWELI. Twende na uongo huu wa kwanza hayo MAUONGO mengine yatafuata au siyo!?