Uchaguzi 2020 Ahadi na Sera za Tundu Lissu katika Uchaguzi Mkuu 2020
Kadoda nguku,

Ngoja nijikite kwenye "UONGO" na UZUSHI wa kwanza juu ya vitambulisho vya wajasiriamali. Ni hivi - ni vizuri watu msiwe wasahaurifu wa mambo yaliyokuwa yakitukuta sisi wajasiriamali. Ni nani asiyejua adha, manyanyaso na usumbufu tuliokuwa tukipewa na mgambo na viongozi mbalimbali katika sehemu zetu za kazi kama huko kwenye masoko, kwenye site mbalimbali au huko mabarabarani tulikokuwa tukipanga vitu, bidhaa au biashara zetu. Kweli mmeshasau mateso hayo ya kuporwa au kumwagiwa bidhaa zetu na hata wakati mwingine kukamatwa na kupelekwa mbele ya PILATO na kuhukumiwa faini za ajabu ajabu ajabu na hata VIFUNGO? Kweli mmesahau kiasi ambacho mnasimama na kusikiliza UONGO NA UZUSHI wa Lissu eti VITAMBULISHO VYETU hivi ni sawa na KODI YA KICHWA? Uongo gani huu?

Haya hilo moja. Je mmesahau USHURU tuliokuwa tukitozwa huko sokoni au barabarani au kwenye vibanda vyetu humu mitaani kwetu? Je mmesahau ule USHURU wa shilingi 500/= hadi 1000/= au 1500/= kwa siku moja kwa kupanga na kuuza vifungu vichache vya nyanya au vitumbua au vitunguu au USHURU wa kiasi hicho kwa kutembeza suruali 5 au 10 za mitumba au kwa viguo 10 vya watoto, MMESAHAU au mnadanganywa na kupotoshwa kwa UONGO na UZUSHI huu wa Lissu!?

Ngoja nimalize kwa kuwapa hesabu ndogo tu ili kuonyesha unafuu wa hizo shilingi 20000/= kwetu sisi wajasiriamali. Shilingi 20000/= ni tozo KWA SIKU 365 AU MWAKA MMOJA! Maana yake ni kwamba tunahitajika kulipa USHURU wa SHILINGI 54/= yaani shilingi HAMSINI NA NNE kwa siku badala ya zile shilingi 500/= au 1000/= au 1500/=. Ni unafuu ulioje! Halafu anaibuka mtu mmoja asiyejua na kufahamu UKWELI kwa vile alikuwa nje ya nchi kwa muda mrefu kiasi cha kusikiliza kila UPOTOFU aambiawo na wapambe wake. Jamani shilingi 54/= kwa siku ndiyo KODI YA KICHWA YA LISSU. Hii ni AJABU NA KWELI. Twende na uongo huu wa kwanza hayo MAUONGO mengine yatafuata au siyo!?
 
Najikita kwenye hoja ya VITAMBULISHO

Safi sana kwani waliokuwa wanawafanyia hivyo wamachinga ni watu tofauti na ccm, ? Kwa nini hivyo kitambulisho visitolewe bure ? Tatizo watu kulazimishwa na kuitungia sheria
 
Safi sana kwani waliokuwa wanawafanyia hivyo wamachinga ni watu tofauti na ccm, ? Kwa nini hivyo kitambulisho visitolewe bure ? Tatizo watu kulazimishwa na kuitungia sheria
Na wewe unataka utuaminishe kuwa waajiriwa wote ni wa CCM? UONGO mwingine huu! Yaani unasema waajiriwa wa serikali kama hao MIGAMBO kweli CHADEMA hawamo kwenye hizo Payroll, kweli au ni mwendelezo ule ule wa UONGO na UZUSHI usio kifani, mnaoiga kwa Lissu!? Kuna msemo wa Kiswahili usemao " Aliyezoea vya kunyonga vya kuchinja haviwezi". Hatuoni taabu kuchangia kidogo kwa maendeleo yetu.
 
Yule mgomea ubunge kule singida ndiyo hoja yake eti wapinzani wataiuza nchi kwa mabeberu
Hoja hiyo ya Lissu na wenzake wakishinikizwa na akina AMSTERDAM ya kutaka kuuza nchi yetu na utajiri wetu kwa mabeberu INGALI PALE PALE. Hii ni kwa sababu Lissu amekuwa akitayarishwa na hao mabeberu kwa miaka mingi tangu akiwa kiongozi kwenye NGO moja iitwayo LEAT yaani Lawyers Environment Association of Tanzania. Lissu amekuwa akitayarishwa kwa miaka mingi na nadhani hata hiyo mipango ya hizo risasi 16 za ndege alizopigwa ni MUENDELEZO huo kwa nia na lengo OVU la kumuibua SASA, wakidhani Watanzania tumelala. Tunajua mengi hivyo watu msije na vioja humu vya ajabu ajabu kama hamjui ukweli. Msichokoze simba aliyelala jamani!
 
A m not of your calibre, you can brainwash others
 
Dalili za mtu kushindwa hoja ni kuanza kumvamia na kumuattack mwenziwe. Hili kwa Bara ni kubandika hoja dhaifu za Lissu anashirikiana na mabeberu. Kule visiwani Maalim Seif anataka kurudisha waarabu. I think you know what I mean, ni hoja za kitoto kabisa.
 
A m not of your calibre, you can brainwash others
Lete hoja Benny Haraba siyo kuanza ku - judge watu humu JF. Ni watu wachache sana wanafahamika humu JF, hao ndio unaweza kujipima nao au kwao lakini siyo kwa wale usiowajua ndugu. Humu JF ni kama Newyork - the Boiling Pot.
 
Kwahiyo mkuu unatetea kabisa watu wapate ajira kwa kudanganya elimu zao?
 
Nilivosoma heading ya uzi wako tu nikapata hamasa ya kusoma zaidi ulichondika ila cha kushangaza nakuta umeandika hoja za kipuuzi kabisa, mfano unavosema masilahi ya wafanyakazi kuongezewa mishahara na marupu rupu, wenye vyeti feki kurudishwa kazini sijui, wastaafu kupata mafao nusu nusu ama kutopata kabisa kam utaacha kazi kabla umri wa kustaafu, ivi kwa akili zako unadhani ni asilimia ngap ya wapiga kura walioajiriwa?

Hivi unajua kuw zaid ya asilimia 70 ya watanzania ni watu wasioajiriwa na walio wengi ni wakulima tu au wafanya biashara wadogo wadogo ? Unadhan hili kundi kubwa la wapiga kura litampigiaje kura tundu lisu wakati wao si waajiriwa serikalin na mambo ya mafao na vikokotozi wao inawahusu nini ? Hata wenye vyeti feki kwa mfano warudishwe kazin wakafanye nn wakat waliingizwa kiharamu ? Ivi Tundu lisu anadhan hii nchi ni ya ku faidiwa na wasomi tu?

vipi kuhusu wasiosoma wanaolima huko vijijini wahatakiwi kufaidi national cake ? National cake inatakiwa igawanwe sawa bhan haijalishi umesoma au haujasoma, umeajiriwa au haujajiriwa but the national cake should be distributed equally to all tanzanians 🙂🙂🙂, karibu robo tatu ya watanzania wanaishi huko vijijini wanalima huko alafu ww unaenda kutupigia habar za kuongeza mshahara cjui marupu rupu inamuhusu nn mtu anaelima kjijini huko, kikokotozi kinamuhusu nn yeye, vyeti vyeki warudishwe kazini ili wakafanye nn, shenzi kabisa, Mm Tundu lisu nimemuelewa kwenye suala la haki za binadamu na uhuru wa watu kujieleza tu labda na katiba mpya ila kwingine simwelewi kabisa ✖
 
Hoja za mabeberu zilikuwa za kudanganyia wananchi wakati wa kupamaba na ukoloni. Kwa sasa hazilipi
Ebo huyu vipi? Unasema kwa sasa mabeberu hawapo? Huu sasa aidha ni ushabiki uliopitiliza au kutokujua mambo - nasita kusema huu ni ujinga - kwani sasa hivi mtaibuka na kusema nimetukana. Hapana ujinga siyo TUSI bali UPUMBAVU ndiyo tusi! Mbeberu wapo, tena wapo LIVE na matendo yao, mazao yao na matunda yao tunayaona in the forms of Lissu.
 
Malipo ya serikali siku hizi yanalipwa kwa control number vipi Vitambulisho vya Mjasiriamali vililipiwa kwa style Hiyo au walikuwa wanakusanya tu hela
 
Malipo ya serikali siku hizi yanalipwa kwa control number vipi Vitambulisho vya Mjasiriamali vililipiwa kwa style Hiyo au walikuwa wanakusanya tu hela
Kwa ID zile za kwanza walipewa ma - RC. Hao ndio walijua namna ya kurudisha hizo pesa huko Serikalini LAKINI vingine vyote baada ya hapo, ni kwa CONTROL NUMBER kwa kwenda mbele, ambazo zinapatikana kwenye ofisi zote za Serikali za Mitaa!
 
Kadoda nguku,

Mkuu upo sahihi

Akazie pia

1. Bima ya afya
2. Katiba mpya
3. Ukabila katika Ajira
4. Pesa za pembejeo walizozulumiwa mawakala
5. Board ya mikopo tanzania na mateso kwa wanufaika na makato yake
6. PAYE 18% kwa wafanyakazi
7. Bomoa bomoa nyumba za watu.
 
Hoja nyingine akandamize ni mauaji na watu waliopotezwa Bn Saanane Azory Gwanda , Simon Kanguye , Akwilina , Lwajabe , ya pili watu waliofungwa kwa kuonewa na kumbambikiza kesi ,Tito Magoti , Theodore Gyan , Rugemalila na wengineo , watu wakikumbushwa hawa wanapata machungu sana bila kusahau waliobomolewa nyumba zao Kimara na kwingine.

IMG_20200908_232916.jpg
IMG_20200831_131922.jpg
 
Mimi si mwandishi muzuri! Napenda kuwajulisha ukweli mchungu usiozungumzwa popote kwa woga wa kupoteza au kupotea kuwa kati ya 100% ya wana CCM salio jinsi kisha na watakaopiga kura, 90% watampigia Lissu wa yupinzani, sababu chache ni hizi:

Moja, Magufuli aliua njia zao za kujipatia rizki! Wengi wakajenga visasi na wakakosa pa kuyasemea haya sasa watakua sema kwa vitendo

Pili, Suala la ununuzi wa Wapinzani kisha kuwapa madaraka huku wenyeji wakitolewa kauli za kishenzi ni uthibitisho mzuri mwingine, munamkumbuka Shonza? Unajua alitoka wapi?

Tatu, Kuwachagua watu wenye vinasaba naye vya kiukoo au kiukabila! Huku wengi kuwaacha wakiwa wanakufa njaa.

Nne, Kuwaweka watu anaowataka yeye kuwa Wagombea ubunge na kuwaacha ware waliochaguliwa kihalali na Wajumbe.

Tano, Dharau zinazooneshwa waziwazi na top layer leadership kwamba wao wanatosha kukiongoza chama chetu.

Unaweza kuyaongeza kadiri umavyokumbuka
 
Kuzuia nyongeza ya mishahara na kupanda madaraja kwa watumishi.

Maisha ya watumishi yamekuwa magumu kuliko awamu zingine. Waliopanda toka 2015 kabla hajaingia madarakani hawajapandishwa hadi leo.

Kura hizo anaenda kuzikosa,zimeenda kwa Lissu.
 
Back
Top Bottom