Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC): Hatuungi mkono Mkataba wa Bandari. Sauti ya Watu ni sauti ya Mungu
Hiyo kampuni ni nzuri zaidi hata kuliko ulivyoieleza,ila kwenye mkataba kuna vipengele kadha wakadha k.m ilivyoelekezaa na TLS vinapaswa kurekebishwa
Hilo liko wazi.
Suala lililopo hapa MAASKOFU hii issue inawahusu nini mpk waingilie kazi isio ya kanisa?

Wamekosa wanakondoo wa kuwauzia maji ya upako mpk wageuze makanisa kuwa vyama vya siasa?
 
Kwa kweli kanisa limetuwakilisha vizuri sana Watanzania kuliko serikali yetu.
Wewe nani hata usiwasilize unaowaongoza?!
Kanisa tunaomba msiishie tu kutoa maoni.
Kuna watu wanakosoa eti Kanisa lisichanganye dini na siasa! Hivi dini na siasa unazitenga vipi? Kwa upande wa Waislamu Mtume Muhammad alipopigana vita vingi 1. Uhud, Khandak, Badr, na Hunayn, je alichanganya dini na siasa? Kwa Wakristo Yohana mbatizaji alimkemea mtawala Herode kwa uovu wa kumuona mke wa ndugu yake akakatwa kichwa, (Marko 6:18), Daniel alikataa amri haramu ya utawala wa Darius (Daniel 6:13) akatupwa kwenye shimo la Simba.Tiini mamlaka ya watawala hata kama ni ya haramu? Kwa kifupi dini na siasa unazitenga vipi?

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Mimi siyo Mkatoliki, ila naufahamu huu ukweli mchungu wa historia :

Mosi, Kanisa la Roma limekuwepo miaka 2000 sasa. Katika hii miaka 2000, limekutana na watu kama Mohammed S.A.W., Kalifa Ummar, Chinggis Khan, Tamerlane, Henry VIII, Napoleon, Gustav, Hitler, Mehmed, Stalin. Hili peke yake linapaswa kukufanya ufikiri kama mtu mwenye akili timamu.

Pili, Kanisa la Roma ndiyo taasisi ya kidini kongwe zaidi hapa duniani. Madhehebu mengi yalikuwepo ila leo hii hayapo. Hujiulizi nini kinafanya Roma iendelee kuwepo mpaka leo hii hata baada ya dola lao la Rumi kuanguka vibaya, ???

Tatu, Kanisa la Roma limeshambuliwa na madikteta hatari ambao wewe na mimi tunawasoma kwenye historia. Watu kama Odoacer, Robespierre, Napoleon Bonaparte walipambana sana na kanisa Katoliki na kutaka kulifutilia mbali, lakini mwishowe ilishindikana, wao wakaenda ila Kanisa bado lipo.

Nne, Kanisa la Roma limekuwepo vipindi vya watu kama Adolf Hitler na Benitho Mussolini, na hawakuweza kulifuta hata kidogo japo walionesha wazi kutolipenda hili kanisa. Tena kuna baadhi ya viongozi wa hili kanisa walishawahi kuwa mafashisti. Kiufupi kama ni michezo michafu ya kisiasa, hii taasisi ambayo inajiita kanisa takatifu la mitume ndiyo mtaalamu. Mikono yake inanuka damu za maelfu wa watu wasio na hatia.

Tano, Kanisa la Roma lilisaidia sana Marekani kuanguasha Ukomunisti kule Barani Ulaya. Kiufupi ni kwamba, The Jesuits waliweza kuwashinda hadi KGB kwenye baadhi ya mambo ambayo yalipelekea maeneo yenye wakatoliki wengi kama Poland yasitawalike hadi kuleta taharuki kubwa ndani ya Urusi ya Kisovieti.

Sita, Raisi wa kwanza wa Tanganyika alitakiwa awe ni Chief Mareale ambaye aliandaliwa na CIA. Ila Raisi akawa kijana Mkatoliki ambaye alifundishwa siasa za Kifabiana kule Scotland kwa mkono wa Waingereza wakishirikiana na Wakatoliki. Baba yetu wa Taifa alisomeshwa na kuandaliwa na hawa watu hadi akawa Raisi.

Saba, kukupasha tu, shule za seminari ndiyo imekuwa sehemu ambazo majasusi na maafisa wengi wa kwenye vyombo vyetu nyeti hapa nchini wanachukuliwa. Tena mbaya zaidi ni kwamba huko TISS wamejaa mapadri, wachungaji, waganga wa kienyeji na masheikh wengi tu. Halafu anaibuka mtu mwenye mawazo mufilisi akidhani anaweza kufanya anachotaka na yasimkute.

Nane, moja ya sababu iliyomfanya Marehemu Yohana apate shida kwenye uongozi wake ni kitendo cha kuanzisha vita vya wazi-wazi na hawa jamaa. Ilifika kipindi kuna mapadri waliondolewa nchini kwenda kusoma kama njia ya kulinda uhai wao dhidi ya hasira za Bwana Yohana. Kuna maaskofu wakubwa walitishwa waziwazi na Yohana. Mambo ya Yohana yaligeuka magumu mno siku zake za mwisho.

NB 1: Unadhani TISS iliyoanzisha miaka ya 60's ndiyo itaweza kuwadhibiti kweli ???

NB 2: Katika historia ya dunia ni Queen Elizabeth, King Gustav, Tsar Ivan na Lincoln ndiyo wamewahi kuwagalagaza wakatoliki kwenye mtifuano wa kisiasa. Huenda Raisi wetu Samia akaingia kwenye hii orodha. Aendelee kutunisha misuli asiwaogope, waislamu wenzake wanamuunga mkono.

NB 3: Tanzania ni nchi inayoongozwa kwa makubaliano na uwiano (Compromise & Balance of Power) baina ya dini hizi kubwa mbili kwasababu ndizo zina ushawishi hapa nchini. Tunapokezana na kuvumiliana, hakuna kiongozi anayetakiwa kuvuka mstari mwekundu na kuharibu uwiano. Ila sasa naona tumeshavuka, sasa tusubiri matokeo.
 
Askofu anaeweza kukuzia maji ya dawasa akakuaminisha wewe kuwa ni maji ya uzima wa milele na ukanunua kijiko kimoja shs elf 50 huyo sio mjinga hata kidogo.
Nadhani mjinga unamjua
Ona hii Mbumbumbu
 
Tafakuri Tunduizi kuhusu tamko la Maaskofu

Tamko la maaskofu linesema SAUTI YA WENGI NI SAUTI YA MUNGU mimi nawakumbusha tu ya KAIZARI AACHIWE KAIZARI na ya MUNGU APEWE MUNGU


Nimelisoma TAMKO LA MAASKOFU na mimi nimeona mambo haya

Mimi nlichoona:
Badala ya kutoa maoni kwamba mkataba urekebishwe (kitu ambacho watanzania walio wengi ndio wanachotaka) tamko linataka huu mkataba uachwe kabisa, yani usiendelee hapa KANISA LIMEIBGILIA SERIKALI kutimiza wajibu wake maana wameipa amri serikali iachane mara moja na huu mkataba ikiwa serikali itauacha huu mkataba wa uwekezaji ni dhahiri kuwa ile kauli ya ALMARHUM SHEIKH ILUNGA HASSAN KAPUNGU rahimallahu kuwa nchi hii KANISA LINA NGUVU KULIKO SERIKALI na hapo ndipo MFUMO KRISTO UNADHIHIRI kwa kuonesha nchi hii inaendeshwa na KANISA

Cha pili: Tamko linataka Bandari tuiendeshe wenyewe, kimsingi na kwa spidi ya sasa kama watanzania bado hatuwezi kuendesha bandari na kufikia viwango hitajika

Cha Tatu: ukiangalia namba 4, tamko linasema “ tukiweka ubia na makampuni yenye ubobezi wa kiteknolojia kutoka sehemu mbalimbali duniani, na sio ubia kutoka nchi moja, tukiweka mikataba yenye tija”..

Hii inamaanisha bado tunahitaji uwekezaji.. sasa tamko linaposema sio uwekezaji wa nchi Moja, kwani Ticts ilikuwa ya nchi ngapi? Si walikuwa wachina pekee? , na tamko linaposema nchi mbali mbali duniani, Dubai(UAE) si ni mojawapo ya nchi zilizopo duniani kama ilivyokuwa China kuendesha Ticts kwa miaka 30?

Hili tamko nadhani lingesema vipengele vya mkataba viwekwe sawa.

Na linapokuja swala la ubobezi, Hata huko Europe na Marekani wanamtumia huyohuyo DP sasa sijui tamko linataka ubobezi gani?!

Kingine, tamko linaposema makampuni ya ndani binafsi ndo yaingie ubia na wawekezaji wa nje, tayari serikali imeshapoteza, wakati sekta kama hizi lazima serikali yenyewe iingie makubaliano na mwekezaji moja kwa moja ili kuwe na direct control, kuliko kupitia kwa kampuni binafsi

Mwisho bila kupepesa maneno, hili tamko halimtaki Mwarabu awekeze, ila kwa kusema “ kutoka sehemu mbali mbali duniani” ni dhahiri kwamba ingekuwa ni nchi ambayo haitoki ukanda wa mashariki ya kati kama Ulaya, basi hili tamko lisingetoka, kama ambavyo halikutoka kwenye mikataba mibovu ya madini, ununuzi wa ndege, na mikataka mingine mibovu. Nadhani baraza la MAASKOFU wanataka kutwambia kuwa itakuwa vizuri zaidi mwekezaji akitoka Vatican au Ulaya na iwe kampuni ya Wazungu Wakristo ila tu wamejificha nyuma ya kichaka wanachokijua wao,

Hapa kanisa limekumbuka kauli ya SAUTI YA WENGI NI SAUTI YA MUNGU ila wamesahau ya

Kaizari aachiwe kaizari na ya Mungu apewe Mungu

Hebu turudi nyuma kwenye historia Kanisa ndani ya nchi hii linapata wapi Moral authority wakati kanisa hilo haohao TEC na CCT walisaini mkataba na serikali 1992 wa kula mabilioni ya PESA maarufu kwa jina la MoU

Mkataba wenye masharti magumu tu kuwa kulipo na hospitali za kanisa serikali isijenge za kwake ipeleke wafanyakazi hapo na mishahara ya hizo hospitali za kanisa itoke serikalini hii ni hatari sana

Serikali imeanza kujenga hospitali zake kila wilaya hili kwao limekuwa tatizo kubwa sana

Hebu tujikumbushe machache kuhusu KANISA NA KADHIA MBALIMBALI ZA TANZANIA

Tutakwenda hivi kwa amri ya Maaskofu hadi lini?

Maaskofu hawaitaki historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika kwa kuwa inawaweka Waislam juu, historia hii ikafutwa.

Ushahidi upo.

Maaskofu hawakuitaka East African Muslim Welfare Society (EAMWS) matokeo yake ikapigwa marufuku kwa amri ya serikali mwaka wa 1968 kwa kuwa ilikuwa inajenga Chuo Kikuu cha Waislam.

Ushahidi upo.

Maaskofu hawakupenda kuona Waislam wanaelimika zikafanywa kila aina ya mbinu kuhakikisha kuwa watoto wa Waislam hawapati elimu ya sekondari wala Chuo Kikuu.

Ushahidi upo.

Maaskofu hawakutaka Organisation of Islamic Conference (OIC) ijenge Chuo Kikuu Tanzania katika miaka ya 1970 na kweli chuo hakikujengwa.

Chuo kikapelekwa kujengwa Mbale, Uganda.

Maaskofu wakakataa Zanzibar kujiunga na OIC na haikujiunga.

Ushahidi upo.

Maaskofu wamekataa kuzirejesha Mahakama za Kadhi zilizovunjwa mwaka wa 1963 na mahakama hakika hazikurejeshwa.

Ushahidi upo.

Yapo mengi lakini tutafakari haya kwa sasa.

Tanzania hii itaendeshwa kwa matakwa ya Maaskofu hadi lini?


JE NCHI HII BAADA YA KUSAINI MoU mwaka 1992 na makanisa ndio makanisa yamepata idhini ya kuiendesha Tanzania?

Na huu ndio MFUMO KRISTO UNAVYOENDESHA TANZANIA

WATANZANIA WENZANGU

Nawaasa tuiache serikali ifanye kazi yake ina vyombo vyake na wataaalamu wake tuliheshimu bunge na serikali katika kutekeleza miradi ya maendeleo kwa Watanzania


Sisi Watanzania WAZALENDO wenye nchi hii tunasema

Kazi iendeleeeeeeee

Sent from my SM-A045F using JamiiForums mobile app
Acha ujinga. ccm waibe mali za umma afu mseme ya kIzari. Watu wakae kimya noooo
 
Niko pamoja na TEC, tuingie kwenye mfungo wa kurudusha Bandarin yetu na kuwapiga upofu vibaka wote na madalari wa dpw.

Mkataba upitiwe upya tuweke nati za kulinda mali zetu
 
Back
Top Bottom