Hiyo kampuni ni nzuri zaidi hata kuliko ulivyoieleza,ila kwenye mkataba kuna vipengele kadha wakadha k.m ilivyoelekezaa na TLS vinapaswa kurekebishwa
Hilo liko wazi.
Suala lililopo hapa MAASKOFU hii issue inawahusu nini mpk waingilie kazi isio ya kanisa?

Wamekosa wanakondoo wa kuwauzia maji ya upako mpk wageuze makanisa kuwa vyama vya siasa?
 
Kwa kweli kanisa limetuwakilisha vizuri sana Watanzania kuliko serikali yetu.
Wewe nani hata usiwasilize unaowaongoza?!
Kanisa tunaomba msiishie tu kutoa maoni.
Kuna watu wanakosoa eti Kanisa lisichanganye dini na siasa! Hivi dini na siasa unazitenga vipi? Kwa upande wa Waislamu Mtume Muhammad alipopigana vita vingi 1. Uhud, Khandak, Badr, na Hunayn, je alichanganya dini na siasa? Kwa Wakristo Yohana mbatizaji alimkemea mtawala Herode kwa uovu wa kumuona mke wa ndugu yake akakatwa kichwa, (Marko 6:18), Daniel alikataa amri haramu ya utawala wa Darius (Daniel 6:13) akatupwa kwenye shimo la Simba.Tiini mamlaka ya watawala hata kama ni ya haramu? Kwa kifupi dini na siasa unazitenga vipi?

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Mimi siyo Mkatoliki, ila naufahamu huu ukweli mchungu wa historia :

Mosi, Kanisa la Roma limekuwepo miaka 2000 sasa. Katika hii miaka 2000, limekutana na watu kama Mohammed S.A.W., Kalifa Ummar, Chinggis Khan, Tamerlane, Henry VIII, Napoleon, Gustav, Hitler, Mehmed, Stalin. Hili peke yake linapaswa kukufanya ufikiri kama mtu mwenye akili timamu.

Pili, Kanisa la Roma ndiyo taasisi ya kidini kongwe zaidi hapa duniani. Madhehebu mengi yalikuwepo ila leo hii hayapo. Hujiulizi nini kinafanya Roma iendelee kuwepo mpaka leo hii hata baada ya dola lao la Rumi kuanguka vibaya, ???

Tatu, Kanisa la Roma limeshambuliwa na madikteta hatari ambao wewe na mimi tunawasoma kwenye historia. Watu kama Odoacer, Robespierre, Napoleon Bonaparte walipambana sana na kanisa Katoliki na kutaka kulifutilia mbali, lakini mwishowe ilishindikana, wao wakaenda ila Kanisa bado lipo.

Nne, Kanisa la Roma limekuwepo vipindi vya watu kama Adolf Hitler na Benitho Mussolini, na hawakuweza kulifuta hata kidogo japo walionesha wazi kutolipenda hili kanisa. Tena kuna baadhi ya viongozi wa hili kanisa walishawahi kuwa mafashisti. Kiufupi kama ni michezo michafu ya kisiasa, hii taasisi ambayo inajiita kanisa takatifu la mitume ndiyo mtaalamu. Mikono yake inanuka damu za maelfu wa watu wasio na hatia.

Tano, Kanisa la Roma lilisaidia sana Marekani kuanguasha Ukomunisti kule Barani Ulaya. Kiufupi ni kwamba, The Jesuits waliweza kuwashinda hadi KGB kwenye baadhi ya mambo ambayo yalipelekea maeneo yenye wakatoliki wengi kama Poland yasitawalike hadi kuleta taharuki kubwa ndani ya Urusi ya Kisovieti.

Sita, Raisi wa kwanza wa Tanganyika alitakiwa awe ni Chief Mareale ambaye aliandaliwa na CIA. Ila Raisi akawa kijana Mkatoliki ambaye alifundishwa siasa za Kifabiana kule Scotland kwa mkono wa Waingereza wakishirikiana na Wakatoliki. Baba yetu wa Taifa alisomeshwa na kuandaliwa na hawa watu hadi akawa Raisi.

Saba, kukupasha tu, shule za seminari ndiyo imekuwa sehemu ambazo majasusi na maafisa wengi wa kwenye vyombo vyetu nyeti hapa nchini wanachukuliwa. Tena mbaya zaidi ni kwamba huko TISS wamejaa mapadri, wachungaji, waganga wa kienyeji na masheikh wengi tu. Halafu anaibuka mtu mwenye mawazo mufilisi akidhani anaweza kufanya anachotaka na yasimkute.

Nane, moja ya sababu iliyomfanya Marehemu Yohana apate shida kwenye uongozi wake ni kitendo cha kuanzisha vita vya wazi-wazi na hawa jamaa. Ilifika kipindi kuna mapadri waliondolewa nchini kwenda kusoma kama njia ya kulinda uhai wao dhidi ya hasira za Bwana Yohana. Kuna maaskofu wakubwa walitishwa waziwazi na Yohana. Mambo ya Yohana yaligeuka magumu mno siku zake za mwisho.

NB 1: Unadhani TISS iliyoanzisha miaka ya 60's ndiyo itaweza kuwadhibiti kweli ???

NB 2: Katika historia ya dunia ni Queen Elizabeth, King Gustav, Tsar Ivan na Lincoln ndiyo wamewahi kuwagalagaza wakatoliki kwenye mtifuano wa kisiasa. Huenda Raisi wetu Samia akaingia kwenye hii orodha. Aendelee kutunisha misuli asiwaogope, waislamu wenzake wanamuunga mkono.

NB 3: Tanzania ni nchi inayoongozwa kwa makubaliano na uwiano (Compromise & Balance of Power) baina ya dini hizi kubwa mbili kwasababu ndizo zina ushawishi hapa nchini. Tunapokezana na kuvumiliana, hakuna kiongozi anayetakiwa kuvuka mstari mwekundu na kuharibu uwiano. Ila sasa naona tumeshavuka, sasa tusubiri matokeo.
 
Askofu anaeweza kukuzia maji ya dawasa akakuaminisha wewe kuwa ni maji ya uzima wa milele na ukanunua kijiko kimoja shs elf 50 huyo sio mjinga hata kidogo.
Nadhani mjinga unamjua
Ona hii Mbumbumbu
 
Askofu anaeweza kukuzia maji ya dawasa akakuaminisha wewe kuwa ni maji ya uzima wa milele na ukanunua kijiko kimoja shs elf 50 huyo sio mjinga hata kidogo.
Nadhani mjinga unamjua
Mbona unarudia kuniquote mara mbili mbili?
 
Acha ujinga. ccm waibe mali za umma afu mseme ya kIzari. Watu wakae kimya noooo
 
Niko pamoja na TEC, tuingie kwenye mfungo wa kurudusha Bandarin yetu na kuwapiga upofu vibaka wote na madalari wa dpw.

Mkataba upitiwe upya tuweke nati za kulinda mali zetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…