Upepo wa Pesa
JF-Expert Member
- Aug 8, 2015
- 21,600
- 35,158
Filosofia inayosomwa na mapadri sio ya kitoto aisee..Andiko la maaskofu limeandikwa na wasomi wa falsafa wana data kamili na wamefanya utafiti wa kutosha HALITAPINGWA kwa mipasho na sentence za kuungaunga
Sent using Jamii Forums mobile app
Haijawa na hadhi hiyo. Tanzania ni Kigango tu kwa TECTz siyo parokia
Safi!Tamko hilo limetolewa leo na Padri Kitime
Kwa Mujibu wa Padri kitime ,TEC imeamua kusimama na wananchi kwenye suala la bandari
Padri kitime amesisitiza kwa sasa serikali inataka kuligawa Taifa kwenye pande mbili wanaokubaliana na wasiokubaliana,lakini wengi wanaokubaliana wanahofi tu kwa kuwa wamepewa dhamana ya uongozi
Padri kitime amesisitiza kuwa wameita wataalamu wote mpaka watu wa wizara wamewaita hivyo wamejiridhisha kuwa mkataba wa serikali na Dp world haufai
TEC inashangazwa na serikali kutaka kuanza kuwazuia watu wasiongelee mambo ya Taifa lao
Padri kitime anahoji kama mkataba unafaa kwanini serikali inahangaika kutaka kubadili sheria lukuki ili ziendane na mkataba wa bandari na kumruhusu Dp world ya Dubai
======
"Ndugu zangu nawasihi mjihadhahari na wote wanaoleta mafarakano na vipingamizi kinyume cha mliyopokea (mapokeo). Waepukeni.Kwa maana watu kama hao wanatumikia tamaa zao kwa kutumia maneno matamu ya kudanganya kupotosha mioyo ya watu wanyofu" (Warumi 16:17-18). Sisi Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania,
1. Tunatambua kuwakwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977), "Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nchi inayofuata misingi ya demokrasia na haki ya kijamii, na kwa hiyo - (a) wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na Serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi kwa mujibu wa Katiba hii; (b) lengo kuu la Serikali litakuwa ni ustawi wa wananchi; (c) Serikali itawajibika kwa wananchi; (d) wananchi watashiriki katika shughuli za Serikali yao kwa mujibu wa masharti ya Katiba" (Rejea Ibara 8, ibara ndogo 1); hivyo ni lazima Serikali iwasikilize wananchi.
2. Kwa kutambua kwamba mamlaka ya Serikali yanatoka kwa wananchi, sisi Maaskofu wa Kanisa Katoliki la Tanzania, tumezisikiliza sauti zao, tumeisikiliza Serikali, na wadau wengine wa maendeleo,tukasali na kutafakari, na hivi tunatamka ifuatavyo:
2.1. Tukizingatia yaliyojiri na yanayoendelea katika jamii ya Tanzania tangu Mkataba huu uwekwe hadharani, taharuki kutokana na mijadala ya hadharani, mijadala ambayo imeligawa Taifa.
2.2. Na tukizingatia kuwa si mara yetu ya kwanza kutoa matamko kama hili kuhusu masuala yanayohusu jamii yetu;
2.3. Na kwa kurejea ibara za Mkataba tajwa hapo juu ambazo zina utata kwa uwekezaji wenye tija kwa Watanzania wa sasa na vizazi vijavyo;
2.4. Na tukiwa tunayashuhudia mashinikizo ya marekebisho ya sheria yanayokusudiwa kufanywa ili kuulinda Mkataba huu ambao Bunge la Tanzania limeuridhia hali tukiona ukiukwaji wa utawala wa sheria.
KWA HIYO:
3. Tukisukumwa na dhamiri iliyo na lengo la kulinda rasilimali, mshikamano, amani, uhuru, na umoja wa kitaifa; tunathubutu kusema kuwa baada ya miaka 63 ya uhuru wa nchi hii, wananchi hawajapenda kuiachia bandari ya Dar es Salaam apewe mwekezaji mmoja aiendeshe,kwa vile Watanzania wenyewe wana uzoefu wa kuiendesha.
4. Tunaona kuwa ni muhimu sasa kuendelea kujenga uwezo wa KITAIFA, kwa sekta zetu za umma na binafsi za Kitanzania tukiweka ubia na makampuni yenye ubobezi wa kiteknolojia kutoka sehemu mbalimbali duniani, na siyo ubia wa kutoka nchi moja, tukitumia mikataba yenye tija tuliyoandaa wenyewe juu ya mashirika yetu ya kibiashara.
5. Tunakiri kuwa utaratibu wa Serikali kuweka wawekezaji kutoka nje tu katika njia kuu za uchumi umetukosesha uendelevu wa vitega uchumi vyetu hasa pale wawekezaji wanapoondoka. Hivyo, bandari ikiwa ni moja ya njia kuu na ya asili ya uchumi inayotuwezesha kufanya biashara kubwa na mataifa mbalimbali, ni lazima iendelee kuwa biashara ya Watanzania wenyewe na ibaki mikononi mwetu hata kama tunaingia ubia wenye tija.
6. Kwa kurejea jitihada tulizofanya kuelewa Mkataba huu na kutoa ushauri wetu ambao haujazaa matunda mpaka sasa,na tukirejea mikutano yetu na Serikali katika ngazi za juu, ya tarehe 12 na 26 Juni mwaka huu 2023:
6.1. Tumefuatiliakwa umakini mijadala, maoni, mapendekezo na vilio vya wananchi walio wengi, ambao ni wamiliki wa bandari na rasilimali zote, na tumetambuakuwa wananchi walio wengi hawautaki Mkataba huu ambao unampa mwekezaji wa nje mamlaka na haki ya kumiliki njia kuu za uchumi kama zilivyobainishwa kwenye Mkataba huu.
6.2. Tumebaini kuwa kama nchitumeshawekeza na kuendeleza bandari, reli, na bandari kavu huku tukiziendesha wenyewe.Hii ndiyo shauku ya wananchi, kusudi tuendelee kujenga uwezo wetu. Hali kadhalika, tumegundua mapungufuyetu ya uendeshaji wa bandari;vile vile tunao uwezo wa kuendelea kujizatiti kurekebisha mapungufu yanayojitokeza, wakati njia za kiuchumi zikibaki mikononi mwetu.
6.3. Kuna mifano tosha jinsi Watanzania tulivyoweza kujenga uwezo katika kuendesha mabenki kama vileNMB na CRDB, taasisi nyeti za umma na za binafsi na kadhalika.
7. Sasa kwa vile wananchi walio wengi hawataki uwekezaji wenye masharti mabovu kama haya katika bandari zetu zote; na kwa kuwa Serikali inawajibika kwa wananchi, lazima viongozi wasikilize sauti ya watu, kwani sauti yao ni sauti ya Mungu.
8. Historia imetufundisha kuwa kupuuza sauti ya wananchi kuhusu mikataba kwa siku za nyuma, kumeisababishia nchi hasara kubwa za kiuchumi, ukosefu wa ajira, na mapato ya kuendeshea huduma muhimu kama vile afya, maji na elimu. Tunashuhudia sasa Serikali kutokuwa na uwezo wa kuajiri na kulipa wafanyakazi wa kutosha katika sekta za elimu na afya ijapokuwa wahitimu wa fani hizo wako mitaani bila ajira. Hii ni kwa sababu vyanzo vikubwa vya mapato, mathalani migodi ya madini, vimemilikiwa na kuendeshwa na wawekezaji kutoka njekwa mikataba mibovu.
9. Kupuuza sauti ya wananchi juu ya uwekezaji usiosikia sauti yao. kumewaletea pia wananchi wa maeneo wanayoishi mateso, kama inavyoonekana kwa jamii za Wamasai wa Loliondo, ambao haki zao za kiutamaduni na kijamii zimekiukwa. Uwekezaji umepewa kipaumbele kisicho na tija na raia wa Kimasai wameachwa wakiteseka.
10. Tumeutafakari kwa makini Mkataba huu. Mkataba huu umechochea mgawanyiko wa wananchi katika kupambana na ukiukwaji mkubwa wa utawala wa sheria, kutozingatiwa uhuru wa taasisi za kidemokrasia na mwingiliano wa mihimili yadola hasa Serikali na Bunge na sasa Mahakama inanyemelewa. KamaWatanzania tunapenda kusema kwamba bila uhuru wa taasisi hizi na utawala wa sheria tutaliangamiza Taifa.
11. Ikumbukwe kwamba, kutokana na mjadala mpana wa suala hili la mwekezaji mmoja kwenye bandari za Tanzania, wananchi wenye mawazo tofauti hawajui wamwendee nani ili misimamo yaoiweze kusikilizwa na kuzingatiwa; kwani Wabunge ambao ni wawakilishi wao wamewatelekeza kwa kufungamana na mwekezaji mmoja, kutokana na Bunge kuridhia Mkataba huu mnamo tarehe 10 mwezi Juni, 2023.
12. Hivyo, sisi Maaskofu Katoliki Tanzania wenye jukumu la kusimamia ustawi wa kila mwanadamu tunamwomba Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa mamlaka aliyo nayo asitishe wasilisho la ridhio hili kwa upande wa pili,na vile vile Bunge nalo lifute ridhio la Mkataba huu unaolalamikiwa.
13. Makubaliano haya ya Kiserikali (Inter-Governmental Agreement IGA yana hatari zifuatazo kwa nchi yetu:
13.1. Kuharibu umoja na amani ya nchi yetu. Tukumbuke amani ikivunjika, yaweza kurudi tena baada ya jitihadi ya vizazi vingi. Nchi jirani kadhaa zimethibitisha hili.
13.2. Rasilimali za nchi zinazolindwa kwa pamoja kuwanufaisha baadhi ya raia na hivyo kuleta ubaguzi wa kiuchumi kinyume cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ibara ya 27
Ibara ndogo ya 1, inayosema "Kila mtu ana wajibu wa kulinda maliasilia ya Jamhuri ya Muungano, mali ya mamlaka ya nchi na mali yote inayomilikiwa kwa pamoja na wananchi..."
14. Ibara zifuatazo za Mkataba huu zina matatizo yatakayosababisha nchi kutofikia uhuru wa kiuchumi (economic independence):
14.1. Ibara ya 2 (1): inayohusu lengo la Mkataba huu ambalo ni kuweka utaratibu unaoibana Tanzania kisheria katika kuendeleza, kuboresha na kuendesha bandari zote za bahari na maziwa, maeneo maalum ya uwekezaji, maeneo ya usafirishaji wa mizigo, na maeneo mengine ya kiuchumi.
14.2. Ibaraya 4: inayohusu wigo wa Mahusiano na Utekelezaji unaoitaka Serikali ya Tanzania kuwajibika kuijulisha Dubai kila fursa ya uwekezaji inapojitokeza.Hiiinakinzana na baadhi ya sheria za nchi yetu, kwa mfanosheria ya ushindani na ile ya manunuzi.
14.3. Ibaraya 5: ambapo DPWorldimepewa haki ya kuendeleza, kusimamia na kuendesha miradi pekee yake, wakati Tanzania inabaki na wajibu wa kumwezesha kufurahia haki hiyo.
14.4. Ibaraya 6:inayoitaka Tanzania kuwajibika kuipatia DP World vibali na vivutio vya kutekeleza miradi yake kama Serikali. Hii inapingana na baadhi ya sheria za kiutaratibu.
14.5. Ibaraya 7: inayoitaka Serikali kuwajibika kutoa mamlaka yanayotakiwa na mwekezaji bila ucheleweshaji.
14.6. Ibaraya 8: Haki ya kutumia ardhi ambapo Mkataba unasababisha uvunjifu wa sheria za ardhi na sheria zinazohusu masuala ya ardhi.
14.7. Ibaraya 10: Usiri wa Mkataba ambapo Mkataba unazuia mamlaka nyingine kama TAKUKURU /BUNGE kufuatilia mikataba.
14.8. Ibara za 23 na 24: zenye ugumu wa kujitoa kwenye Mkataba.
HITIMISHO:
15. Ni vyema, ni busara na ni hekima Serikali kuwasikiliza wananchi, maana kutowasikiliza ni kujiletea matatizo makubwa zaidi siku za usoni kwani wananchi hawahawa watavitaka vizazi vijavyo kuondokana na unyonywaji huu, kama tunavyoona kwenye kesi nyingi zinazoendelea sasa hivi katika mahakama za kibiashara za kimataifa dhidi ya mikataba iliyovunjwa na Serikali ya Tanzania. Tukumbuke mikatabaya madini miaka ya '90 viongozi wa dini na asasi za kiraia walipinga uwekezaji wa namna hii, na Serikali ikatumia mamlaka zake kuridhia mikataba hii na tunashuhudia ikivunjwa na nchi kulipa fidia kubwa. sasa hivi
16. Tunasisitiza kwamba SAUTI YA WATU NI SAUTI YA MUNGU, hivyo basi kuwasikiliza wananchi na kufanya maamuzi kadiri wanavyotaka kutailetea serikali heshima kubwa ya kuwa sikivu kwa watu. Kinyume cha haya, Mwenyezi Mungu anatuonya kupitia Nabii Yeremia anaposema: "Kama kapu lililojaa ndege walionaswa, ndivyo nyumba zao zilivyojaa mali za udanganyifu. Ndiyo maana wamekuwa watu wakubwa na matajiri, wamenenepa na kunawiri. Katika kutenda maovu hawana kikomo hawahukumu yatima kwa haki, wapate kufanikiwa, wala hawatetei haki za maskini" (Yeremia 5:27-28).
17. Hivyo tukiwajibika kimaadili, tunaona ni jukumu la serikali kusikiliza wananchi wanaotaka mkataba huu ufutwe. Kwa kuwa tumeonesha kuwa Tanzania tumeshawekeza na kuendeleza bandari, reli na bandari za nchi kavu; niwajibu miradi hii tuiendeshe Watanzania wenyewe huku tukikaribisha ubia tunaoudhibiti wenyewe. Hiki ndicho wananchi wanachokililia kusudi tujenge uwezo wetu wenyewe. Kwa vile tumegundua mapungufu yetu ya uendeshaji wa bandari, tunaweza kujizatiti kurekebisha mapungufu hayo wakati njia za kiuchumi zikibaki mikononi mwetu. Kwa sababu hizo na maelezo yote ya hapo juu, sisi Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania hatuungi mkono Mkataba huu.
Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanzania.
Ni sisi Maaskofu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania:
1. Askofu Mkuu Gervas Nyaisonga - Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki
Tanzania, na Askofu Mkuu wa Mbeya
2. Askofu Flavian Kassala - Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki
Tanzania, na Askofu wa Geita
3. Askofu Mkuu Beatus Kinyaiya OFMCap - Askofu Mkuu wa Dodoma
4. Askofu Mkuu Paul Ruzoka - Askofu Mkuu wa Tabora
5. Askofu Mkuu Yuda Thadei Ruwa'ichi OFMCap - Askofu Mkuu wa Dar es
Salaam
6. Askofu Mkuu Damian Dallu - Askofu Mkuu wa Songea
7. Askofu Mkuu Isaac Amani - Askofu Mkuu wa Arusha
8. Askofu Mkuu Renatus Nkwande - Askofu Mkuu wa Mwanza
9. Mwadhama Protase Kadinali Rugambwa - Askofu Mkuu Mwandamizi wa
Tabora
10. Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa - Askofu wa Iringa
11. Askofu Severine NiweMugizi - Askofu wa Rulenge-Ngara
12. Askofu Augustine Shao CSSp - Askofu wa Zanzibar
13. Askofu Michael Msonganzila - Askofu wa Musoma
14. Askofu Ludovick Minde ALCP/OSS - Askofu wa Moshi
15. Askofu Method Kilaini - Msimamizi wa Kitume wa Bukoba
16. Askofu Joseph Mlola ALCP/OSS - Askofu wa Kigoma
17. Askofu Agapitus Ndorobo - Askofu wa Mahenge
18. Askofu Rogath Kimaryo CSSp - Askofu wa Same
19. Askofu John Ndimbo - Askofu wa Mbinga na Msimamizi wa Kitume wa Njombe
20. Askofu Salutaris Libena - Askofu wa Ifakara
21. Askofu Almachius Rweyongeza - Askofu wa Kayanga
22. Askofu Liberatus Sangu - Askofu wa Shinyanga
23. Askofu Titus Mdoe - Askofu wa Mtwara
24. Askofu Eusebius Nzigilwa - Askofu wa Mpanda
25. Askofu Bernadin Mfumbusa - Askofu wa Kondoa
26. Askofu Prosper Lyimo - Askofu msaidizi wa Arusha
27. Askofu Edward Mapunda - Askofu wa Singida
28. Askofu Beatus Urassa ALCP/OSS - Askofu wa Sumbawanga
29. Askofu Anthony Lagwen - Askofu wa Mbulu
30. Askofu Filbert Mhasi - Askofu wa Tunduru Masasi
31. Askofu Lazarus Msimbe SDS - Askofu wa Morogoro
32. Askofu Simon Masondole - Askofu wa Bunda
33. Askofu Henry Mchamungu - Askofu msaidizi wa Dar es Salaam
34. Askofu Stefano Musomba OSA - Askofu msaidizi wa Dar es Salaam
35. Askofu Wolfgang Pisa OFMCap - Askofu wa Lindi
36. Askofu Christopher Ndizeye - Askofu wa Kahama
37. Askofu Mteule Thomas Kiangio - Askofu mteule wa Tanga
Imetolewa Dar es Salaam,
Tarehe 18 ya Mwezi Agosti Mwaka wa Bwana 2023.
Mhashamu Askofu Mkuu Gervas Pd. Charles Kitima
Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania. Katibu Mkuu wa Baraza.
Yuko TaboraCardinal rugambwa Yuko wapi!?
Waisalam wenzake wanamuunga mkonoMimi siyo Mkatoliki, ila naufahamu huu ukweli mchungu wa historia :
Mosi, Kanisa la Roma limekuwepo miaka 2000 sasa. Katika hii miaka 2000, limekutana na watu kama Mohammed S.A.W., Kalifa Ummar, Chinggis Khan, Tamerlane, Henry VIII, Napoleon, Gustav, Hitler, Mehmed, Stalin. Hili peke yake linapaswa kukufanya ufikiri kama mtu mwenye akili timamu.
Pili, Kanisa la Roma ndiyo taasisi ya kidini kongwe zaidi hapa duniani. Madhehebu mengi yalikuwepo ila leo hii hayapo. Hujiulizi nini kinafanya Roma iendelee kuwepo mpaka leo hii hata baada ya dola lao la Rumi kuanguka vibaya, ???
Tatu, Kanisa la Roma limeshambuliwa na madikteta hatari ambao wewe na mimi tunawasoma kwenye historia. Watu kama Odoacer, Robespierre, Napoleon Bonaparte walipambana sana na kanisa Katoliki na kutaka kulifutilia mbali, lakini mwishowe ilishindikana vibaya mno.
Nne, Kanisa la Roma limekuwepo vipindi vya watu kama Adolf Hitler na Benitho Mussolini, na hawakuweza kulifuta hata kidogo. Tena kuna baadhi ya viongozi wa hili kanisa walishawahi kuwa mafashisti. Kiufupi kama ni michezo michafu ya kisiasa, hii taasisi ambayo inajiita kanisa takatifu la mitume ndiyo mtaalamu. Mikono yake inanuka damu za maelfu wa watu wasio na hatia.
Tano, Kanisa la Roma lilisaidia sana Marekani kuanguasha Ukomunisti kule Barani Ulaya. Kiufupi ni kwamba, The Jesuits waliweza kuwashinda hadi KGB kwenye baadhi ya mambo ambayo yalipelekea maeneo kama Poland yasitawalike hadi kuleta taharuki kubwa ndani ya Urusi ya Kisovieti.
Sita, Raisi wa kwanza wa Tanganyika alitakiwa awe ni Chief Mareale ambaye aliandaliwa na CIA. Ila Raisi akawa kijana Mkatoliki ambaye alifundishwa siasa za Kifabiana kule Scotland kwa mkono wa Waingereza wakishirikiana na Wakatoliki. Baba yetu wa Taifa alisomeshwa na kuandaliwa na hawa watu hadi akawa Raisi.
NB 1: Unadhani TISS iliyoanzisha miaka ya 60's ndiyo itaweza kuwadhibiti kweli ???
NB 2: Katika historia ya dunia ni Queen Elizabeth, King Gustav, Tsar Ivan na Lincoln ndiyo wamewahi kuwagalagaza wakatoliki kwenye mtifuano wa kisiasa. Huenda Raisi wetu Samia akaingia kwenye hii orodha. Aendelee kutunisha misuli asiwaogope, waislamu wenzake wanamuunga mkono.
Lineker hapaLile la shura ya maimamu hukuliona la kijinga lakini.
Tujadili vipengele vya mkataba kama ni vya ovyoTusubiri tamko la Bakwata nalo,maana Mashekh wa mkoa na wasomi wakubwa wakiislaam tayari wanaenda kukutana Dodoma.
Kitima ataichafua nchi.
Ngoja tuone mwisho wa hili sakata.
Utakuta hata saba hukumalizaWaliondila zero kabisa yaani eti wapewe wazawa then tuingie ubia hapa ndo utajua Phd za kupewa zipo kibao ili mradi umsujudie mzungu.
Utumbo mtupu kwa mweny akili timamu .
Point zao ni hizi[emoji117] waendelee kupitisha mali zao ili kufanya biashara kwa mgongo wa kanisa .
Ukiona mtu anakubali lile bandiko mawili hajasoma au hakuelewa collacation baina ya vifungu ,maana wanaandika na katika madai yao hamna muunganiko .
Waanza kupinga uwekezaji ili wapewa wazawa then wanakuja kutaka ubia na watu wa nje[emoji28][emoji28]hapa kuna phd au matope ya kukariri kingereza?
Waliambiwa PD world wanakuja kuwa kweny management au kutumia teknolojia katika uendeshaji je wanakataa lipi na wanakubali lipi?
Tukisema mtasema tuna udini ila kwa akili za kuzaliwa tu ukijua kusoma yale maazimio yao ni utopolo na hawajui kitu vichwa empty.
Mkuu niazime laki basi ntakurudishia. Mjini njaa!Maskin ni wewe yaan ungekuwa unanijua utazimia kwa kifupi naweza kuwekeza hata kwenye bandari Hiyo unayodalalia
Ulikua coma!?Yuko Tabora
Tuhuma za uongooo , nmesoma kuanzia La kwanza mpaka. Chuo Kikuu na waislam.Tafakuri Tunduizi kuhusu tamko la Maaskofu
Tamko la maaskofu linesema SAUTI YA WENGI NI SAUTI YA MUNGU mimi nawakumbusha tu ya KAIZARI AACHIWE KAIZARI na ya MUNGU APEWE MUNGU
Nimelisoma TAMKO LA MAASKOFU na mimi nimeona mambo haya
Mimi nlichoona:
Badala ya kutoa maoni kwamba mkataba urekebishwe (kitu ambacho watanzania walio wengi ndio wanachotaka) tamko linataka huu mkataba uachwe kabisa, yani usiendelee hapa KANISA LIMEIBGILIA SERIKALI kutimiza wajibu wake maana wameipa amri serikali iachane mara moja na huu mkataba ikiwa serikali itauacha huu mkataba wa uwekezaji ni dhahiri kuwa ile kauli ya ALMARHUM SHEIKH ILUNGA HASSAN KAPUNGU rahimallahu kuwa nchi hii KANISA LINA NGUVU KULIKO SERIKALI na hapo ndipo MFUMO KRISTO UNADHIHIRI kwa kuonesha nchi hii inaendeshwa na KANISA
Cha pili: Tamko linataka Bandari tuiendeshe wenyewe, kimsingi na kwa spidi ya sasa kama watanzania bado hatuwezi kuendesha bandari na kufikia viwango hitajika
Cha Tatu: ukiangalia namba 4, tamko linasema “ tukiweka ubia na makampuni yenye ubobezi wa kiteknolojia kutoka sehemu mbalimbali duniani, na sio ubia kutoka nchi moja, tukiweka mikataba yenye tija”..
Hii inamaanisha bado tunahitaji uwekezaji.. sasa tamko linaposema sio uwekezaji wa nchi Moja, kwani Ticts ilikuwa ya nchi ngapi? Si walikuwa wachina pekee? , na tamko linaposema nchi mbali mbali duniani, Dubai(UAE) si ni mojawapo ya nchi zilizopo duniani kama ilivyokuwa China kuendesha Ticts kwa miaka 30?
Hili tamko nadhani lingesema vipengele vya mkataba viwekwe sawa.
Na linapokuja swala la ubobezi, Hata huko Europe na Marekani wanamtumia huyohuyo DP sasa sijui tamko linataka ubobezi gani?!
Kingine, tamko linaposema makampuni ya ndani binafsi ndo yaingie ubia na wawekezaji wa nje, tayari serikali imeshapoteza, wakati sekta kama hizi lazima serikali yenyewe iingie makubaliano na mwekezaji moja kwa moja ili kuwe na direct control, kuliko kupitia kwa kampuni binafsi
Mwisho bila kupepesa maneno, hili tamko halimtaki Mwarabu awekeze, ila kwa kusema “ kutoka sehemu mbali mbali duniani” ni dhahiri kwamba ingekuwa ni nchi ambayo haitoki ukanda wa mashariki ya kati kama Ulaya, basi hili tamko lisingetoka, kama ambavyo halikutoka kwenye mikataba mibovu ya madini, ununuzi wa ndege, na mikataka mingine mibovu. Nadhani baraza la MAASKOFU wanataka kutwambia kuwa itakuwa vizuri zaidi mwekezaji akitoka Vatican au Ulaya na iwe kampuni ya Wazungu Wakristo ila tu wamejificha nyuma ya kichaka wanachokijua wao,
Hapa kanisa limekumbuka kauli ya SAUTI YA WENGI NI SAUTI YA MUNGU ila wamesahau ya
Kaizari aachiwe kaizari na ya Mungu apewe Mungu
Hebu turudi nyuma kwenye historia Kanisa ndani ya nchi hii linapata wapi Moral authority wakati kanisa hilo haohao TEC na CCT walisaini mkataba na serikali 1992 wa kula mabilioni ya PESA maarufu kwa jina la MoU
Mkataba wenye masharti magumu tu kuwa kulipo na hospitali za kanisa serikali isijenge za kwake ipeleke wafanyakazi hapo na mishahara ya hizo hospitali za kanisa itoke serikalini hii ni hatari sana
Serikali imeanza kujenga hospitali zake kila wilaya hili kwao limekuwa tatizo kubwa sana
Hebu tujikumbushe machache kuhusu KANISA NA KADHIA MBALIMBALI ZA TANZANIA
Tutakwenda hivi kwa amri ya Maaskofu hadi lini?
Maaskofu hawaitaki historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika kwa kuwa inawaweka Waislam juu, historia hii ikafutwa.
Ushahidi upo.
Maaskofu hawakuitaka East African Muslim Welfare Society (EAMWS) matokeo yake ikapigwa marufuku kwa amri ya serikali mwaka wa 1968 kwa kuwa ilikuwa inajenga Chuo Kikuu cha Waislam.
Ushahidi upo.
Maaskofu hawakupenda kuona Waislam wanaelimika zikafanywa kila aina ya mbinu kuhakikisha kuwa watoto wa Waislam hawapati elimu ya sekondari wala Chuo Kikuu.
Ushahidi upo.
Maaskofu hawakutaka Organisation of Islamic Conference (OIC) ijenge Chuo Kikuu Tanzania katika miaka ya 1970 na kweli chuo hakikujengwa.
Chuo kikapelekwa kujengwa Mbale, Uganda.
Maaskofu wakakataa Zanzibar kujiunga na OIC na haikujiunga.
Ushahidi upo.
Maaskofu wamekataa kuzirejesha Mahakama za Kadhi zilizovunjwa mwaka wa 1963 na mahakama hakika hazikurejeshwa.
Ushahidi upo.
Yapo mengi lakini tutafakari haya kwa sasa.
Tanzania hii itaendeshwa kwa matakwa ya Maaskofu hadi lini?
JE NCHI HII BAADA YA KUSAINI MoU mwaka 1992 na makanisa ndio makanisa yamepata idhini ya kuiendesha Tanzania?
Na huu ndio MFUMO KRISTO UNAVYOENDESHA TANZANIA
WATANZANIA WENZANGU
Nawaasa tuiache serikali ifanye kazi yake ina vyombo vyake na wataaalamu wake tuliheshimu bunge na serikali katika kutekeleza miradi ya maendeleo kwa Watanzania
Sisi Watanzania WAZALENDO wenye nchi hii tunasema
Kazi iendeleeeeeeee
Sent from my SM-A045F using JamiiForums mobile app
Wahuni Tu haooHuu ugali wa Viongozi (BANDARI) Yeyote atakayejaribu kuusogelea lazima akumbane na mkono wa chuma ikiwemo kesi ya Uhaini na Mapinduzi ya Mdomo. Mods mpo hapa embu rekebisheni apo ni Baraza.View attachment 2720868
Ngoja sheikh Mwaipopo ajeWewe ni Lijingaa TEC yenyewe imesema hawana Shemasi katika Seminari hiyo.
Kuhusu hiyo Sheikh [emoji1787], masheik Huwa hawana Elimu ya Darasan, wengi wao ni wkaimbia Umande ambao walikataa shule Kwa sbabu hawana akili, wakabaki kukimbilia Elimu za madrasa, Alfuu beer, teee see jiiii .
Kwahivo, Kimantiki, Masheik ubwabwa hawana ufaham wa kuzungumzia Suala la DP.
Mimi sio Mkatoliki, ila Baraza la TEC wote ni wasomi kwelikweli , huwez kua Askofu huna shule kichwan!!.
SawaThat's JF forum problem.
Mimi sina muda wa kutuma ujumbe twice
Nitajie sheikh au maalim wa msikiti mwenye phd hapa tanzaniaWaliondila zero kabisa yaani eti wapewe wazawa then tuingie ubia hapa ndo utajua Phd za kupewa zipo kibao ili mradi umsujudie mzungu.
Utumbo mtupu kwa mweny akili timamu .
Point zao ni hizi👉 waendelee kupitisha mali zao ili kufanya biashara kwa mgongo wa kanisa .
Ukiona mtu anakubali lile bandiko mawili hajasoma au hakuelewa collacation baina ya vifungu ,maana wanaandika na katika madai yao hamna muunganiko .
Waanza kupinga uwekezaji ili wapewa wazawa then wanakuja kutaka ubia na watu wa nje😅😅hapa kuna phd au matope ya kukariri kingereza?
Waliambiwa PD world wanakuja kuwa kweny management au kutumia teknolojia katika uendeshaji je wanakataa lipi na wanakubali lipi?
Tukisema mtasema tuna udini ila kwa akili za kuzaliwa tu ukijua kusoma yale maazimio yao ni utopolo na hawajui kitu vichwa empty.
Pole sanaWaliondila zero kabisa yaani eti wapewe wazawa then tuingie ubia hapa ndo utajua Phd za kupewa zipo kibao ili mradi umsujudie mzungu.
Utumbo mtupu kwa mweny akili timamu .
Point zao ni hizi[emoji117] waendelee kupitisha mali zao ili kufanya biashara kwa mgongo wa kanisa .
Ukiona mtu anakubali lile bandiko mawili hajasoma au hakuelewa collacation baina ya vifungu ,maana wanaandika na katika madai yao hamna muunganiko .
Waanza kupinga uwekezaji ili wapewa wazawa then wanakuja kutaka ubia na watu wa nje[emoji28][emoji28]hapa kuna phd au matope ya kukariri kingereza?
Waliambiwa PD world wanakuja kuwa kweny management au kutumia teknolojia katika uendeshaji je wanakataa lipi na wanakubali lipi?
Tukisema mtasema tuna udini ila kwa akili za kuzaliwa tu ukijua kusoma yale maazimio yao ni utopolo na hawajui kitu vichwa empty.
Ukweli unauma wazee wa masters na phd za kupewa hata kung'amua mambo hamjui.Utakuta hata saba hukumaliza