Na kwa wale msiofahamu waraka huu utasomwa makanisa yote jumapili.
Hii pressure ni kubwa sana na mapadre wata comment kwa vijembe sana.

Lakini Maaskofu wangu nawauliza ,wakati jiwe akiwa anasagasaga demokrasia na kuibaka katiba mbona mlipiga superglue midomo yenu?Mhashamu Niwemugizi peke yake alisimama kumkemea.

Naamini hata huu mkataba angeuingia jiwe wala msingesema lolote.
Imekuwa hivi hata kipindi cha Kikwete nyaraka ni nyingi kupinga hili na lile(sio mbaya)lakini isiwe atawalapo Rais kutoka uislamu tu.
Tukemee uovu nyakati zote.
TUMSIFU YESU KRISTO
KRISTOOOOOO....
 
Hii ni first button from TEC, kaza shingo wabofye another button.

Tumsifu Yesu Kristo.......
 
..kama Maza anawapenda sana Dp World basi mshaurini awalete kama Ticts ya kina Karamagi.

..lakini mkataba unaotulazimsha mpaka tubadili sheria zetu, tena tulizoandika juzi tu 2017, unatia mashaka makubwa na haukubaliki.
Aiseee hao DPW sijui wamewapa nini. Mpaka katiba wanaweza badilisha kabisa.
 
Wqgalatia bana nikuulize kitu mkataba kati ya serikali na Barick kuchimba dhahabu miaka 100 wananchi walishirikishwa ? Hawa maskofu walitoa tamko wewe baada ya miaka 100 na maskofu wako mtakuwa hai?
Mkataba wa madini ulikuwa siri na huwezi kutengua baada ya kuingia ila huu wa bandari ndio wanaingia
 
Kanisa Moja Takatifu la Mitume 😀

Ngoja niisome maana mtangazaji Namba 2 nchini baada ya Kikeke Dr Kitenge amesema Fr Kitima amelichakachua Tamko 😂🔥
 
Jinyonge mkuu. Wamekosoa mkataba hawajokosoa uislamu.
TUKUMBUKE MWAKA 1992

Mwaka 1992, Serikali iliingia Mkataba na Makanisa kupitia Taasisi zao za TEC na CCT. Chini ya Makubaliano yale, hospitali za Makanisa zitatumika kwa wananchi wote pale ambapo Serikali haina hospitali.

Kwa kufanya hivyo, Serikali itakuwa na wajibu wa kuyapa Makanisa fedha za kuendesha hospitali hizo ingawa umiliki wa hospitali utabaki kuwa wa Makanisa.

Ifahamike kuwa fedha hizo zinatokana na kodI za Watanzania wote; Waislamu, Wakristo, Mabaniani, Magoha, Makadiani, na hata wale wasio na dini.

Nini athari za Mkataba huu ? Mkataba huu wa kibaguzi una athari nyingi. Kwanza:

Serikali inatumia kodi za wananchi kuyapa Makanisa kuendesha shughuli zake za kuimarisha Ukristo.

Tunasema hivyo kwa sababu utaratibu unaotumika ni kuwa Serikali inatoa fedha kwa Makanisa ambayo wao ndio wanapanga matumizi ya fedha zile na sio Serikali.

Pili, kwenye Jamii, Makanisa yanaonekana ndio yanatoa huduma za Jamii na hivyo kujenga saikolojia kwa wananchi kuwa Ukristo ndio unajali wananchi.

Athari ya tatu ni kuwa Makanisa yananyonya wananchi kwa sababu pamoja ya kuwa hospitali zile zinapata fedha kutoka Serikalini, bado wananchi wanalipia huduma.

Nne, Mkataba hauna ukomo, yaani ni wa milele. (Wakristo wataendelea kupewa hayo mabilioni na Waislamu watanyimwa milele).

Kwa tafsiri nyingine ni kuwa Serikali imejivua kwenye wajibu wa kutoa huduma za Jamii na kuchagua Makanisa kuwa ndio wakala wake.

Tunapenda kuwakumbusha Watanzania kuwa wakati Mkataba huo unasainiwa aliyesaini Mkataba ni Bwana Edward Lowassa aliyekuwa Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu. Huyu ni Mkristo

Kwa utaratibu wa Serikali, Lowassa alikuwa Waziri wa Nchi, hivyo basi Waziri mwenye dhamana ni yule mwenye ofisi yake kwa maana ni Waziri Mkuu.

Wakati unatiwa saini Mkataba, huo Waziri Mkuu alikuwa John Samwel Malecela ambaye ni Mkristo.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye ndie aliyeishauri Serikali isaini Mkataba ule ambao kwanza hauna ukomo (mkataba wa maisha) na pili unatumia kodi za wananchi kuimarisha Ukristo alikuwa Damian Lubuva ambaye ni Mkristo.

Kwa upande wa Kanisa mwanasheria wao alikuwa Prof Balozi Costa Mahalu, Mkristo.
Kwa maana hiyo, upande wa Serikali, Mkataba ule umeasisiwa na kusimamimwa na Wakristo watupu. Waziri wa Nchi Mkristo, Waziri Mkuu Mkristo, Mwanasheria Mkuu Mkristo.

Ni Wakristo! Wakristo! Wakristo!

Kama kwenye hoja ya makubaliano ya Bandari ni Wazanzibari wawili (ambao ni Waislamu) wamesaini makubaliano ya kuiuza Tanganyika, Mbona Waislamu hawakulalamika pale Wakristo 3 wazito Serikalini walipobuni mbinu za kutumia kodi za wananchi kuimarisha dini yao Ukristo Tanzania?

Kama hoja ni ukomo wa mkataba, mbona Mkataba huu wa Serikali na Makanisa hauna ukomo? Ni mkataba wa milele na ndio maana mpaka leo (miaka 30 sasa) bado unaendelea kutumika.

Bado Serikali inaendelea kutekeleza Mkataba wa kibaguzi ambapo inatumia kodi za wananchi wote kuimarisha shughuli za Kanisa.

USHAHIDI

Tarehe 23 Januari 2019, Rais Magufuli alikutana na viongozi wa dini zote IKULU. Kwenye Mkutano ule Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana ambaye pia ni Askofu wa Dayosisi ya Tanga Bwana Maimo Mndolwa alilalamika kwa Rais Magufuli kuwa Serikali inavunja Mkataba kwa kujenga hospitali kwenye maeneo ambayo Kanisa imeachiwa kuwa na hosptali ambazo zinapewa fedha na Serikali.
Amelalamika hivyo kwa sababu Mkataba wa Makanisa na Serikali hauna ukomo. Kila penye hospitali ya Kanisa, Serikali haikutakiwa kujenga hospitali yake. Badala yake, Serikali inatakiwa kuendelea kutoa fedha za kodi kuwapa Makanisa ili ziendeshe hospitali zao na kuimarisha Ukristo kwa kutumia jasho la Watanzania.

Katika kusisitiza madai yake, Askofu Mkuu alitoa ushahidi wa hospitali zilizojengwa na Serikali katika Wilaya ya Ifakara, Ngara na Muheza ambazo kwa mujibu wa Mkataba wa 1993, Serikali haikutakiwa kujenga hospitali hizo za Wilaya.

Kitendo cha Serikali kujenga hospitali hizo kinatafsiriwa na Kanisa kuwa Serikali imevunja Mkataba kwa sababu sasa inatoa huduma hiyo muhumu kwa wananchi.

Askofu Mkuu alifafanua kua matatizo haya yapo kwenye ngazi ya Wilaya kwa sababu kwenye ngazi za juu, hakuna tatizo kwa kuwa kuna Msimamizi anaesimamia Mkataba huo.

Hapa Askofu Mkuu alikuwa ana maana kuwa hospitali za KCMC ya Moshi, Bugando ya Mwanza na CCBRT ya Dar es Salaam ambazo zote ni mali ya Kanisa bado zinaendelea kupata fedha za kodi huku zikiendelea kuwalipisha wananchi kwa huduma wanazopewa kwenye hospitali hizo.

Rais Samia Suluhu Hassan alifanya Mkutano na Baraza la Maaskofu la Kanisa Katoliki Tanzania uliofanyika Kurasini tarehe 25 Juni 2021. Katika risala yao, Baraza la Maaskofu limeilaumu Serikali kwa kujenga hospitali zake kinyume cha Mkataba wa 1992, na Makanisa.

Kwenye risala hiyo, Baraza la Maaskofu limeshangaa kuona Serikali inajenga hospitali kwenye Wilaya ambazo Makanisa tayari yana hospitali zao. Wamehoji kwa nini kuwepo na ushindani wa kutoa huduma hizo?

Kwa maana nyepesi, kwa nini Makanisa yasiachiwe kuendesha hospitali maisha (milele) na kuendelea kupewa ruzuku zinazotokana na kodi za wananchi?

Risala hiyo ni ya chombo cha juu kabisa katika Kanisa Katoliki ambao leo viongozi hao hao wanaohoji na kulalamika kuhusu makubaliano ya Serikali na DP World kuwa hayana ukomo!

Kanisa hilo hilo ambalo linapiga kelele kuhusu mkataba wa Serikali na DP World, ndilo ambalo kiongozi wake Askofu Method Kilaini alipewa shs. 80.9 milioni, Askofu Eusebius Nzigirwa alipewa shs. 40.4 milioni na Mchungaji Alphonce Twimanye Simon alipewa shs 40.4 milioni fedha za Rushwa zilizotokana na kashfa ya akaunti ya Tegeta ESCROW.

Hadi leo Kanisa halijatangaza hadharani hatua za kinidhamu iliyowachukulia viongozi hao. Ukimya huu tuutafsiri vipi? Kwa ukimya huu, Kanisa linapata wapi “moral authority” ya kupinga mkataba wa DP World.
🍉🍉🍉🍉🍉🍉🍉
 
Hawa jamaa nilikuwa nawachukulia poa.

Ila majuzi nikashuhudia padri mmoja anatoa neno halafu anasema na vifungu kutoka kwenye Qur'an tena Kwa Kiarabu kama wale mashekh.

Ikabidi nianze kuwatafakari upya hawa Jamaa.
 
Catholic wanaongoza dunia.
 
Nchi yetu inaendeshwa kwa utawala wa sheria na serikali yetu ni ya kidemokrasia inayotokana na watu wenyewe kwa mujibu wa Katiba yetu.

Nchi Ina mihimili 3 ya serikali, bunge (wananchi) na mahakama. Kati ya mihimili hii 3 wananchi bila kujali umri, jinsia na dini zao wanawakilishwa na wabunge wao wa majimbo katika kufanya maamuzi kuhusu wao.

Baraza la Maaskofu limesika likitoa matamko na maazimio kuhusu uwwkezaji kwenye bandari, Huku likisema wananchi wengi hawaupendi mkataba wa ubinafsishaji wa bandari. Hao wananchi ni akina nani, wako wangapi na wamekutana wapi kuwauliza maoni Yao? Nchi Haina dini, tukutane kwenye kampeni za uchaguzi na kisanduku chakula kama Kuna mwenye njia/sera mbala ya namna ya kuindesha nchi badala ya kikundi Cha watu kutaka kuwasemea wananchi wote nchini kitapeli.

Jambo lolote na hoja yoyote haiwi na nia njema kama ikichanga maneno kama Tanganyika, Zanzibar, watanganyika, wazanzibar, waisilamu, wakristo, wazayuni, Wazungu, au Waarabu. Maneno haya ni hatari sana kusikika majumbani, mtaani, kazini na kwenye taasisi mbalimbali. Ukiyasikia yaepuke na yazimwe kwa gharama yoyote ile ili yasiote, kumea na kuzaa mbegu.

Tutailinda Katiba
 
Muulize Kabila kitu Maaskofu wa Katolik walinfanyia kule Congo, au Muulize Mugabe alivyo kuwa anapelekwa mputa na hao katolik, usiche na hao watu
 
WARAKA WA MAASKOFU SIO ITHIBATI ZA MAONI YA WATANZANIA.

Na Thadei Ole Mushi

Niseme kwa kifupi sana kuhusu ujumbe wa baraza la Maaskofu kuhusu Bandari. Kwanza nisema wazi kuwa nawaheshimu sana vingozi wangu hawa wa Dini. Cha pili nisema tamko lao naliheshimu kwa kuwa wametumia haki yao ya kikatiba kutoa Maoni. Cha tatu niseme ni TEC ni moja ya vyombo imara sana kijamii hivyo wanatakiwa kila kitu wanachokisema hawaangalia zaidi maslah ya taifa.

Niwakumbushe vitu viwili kabla ya kuendelea. Cha kwanza ni kisa cha kuuwawa kwa mtu anayeitwa Galileo Galilei 1633. Nafahamu kisa hiki mnakijua, kwa manufaa ya wote ni kwamba Galileo kama mwanasayansi aligundua nadharia ya “Copernican” kwamba alithibitisha kisayansi kuwa “Dunia ndio huzunguka jua” nadharia hii ilienda kinyume kabisa na mafundisho ya kanisa kuwa “Jua ndio lililokua linaizunguka Dunia”. Kwenda huko kinyume na mafundisho ya Kanisa alitiwa hatiani na kuteswa vikali hadi kufa. Maandiko ya Roma yameandika kuwa alihojiwa vikali “Italo Mereu” wataalamu wa lugha wanasema Italo Mereu ni mateso makali hadi kufa.

Kwenye hili kanisa lilikuwa limefanya Makosa pasipokutafiti na kujiridhisha.

Kisa cha pili ni tukio la 1992 la Jaji Fransis Nyalali alipowasilisha ripoti ya Tume kuhusu mapendekezo ya watanzania ya uanzishwaji wa vyama vingi vya Siasa. Asilimia 80 walikuwa hawataki vyama vingi vya Siasa, ni Asilimia 20 tu waliyotaka vyama vingi vya siasa. Asilimia ndogo ilishinda na kuanzishwa vyama vingi vya Siasa.

Hoja yangu.

Kwenye waraka wa Maaskofa wamesimamia misingi mikubwa miwili kujenga hoja zao. Moja ni kwa nini taifa Moja la Kiarabu kupewa kandarasi yote, na hoja ya pili ni kwamba kwa vipimo vyao wenyewe wanadai watanzania wangi wanalalamika kuhusu huo mkataba. Maelezo mengine yalijazilizia nyama tu kwenye hoja hizi mbili.

Kwa kutumia kisa cha Galileo hapo hapo juu Baraza la Maaskofu halijapewa athibati (certification) kwamba mawazo yao na mitazamo yao itakuwa sahihi kwa asilimia 100. Lakini kuna hoja inajengwa hapa kuwa watanzania wengi sijui wametumia kipimo gani kupata hao wengi lakini hata kama ni wengi kuna hoja za Msingi zimeelezwa kila kukicha faida ya kuwekeza pale Bandarini. Watu wachache waliona vyama vingi vya siasa vina tija wakavipitisha.!!!

Ok

Maaskofu wanasema walitaka wazawa zaidi kuwekeza pale bandarini. Ni jambo jema sana…. Dunia ya Sasa rasilimali zake huwezi kuzifaidi mwenyewe. Hata kwa mataifa yaliyoelendea wanafika mahali wanabidi waite wawekezaji. Hakuna Nchi Duniani haina wawekezaji toka kwenye mipaka ya nchi zao.

Dunia inahama kwa haraka sana hasa mataifa yanayoendelea. Sera kubwa ni kuwekeza kwenye Teknolojia na ku Negleti raw materials za Africa. Kwa leo unaweza ukawa na Pamba usipate pa kuiuza, Kahawa ukakosa, tumbaku ukakosa nk. Lakina wao toleo jipya la I Phone tu watu wanapangana madukani kununua kwa bei wanayotaka wao. Hata haya Madini, Wanyama pori, Bandari nk watafika mahali wata-Neglet ni busara sana kuzitumia kipindi hiki maana muda unakuja itabaki historia.

Bado mifumo ya Dunia inatulazimisha kuwekeza, Kenya na Tanzania zikipigana uchumi wa Dunia hautaathirika lakini Urusi na Ukreni athari zake tunaziona.

Leo mmerekani ameamua kubana dola yake kila mtu anahangaika, akizidi kubana tutauziana nyanya moja elfu moja. Katika mazingira kama hayo unatokaje kwenye huo mnyonyoro?

Tatizo la Tanzania hatupendi fact ndio maana Prof Mhongo alivyosema hakuna mtanzania wa kuwekeza kwenye Gas na Mafuta tulimshangaa.

Nafikiri.

1. Baraza la Maaskofu lingeona kwanza dhamira njema iliyopo kwa Rais kwenye kuwekeza pale Bandarini bila kuangalia ni taifa gani limepewa hiyo Kandarasi.

2. Baraza la Maaskofu lingeona ufisadi, Urasimu, na wizi uliopo pale Bandarini washauri kwa umakini zaidi.

3. Baraza la Maakofu lisifikiri kuwa ni Tanzania tu ina Bandari. Majirani zetu wanazo na hii ni vita ya kukamata Soko la nchi za Congo, Malawi, Zambia, Uganda, Rwanda na Burundi.

4. Nchi tajwa hapo juu ambazo hazina Bandari mizigo yao kwa Mwaka ni tani milioni 60 kwa pamoja. Bandari ya Daresalam Mwaka jana na Juzi ni tani milioni 8 tu ilipitishwa. Jambo la Msingi la kujiuliza tani 58 milioni zilipitishiwa wapi? Tusifikiri ni sasa wenyewe tuna bandari.

5. Baraza la Maaskofu limerudia kosa lile lile la baadhi ya watu wa kawaida. Kutaja Dubai kama nchi pakee iliyopewa Bandari sijui wana nia gani ndani ila wamerudia pale pale kitu ambacho kinatoa Mwanya kwa ndugu zetu waislamu wanawaza kuja na waraka wao na ndio wataligawa taifa kabisa.

6. Kama waraka huu utaenda makanisani kama ulivyo ni waumini kulishwa Propaganda na Interest za watu wachache. Nafikiri ni Busara kujikita kwenye vifungu vilivyokosewa zaidi na kushauri virekebeshweje.

Anyway…

Baraza la maaskofu lingeweza kujikita kwenye vifungu vinavyoonekana vina kasoro kuliko kubeba makando kando mengine yanayoharibu ujumbe na nia njema ndani yake. Tujitahidi kuliunganisha Taifa

C&P from👇
Ole Mushi
0712702602
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…