Nahisi Ndugu Ndugai Bado anapwaya sana katika nafasi yake ya uspika, ni mwaka wa tatu sasa hatujaona hata meno ya Bunge kuiwajibisha serikali katika masuala nyeti na Muhimu,
Nakumbuka kipindi cha jamaa Kikwete Bunge limewajibisha serikali Mara kibao sana na nashangaa mpaka Leo tuna mengi ya kuhoji lakin Bunge linaiogopa serikali,
Kuna masuala nyeti sana lakin Bunge Lipo kimya,
Naona viatu vya Makonda vinampwaya ndugai,
Hata wakati wa mwalimu Nyerere ambaye tunaamini ndo alikuwa mkali na ndo alikuwa rais kweli, lakin Bunge lilihoji na kuisimamia serikali ipasavyo mpaka saa nyingine kuikataa miswada na Nyerere ku surrender
Kipindi hicho Adam Sapi Mkwawa akiwa spika bunge lake lilikataa muswada wa Rais na kuurudisha na Rais akabwaga manyanga. Tena siyo hawa marais wa kuja bali ni Rais anayeheshimiwa hata miaka 200 ijayo yaani Rais Julius Nyerere. Je, ilikuwaje? Ilikuwa hivi.
Mwaka 1969 Waziri wa Elimu, Solomon Eliufoo aliugua na ikaonekana anaweza asiendelee kuwepo serikalini. Serikali kwa ku-panic ikapeleka muswada bungeni unaohusiana na mafao au maslahi ya mawaziri hasa wanaougua.
Muswada huo ulileta mgawanyiko bungeni ukizingatia kwamba ni miaka miwili tu tangu siasa ya Ujamaa na Kujitegemea itangazwe pia miiko ya uongozi.
Bunge likaukataa muswada ule likamrudishia Rais Nyerere ili ikiibidi afanye lolote na kama ni kuurudisha tena basi na iwe ili hatimaye wavunje bunge na nchi irudi kwenye uchaguzi.
Rais Nyerere mwenyewe alipohojiwa na waandishi alinywea na kusema "the parliament had a point" yaani bunge lilikuwa na hoja na hakuthubutu kuupeleka tena bungeni.
Haya, niambieni ni bunge lipi tena lililowahi kufauluujasiri kama huu. Wote waliobaki na mnaowataja wafyata mkia watupu, tena kukiwa na hatauwezekano wa kuhama vyama.
Leo hii Viatu vya Makinda ni vikubwa mno kwa ndugai