Martin George
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,695
- 1,470
Kwenye nyumba za ibada hakuna kuulizana maswali na huku kanisani ukiwa ni mtu wa kuhojihoji unaweza kutengwa. Kwenye mambo ya kiimani ni utaratibu mzuri na tunaukubali kwani nyumba za ibada ziko nyingi ukishindwa kwa Kakobe utaenda kwa mzee wa upako. Sasa ni kama vile bunge ambalo ni la kimwili zaidi linatamani kuiga utaratibu huu wa ' mchungaji kutohojiwa' na kwamba wale wenye kiherehere watatengwa hadi mwisho wa uhai wa bunge. Sidhani kama ni jambo jema sana kwani kazi ya mbunge ni kusema sasa kwanini asiseme?!!! Na kama ni kumtenga kwani mbunge anachaguliwa na bunge au ' ANAPELEKWA' bungeni na kura za wananchi. Nyumba za ibada zina wenyewe anaweza kuwa Yesu, Mtume nk lakini bunge ni la wananchi. Unapomtenga mbunge X humuathiri yeye bali wananchi waliomtuma bungeni, ahsante!!