Katika nchi inayofuata utawala wa kisheria wa kikwelikweli, huyu Ndugai wakati huu alipaswa kuwa jela na siyo kukalia kiti cha Spika!

Kwani watanzania mmesahau kuwa ni huyo huyo Ndugai ambaye alimchapa bakora mgombea mwezie wa CCM wakati wa kura za maoni mwaka 2015 kule Kongwa hadi akazirai?

Lakini Polisi 'walimgwaya' Ndugai na wala hawakumkamata katika kosa hilo la jinai!

Huo ni ushahidi tosha kuwa sheria za makosa ya jinai za Tanzania zina 'macho' na kuangalia nani aliyefanya kosa hilo.....

Tukirejea tukio la leo Ndugai amethibitisha kuwa hafai kabisa kuwa Spika wa Bunge letu kwa kuonyesha upendeleo wa dhahiri kwa wabunge wenzie wa CCM.

Mbunge mmoja mwanamama aliwasha Mic na kusikika wazi wazi akimuita Mnyika mwizi, cha kushangaza kupita kiasi badala ya Spika Ndugai kumchukulia hatua Mbunge huyo 'mshari' wa CCM badala yake Ndugai akaagiza askari wa Bunge wamtoe msobe msobe Mheshimiwa Mnyika utadhani ni kibaka!
 
Kama Ndugai alishindwa kuwa mvumilivu kwenye kikao cha uchaguzi wa CCM mpaka akamtandika mpinzani wake kwa rungu kichwani hadi kuzimia inamaana hiyo nyongo yake inahitaji msaada wa kisaikolojia.
Ajifunze kwa mwenyekiti Zungu
 
Humu kuna watu mambo yakienda kama watakavyo utasikia bora spika kuliko maadam spika Leo wamegeuka kisa kakataa upuzi wao na bado wataisoma namba
 
Na
Humu kuna watu mambo yakienda kama watakavyo utasikia bora spika kuliko maadam spika Leo wamegeuka kisa kakataa upuzi wao na bado wataisoma namba
Upuuzi gani unaoongelea?

Kwa hiyo kwako wewe unaona kwa Mbunge wa CCM kumwita Mnyika mwizi ni sahihi, ila wakati ule Halima Mdee alipomuita huyo huyo Ndugai fa....laaa aling'ang'aniwa utadhani kaua mtu!

Kwa system ya Ndugai anayoendelea nayo ya kuwapendelea waziwazi wabunge wenzake wa CCM kwa kuwaacha wawatukane na kuwakashifu wabunge wa upinzani bila kuwachukulia hatua yoyote, naziona dalili za wazi kabisa kuwa siku chache zijazo wabunge wa upinzani nao wataona 'uvumilivu umetosha' na wataamua kuzichapa kavu kavu na wabunge wenzao wa CCM......

Hapo ndipo tutakapoona ni nani 'wakali' wa masumbwi kati ya wabunge wa CCM na wale wa Ukawa......
 
Nyie mna matatizo kweli si mlisema bora ndugai kuliko huyo tulia ackson
Mkuu unapokuwa na shetani wawili. Ukisema mmoja ni bora kuliko mwingine, yule uliyesema ni bora habadiliki kuwa malaika. Anabaki kuwa shetani tu. Ndugai na Tulia wote hawafai kuongoza bunge, lakini kuna afadhali kidogo kwa Ndugai kuliko Tulia.
 
Ndugai ni spika wa hovyo ambae hajawahi kutokea katika historia ya bunge tokea lilipoundwa nadhan ni vema sheria zinazoongoza bunge zingebadilishwa ili tuweze kuwa na maspika kama Pandu Amiri Kificho kwani huyu ni mtu sahihi kabisa kwa kuongoza mhimili kama wa bunge.
 
Huyu jamaa spika wa Jamhuri ya Tanzania inaonyesha alichapwa sana bakora alipokuwa mtoto,Ningependa kuwaasa Watanzania tuache kuwapa adhabu za kuwapiga bakora watoto wetu,matokeo yake ndio hayo
 
Kuna migogoro mingine unaweza kujitengenezea au kuiepuka kwa kutumia diplomacy ways, kutumia nguvu kuzima mambo kuna faida na hasara, ila hasara ni nyingi, kwani watu watajua, na wakijua watadadusi na wakipata kitu tofauti unaweza kuaibika
 
Bavicha sijui mnakula nini.Ni mwezi uliopita tu mlimsifia spika kuwa amejitambua kwa sasa yupo vizuri na sifa chungu nzima
Kama alisifiwa kwa kufanya vizuri ni sawa na ni haki yake apate hizo sifa. Lakini hiyo haizuii kukosolewa anapofanya vibaya. Hata Lukuvi amesifiwa na Mbowe na Mdee kwa sababu anafanya vizuri kama waziri kwenye wizara yake. Sasa kama ataboronga lazima akosolewe tu. Hili ni jambo la kawaida tu mkuu.
 
Ni Pimbi na Ndezi hawana tofauti wote waguguna mihogo!
Kwani umemsikia mhere mwita akiwalinganisha spika na naibu wake? Kwani kama walimsema yeye ni afadhali kuliko naibu wake inamanisha yeye hana upungufu. Yaani sijui elimu yenu ndiyo ndogo kwa kifupi ni kwamba kama walisema spika ana unafuu halafu wakataja madhaifu yake haya na kwa vile hawajasema kuwa kwasasa naibu ni bora kuliko spika basi naibu anabaki kuwa Bomu la nyuklia wakati spika akiwa la kurusha kwa grunedi kwa mtazamo wa mhere
 
5)-Anaongozwa na Mhemko, Hana Busara wala Hekima kwa Suala la Mnyika hajatumia Busara wala Hekima Mropokaji.
Naomba nikiri wazi kuwa huyu jamaa busara, hekima na akili zake zimeharibiwa na viwavi. Inawezekana utotoni alikula sana viwavi jeshi ndiyo maana hana akili hata kidogo!! Bahati yake yule jamaa akiyetaka kuuliwa kwenye kampeni alitulizwa kwa ukuu wa wilaya, vinginevyo tungekuwa tumemzika!! Alivyopelekwa India kipindi kile nusura arudi kwenye buti ya ndege!!
 
Chongo na kipofu (lugha ya kimaandiko) wote ni walemavu! usijaribu kufananisha kipepeo na nondo mkuu!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…