Rais Samia apandishwa Basi huko London kwenye Msiba wa Malkia Elizabeth II
Tungemuona na mfalme wa Japan na Biden mle ndani isingekuwa maneno.Wametuvunjia heshima sana maraisi wetu waafrika kuwabeba namna ile.Eti raisi Mnangagwa ndiye aliyejitolea kuwa dereva.
Huu uzi nimecheka hatariii
 
Nasikia hakuna hata kiongozi mmoja kutoka ulaya aliyepandishwa basi kwenye msiba wa Rais Mandela kwani hawakuziona hizo foleni au usalama,,,hawa watu dawa yao nikutowashobokea nakukomaa tujenge nchi zetu,,,wanatudharau kwakua tunawategemea!
Magufuli aliliona ilo ndiyo maana akakomaa nyumbani kujenga nchi kama Viongozi wa Asia mfano Singapore, Indonesia, Vietnam, huwezi kuwaona wakizurura kwa wazungu hovyo.
 
Aibu!

Huko London kwenye msiba wa Queen Elizabeth II, Rais Samia wa Tanzania ni mmoja wa Viongozi waliopandishwa kwenye basi.

Nb: Kuna kila dalili Rais wa bongo alikuwa ana mind mpiga picha 😄.

View attachment 2361396
Mimi nina mashaka na ubaguzi hapa kwa sababu sijaona sura ya "Mdhungu" hata mmoja waliopanda pamoja kwenye hii bus, waafrika kwao Wadhungu kwao., au tuseme yawzekana waafrika wana mashaka nao na korona?
 
Tusichukulie poa kwa sababu Samia ni Rais kama Biden watakuwa na hadhi sawa.Kubali kataa ndo maana walioingia na magari yao ni Biden na PM wa Israel
Kwahiyo Samia ni Kinyamkera tu mbele ya Biden?

Mbona akiwa Tanganyika anatembea na msururu wa VIEITE mia tano?
 
Wakati watu kama akina magufuli wanapambana kutahiri fikra zetu, mbuzi kadhaa wakawa wanambeza, mbaya zaidi wengine wanatunzwa na hawa hawa wanaotudharau.

Anyaway as long as wote wamewekwa ktk bus, nadhani watakuwa wametumia wasaa huo kutafakari kwa pamoja juu ya namna wanavyochukuliwa na hao watu.
Msiba wa Nyerere ulikuwepo?
 
Kila kiongozi angekuwa na msafara wake, shughuli ingeisha wiki mbili zijazo. Inampunguzia nini. Amemaliza kazi aliyoiendea vizuri na kuiwakilisha nchi. I think there is no harm for our President to share transport with other African colleagues to ease the logistical challenges during the farewell to her Majesty, Queen Elizabeth
 
Sasa kama Rais ndani ya basi je wale wapambe si wamebakia hotelini, protokali zote kwishnei...

Kweli Tanzania nchi ndogo sana, maana ningefarijika kama marais wa Ufaransa, Ujerumani US, Canada nao ningewaonamo humo.
Fanya makubwa kwako. Usidai hadhi usiyostahili ugenini. Kuaga msiba kaaga vizuri, cha mno nini?
 
ndomana ata yule mzungu wa simba sio mzungu tena amekuwa mzunguko
 
Kila kiongozi angekuwa na msafara wake, shughuli ingeisha wiki mbili zijazo. Inampunguzia nini. Amemaliza kazi aliyoiendea vizuri na kuiwakilisha nchi. I think there is no harm for our President to share transport with other African colleagues to ease the logistical challenges during the farewell to her Majesty, Queen Elizabeth
Hivi kwenye kikao cha UN general Assembly huwa wanapanda mabasi? Kwanini U.K wasingefanya jinsi ile ile? Well kama ingekuwa hakuna ubaguzi wala si tatizo, tatizo linakuja pale ambapo wengine wanawekwa pamoja wengine wanapewa presidential/head of states treat...Inamaana tunakubaliana kwamba wapo wkaubwa zaidi ya wengine humu duniani. Kama ndivyo uhuru tulionao na sovereignty inamaana gani?
 
Tumetukanwa, tumedhihakiwa, tumechoreka na tumedharauliwa maradufu ya walivyotudharau walipokuwa Wakoloni wetu.

Hakuna comment iliyoniuma GENTAMYCINE kama hii isenayo "....Nyani njiani Kutalii Jiji la London ili Wakastaarabike wakirejea Makwao Maporini..... "

Na kuna Mwingine 'Kazumu' Bichwa la 'Hustler' na 'Chogo' chemba lake kisha akasema Nyani akitafakari jinsi atakavyoidaka Ndizi yake.

Na kuna Rais mwingine sijamwona na kumtambua vyema ila amekaa kama dirishani mkono kauweka Usoni huyu kuna Mzungu Mmoja 'Kakomenti' kuwa Nyani akiona Aibu kupigwa Picha.

Kifupi huko Mitandaoni kwa Wazungu leo Neno la Nyani limetumika na kupata Mashiko mno na natamani sana nami niwajibu kwa Hasira, ila tatizo sijui Kiingereza hivyo nawaombeni mnaokijua nanyi muwafuate huko mkawajibu Wasomi wenzenu.

Mkiambiwa siyo kila Tukio muwe na Kiherehere nalo Kwenda Kulihudhuria muwe mnatuelewa matokeo yake mmezikimbia Nchi zenu kwa Malalamiko ya Wananchi wenu juu ya Hali Ngumu ya Maisha na kwenda Kupumzisha Akili London matokeo yake Mmesanifiwa kwa kupakiwa pamoja kama Ndizi za Mgeta Morogoro na Kutudhalilisha hadi Wenye Akili Kubwa mliotuacha huku Barani Afrika.
Weka screen shots itapendeza zaidi ila ukweli ni kwamba kwa Sasa viongozi wote wa Afrika ni puppets wa wazungu na wanadharaulika sana hivyo sio ajabu kujipeleka London huku wakiwa hawana umuhimu wowote huko.
 
Respect is earned my friends, hapo U.k imetupa nafasi ya kujitafakari kama dunia kwamba; wao bado ndiyo wafalme wa dunia hii na serikali yao ni USA na Isarel pengine...What a message to the world!

Watu wa dunia waliotendewa haya ni jukumu lao kusema ndiyo au kusema hapana na kukataa hii treat kama Rusia alivyojionyesha kwamba anataka kuleta balance of power na kuondoa mambo ya fulani kuwa ndiyo final and conlusive...Hata ukoloni enzi hizo kuna watu walikuwa wana justifications, kila kitu kina justification mpaka pale yule anayetendewa anapong'amua kama its not right na ku contend. Otherwise, hao royals bado wnaa hizo perception wao ni royal kwa dunia na siyo kwao tu na ndiyo sababu hakuna aliye object...Sasa je kama huyo malkia mwenyewe anhefanyiwa hivyo yeye na watu wake wangekubali? If not then its obvious perception yao ni kuwa they deserve higher status compared to the rest of the world. Hakuna discussion hapo
 
Siyo wazungu wote Wana mawazo hayo usilete chuki zisizo na msingi nisawa na hapa Bongo kuna baadhi ya watu wa ovyo Wana mtukana na kuwabagua wazungu mf ni Dejan wa Simba
mti wa mbuyu ni mbuyu tu, hata kama siku utatoa majani ya mpapai usisahau kuwa ni mbuyu.

FATA MZIZI.
 
Magufuli aliliona ilo ndiyo maana akakomaa nyumbani kujenga nchi kama Viongozi wa Asia mfano Singapore, Indonesia, Vietnam, huwezi kuwaona wakizurura kwa wazungu hovyo.
Na alipo maanisha kweli dunia ilikubali ku bow kwake, ndiyo sababu yule mzito wa Barrick alipanda ndege kuja negotiate naye nchini kwake na siyo yeye kwenda huko...Hata kama hajadumu lakini alithibitisha kitu kwa dunia kwamba nchi lazima iheshimiwe!
 
Umeamua tu kuwatukana hawa viongozi wa hili bara.

Hata viongozi wa nje kama PM wa Canada, kiongozi wa Ujerumani, PM wa Bangladesh na viongozi wengine maarufu walipanda pia 'Bus'.
 
Genta... sasa kama beberu kaamua kukubagua hilo linakuchefua nini ili mradi anakugea peremende kwenye bakuli lako angalau upooze njaa?
 
Umeamua tu kuwatukana hawa viongozi wa hili bara.

Hata viongozi wa nje kama PM wa Canada, kiongozi wa Ujerumani, PM wa Bangladesh na viongozi wengine maarufu walipanda pia 'Bus'.
Huna Akili.
 
Back
Top Bottom