Rais Samia apandishwa Basi huko London kwenye Msiba wa Malkia Elizabeth II
Afrika bhn Sasa Kila rais angepewa usafir Wake binafsi ingekuwa fujo na kazi zisingefanyika maana idadi ya polisi haitoshi wamechuka sehemu tofauti Ila nimependa
Unajua walichofanya ni Ku limit idadi ya watu kwenye tukio, Kila Rais akija na ufalme wake si chini ya watu 20! Ingekuwa vurugu kama ulivyosema, na Mapompus ya watu weusi kama unavyojua tena, Lakini wameeliminate wapambe wote.
Nafikiri hata hapa Bongo tumeshawahi kufanya kuna wakati wa uapisho au msiba walipandishwa kwenye basi marais wote.
 
Nyie mlitaka misafara kwa viongozi wote ehh

Ova
 
Uzuri wa Magufuli ulikua ni sehemu kama hii, asingependa!

Anyway Rest In Peace malkia.

Wito tuendelee kuongeza juhudi kupambana na umasikini, umasikini unatweza utu, heshima, wadhifa na haki pia, hii ni kwa mtu moja moja,taifa na hata bara kwa ujumla wake.
 
Wazungu wanatoa somo kwa viongozi wa afrika kuwa wasipende kutembelea v8 maana yanafilisi nchi.waingereza wao wamebana matumizi wakawapakiza kwenye basi, lakini naamini ingekuwa kwetu zingenunuliwa v8 hata kwa mkopo.safi sana uk mmewapa somo namna ya kutumia fedha za umma na wakirudi wanaweza kubadilika na wasipobadilika basi wananchi tutawalazimisha wabadilike.
 
Kama kuna anayehitaji mfano wa umasikini (wa kifedha na kifikra) tulio nao, huu uzi ni case study nzuri. Progressive thinker ataona uhalisia wa foleni na changamoto za logistics, ataona mwelekeo wa kidunia kuhusu utunzwaji wa mazingira na pengine kuhoji ndege binafsi zilizotumika kuhudhuria shughuli za maziko. Wenzangu na Mimi tutaona tumedharauliwa kwa umasikini au pengine weusi wetu.

Wakati huo shughuli yenyewe ikiwa ni pamoja na misafara ya viongozi wetu imelipiwa japo kwa kiasi fulani na mlipa kodi wao ambaye kwake leo amepata nafasi ya siku ya ziada ya kupumzika nyumbani kabla hajarudi kwenye kazi ya kima cha chini.
 
Unajua walichofanya ni Ku limit idadi ya watu kwenye tukio, Kila Rais akija na ufalme wake si chini ya watu 20! Ingekuwa vurugu kama ulivyosema, na Mapompus ya watu weusi kama unavyojua tena, Lakini wameeliminate wapambe wote.
Nafikiri hata hapa Bongo tumeshawahi kufanya kuna wakati wa uapisho au msiba walipandishwa kwenye basi marais wote.
Tatizo afrika tunataka kutukuzwa mpaka ugenini yaani wanavyokwamisha mambo huku afrika wanataka kwenda kukwamisha mpaka ugenini tujifunze kwenye hili
 
Back
Top Bottom