Uchaguzi 2020 Ahadi na Sera za Tundu Lissu katika Uchaguzi Mkuu 2020
Akifuta hizo elfu saba saba zenu, pesa wanazolipwa wasiojulikana, wasanii, bilioni 1.2 anayojilipa kila mwezi kufanyia starehe tu na mengineyo mengi ya hovyo, pesa itapatikana kwa wingi.
Nina wasiwasi, kama hunyonyeshi basi siku zako za kujifungua ziko karibu, au una mimba changa umeanza kutematema mate na kujitapikia?
 
2015 Magufuli hakuwa anafafanua chochote zaidi ya kupiga pushup na kusema, serikali ya Magufuli itakuwa ya hapa kazi tu. Kisha akawa anakazia akiwa rais kuna watu watalimia meno. Lisu weka mashambulizi hapo ccm wanaanza kupaki basi. Ufafanuzi utauona akiwa ikulu fullstop.
Elimu bure
Mil 50 kila kijiji
Kufufua shirika La ndege
Tanzania ya viwanda
 
Kamwaga sera nzuri bt kinachomponza ni ule unafiki wake kwenye sakata la madini, mtu aliekua akipiga kelele tunaibiwa madini then akaja kuwatetea wezi hao hao, huyo ukimpa nchi si atauza kila kitu alale mbele.
 
Ila kitu ambacho Chadema wanatakiwa wakishugulikie haraka Lissu asichelewe kuongea maana muda una kua mdogo na mambo mengi mkutano mwingine aanze kuongea saa 9 ikiwezekana kama atakua na pumzi akichoka apewe wa kumsaidia.
Hawezi kuchoka

Sent from my SM-J250F using JamiiForums mobile app
 
Kwa Hiyo uchumi Wa Uganda ni Mkubwa zaidi ya Tanzania kwa Mifumo ya Kodi kuliko Tanzania Acheni Kudeka hakuna Maendeleo yasio ma maumivu ndani yakoo yaani hata ka CHADEMA wachukue nchi msituamishe kila kitu kitakwenda kama mteremkooo kwanza kujielewa tu hamjielewi mtatauelewesha kweli kuwaelewa MAGUFULI NI NAMBII ASIEKUBALIKA KWAO ILA HUKO DUNIANI WANAMTAMANI Leo kasemaaa Atafundiaha Adubuuu

Kwa udicteta ni number one kweli maana hofu imetanda hadi kwa viongozi wa dini tuliwasikia akina kakobe sasa wameunga juhudi. Katika udikteta wa hivyo hatuwezi kupata maendeleo ya watu yanayotakiwa. Watanzania wanataka uhuru na haki lakini kukosekana kwa uhuru na haki ni bora hata umasikini lakini wakawa huru hata Nyerere alikuwa anatembelea hayo maneno.

Haiwezekani kujisifia kuwa kuna maendeleo wakati hata watumishi wa serikali yake wamenyimwa nyongeza ya mishahara iliyopo kisheria. Hivi ukipita pale ubungo unaweza kueleza ni kwanini lile jengo la TANESCO lilibomolewa pale mbele maana barabara imejengwa hata hajaongezeka upana wowote ule si ndo udikteta wenyewe tena alitamba kabisa kuwa wakati wa kikwete alizuiwa.

Binasfi napenda sana Rais anayetambua uhuru wa watu pamoja na haki zao kama hizo nyongeza za mishahara yao pamoja na kwamba ni sheria imekiukwa kwa ubabe tu japo kiongozi anakuwa ameapa kulinda katiba ya nchi. Na sheria zote zinatokana na katiba ya nchi.
 
Jana ulinikera sana mpaka nikakutukana! Ona sasa leo ulivyoaibika! Itabidi nikutafute hapo jijini tuyajenge!
 
Elimu bure
Mil 50 kila kijiji
Kufufua shirika La ndege
Tanzania ya viwanda

Elimu bure aliiga cdm ambayo ilikuwa ni sera yao toka 2010. Milioni 50 kila kijiji wala usiseme maana ni utapeli kama utapeli mwingine. Kufufua shirika la ndege ni kweli ila mbinu aliyotumia kajichanganya. Tanzania ya viwanda imegeuka kuwa ni hadithi ya kufufua maiti. Na hoja ya msingi sio kutaja ahadi, bali hakufafanua atatekeleza vipi hizo ahadi zake.
 
Mikakati ya kufanya haya ni hipi? Hata mimi haya naweza kuahidi!

Yani watu wapewe mkopo halafu wasirejeshe hahahaha
 
Tulia kidogo,nijibu hiyo pesa ataipata wapi ambapo Magufuli kashindwa kuipata?
Lissu atapata pesa ya kutimiza ahadi zake pale-pale Mzee Pombe alipopata pesa ya kujenga Chato International Airport.

Mataga leo speech ya Lissu imewauma mnoooo kwa kuwa imegusa watanzia wanaotaabishwa na Mzee pombe na CCM.
 
Back
Top Bottom