Kikatiba hakuna mahala imeandikwa kuhisiana na nguvu ya maaskofu ila uliwahi kujiuliza nguvu ya dini katika amani ya nchi zote duniani iko wapi? Uliwahi juwa kuwa viongozi wanapo kula kiapo huapa kwa kushika vitabu vitakatifu vya dini zao na sio katiba ya nchi? Uwahi jiuliza kwanini katika kila mihadhara ya raisi anapo ongea na wananchi kwenye jukwaa lake huketi pamoja na viongozi wa dini katika eneo husika na sio polisi na viongozi wajuu tu? Ulishawahi juwa kwanini raisi huwa ana fanya vikao na viongozi wa dini mbalimbali ikulu?
Haya ni maswali machache tu yanayo hitaji tafakuri yako mkuu,
Hili swala unatakiwa juwa dini ina sehemu kubwa sana kuwapa unafuu serikali yetu kwaku hubiri amani,utulivu na upendo ndio mana serikali ina weza kutoa matamko makali sana ila watu wakaendelea kuwa watulivu kupitia viongozi wao wa kidini wakiwasihi kupendana, kuwa wepesi wa hasira na kusamehe.
So unapo sema huelewi nguvu ya maaskofu iko wapi nadhani hukuwa umewaza kwa mapana zaidi, pia subiria matamko mengine toka dini mbalimbali na uwakika wanakuja na wao maana nyuma yao wanaongoza mamia na maelfu ya waumini waki wahubiria utulivu na upendo kwa niaba ya serikali leo hii wakipuzwa udhania itakuwaje?

"Mind spiritual and natural powers exist and your leaders know, but choose to ignore at a times."
 
Hakuna hata moja la ukweli hapo hata wewe uwezi thibitisha hayo kuwemo kwenye IGA ni mambo waliyoyaokota mitandaoni tu.

Ni kikundi cha watu waongo

2 (1) inazungumzia IGA consultative committee. Kamati itakayokuwa inapanga na kuamua jinsi uwekezaji utavyo tekelezwa among other things. Isitoshe hakuna 2 (1), kuna 2 (a), (b) na (c).

Ibara ya 4 inazungumzia ‘uwanda wa ushirikiano na taasisi zitakazo tumika katika utekelezaji wa mkataba. Na 4 (1) ina kuelezea uwanda wenyewe ni maeneo yaliyotajwa katika appendix 1.

4 (2) inasema Tanzania itahitaarifu Dubai World zitakapo tokea fursa nyingine za uwekezaji, ili na wao waweze kuweka bid yao kwenye kushindania hizo tender. Lakini si kwamba lazima washinde au wapate wao hizo fursa. The English word used ‘to submit their proposals’ hiyo maana yake ni kuomba tender sio kupewa.

Ni hivi I can’t go through all the nonsense ambazo serikali ishajibu ni mambo tu wanayo yaokota mitandaoni yasiyo na kichwa wala miguu.
 
Sauti ya watu haiwezi kufananishwa na sauti ya Mungu binadamu tumejaa mapungufu au huu kauli ina fananishwaje?
 
Bahati nzuri kwenye siasa unadili na kitu kimoja kwa wakati acha 2025 watatoa waraka mwingine sawa ila tu waraka hautachagua wanasiasa na pia itakuwa kosa la kimkakati kwa kufanya hivyo watapoteza zaidi hadi MOU ile "gone are the days where the religious leaders decide politics of the country"
 
Waraka umesomwa leo hapa kwenye Jumia ya Mt. Marcelino. Kila muumini moyo umesuuzika. Napita bar nipate kabisa
 
Tutaona.. kama serikali na ccm wake kama hawato tubu 😅😅😅
 
Nimejibu za mwenzako 2 na 4; na wewe wacha nikujibu article 5 na 6.

Ibara ya 5 inazungumzia haki ya kuendeleza (miradi ya appendix 1), kusimamia uendeshwaji wa maeneo hayo (manage) au kuendesha maeneo hayo wao wenyewe (operate). Basically huo ndio msingi wa ‘concession agreement’ mtu akishawekeza anarudisha hela yake kwa kuendesha hayo maeneo kwa muda watakao kubaliana mpaka hela yake irudi; hata TICTS wamekaa bandarini kwa mkataba wa aina hiyo. Sasa hayo makubaliano mmeambiwa bado amtaki kuelewa mpaka wajue ataweka kiasi gani ndio wapangiane muda.

Ibara ya 6 inaelezea mambo ambayo serikali inabidi iridhie na kutoa vibali.
6 (1) ili miradi ya uwekezaji ianze serikali inajukumu la kuhakikisha mwekezaji anapata vibali vya kufanya hizo kazi ndani ya Tanzania katika maeneo husika, wanapewa uhalali wa kutumia ardhi ya sehemu za uwekezaji (kwa mujibu wa sheria za Tanzania), wanapata baraka za wenyeji katika maeneo hayo, pamoja na kupewa misamaha mingine ambayo wanapewa wawekezaji kwa mujibu wa sheria za Tanzania.

6 (2) baada ya kupewa maeneo hayo kama walivyoomba wapewe kwa misingi ya 6(1) iwapo huko mbele ikitokea mtu anaenda kudai eneo au anataka kuchukua eneo kinguvu serikali inawajibu wa kuingilia kati na kuwaondoa hao watu.
 
Usikute hata mkataba wenyewe hawajausoma wala hawahujui cha ajabu eti nao wanatoa tamko. ila dini hizi...mmmh!! Basi tu
Hapa unaongelea wakatoliki Watu ambao ni makini jama hujui kitu shut up
 
halafu yanatokea matutusa yanapinga hiuu waraka wa TEC wakati ni kwa maslahi mapana kwa vizazi hivi na vijavyo. Kukosa akili ni ugonjwa mbaya sana sana!
 
Wakatoliki ndo hawataki mkataba na Dpworld kisa ni waarabu waislam...
Hakuna cha kasoro za mkataba zirekebishwe wala Mahakama imesema mkataba hauna shida...

Wako very very clear....
Only watu wajinga ndo watajifanya hawajaelewa
Tatizo sio mkataba mbovu tatizo wao kama wao hawautaki na hii ni toka mwanzoni kabisa na hawataki uwekezaji sasa kama hawataki waarabu mbona wanyarwanda pale kwao Qatar imewekeza kwenye usafiri wa anga nakujenga viwanja na kumiliki shirika la ndege tena wazi kabisa rwanda air limenunuliwa kwa zaidi ya nusu na wanyarwanda wanajua na Kagame kakubali sasa sisi tunakuwa taifa gani kwa kuwa tu au sababu tu za kiimani za kundi fulani basi ndio ziamue kabisa maamuzi ya taifa hii haikubaliki na wala haina tija wao wamesema sawa ni uhuru wao kuongea ila wasizingatiwe hata kidogo kwa hili wapuuziwe kwa kuwa wanachowasilisha hakina maslahi kwa taifa.
 
Sasa saini alizomwagika mama na yule Mbarawa ni nini zile?
 
Tutaona.. kama serikali na ccm wake kama hawato tubu 😅😅😅
Huo muda ulishapita polarised politics hazina sehemu tena ktk nchi hii zile siasa za kuegemea dini au taasisi hazina nafasi wala ushawishi jumuia za watanzania za sasa ziko less religious ikija masuala ya siasa ila zikifikia masuala ya kijamii kama ndoa na mazishi hapo ndio religion inakuwa na mchango ndio maana ndani ya vyama kuna watu wa aina zote kwa ajili ya kupush ajenda ya vyama na nchi
"Mwisho Tanzania ni ya watu wote"
 
Watanzania tumezidi kuwa wanafiki na hatupendi kusema ukweli

Kwanini tunapindisha ukweli kuwa Rais wetu Samia amekiuka katiba ya nchi kitu ambacho ni UHAINI MKUU hivyo basi aachie madaraka

Shinikizo hapa ilikuwa ni samia kuachia madaraka na sio mjadala wa bandari kwani huo tayari umepita hadi bungeni
 
Acha uongo wewe! Lini Papa karuhusu ndoa za jinsia moja??!!! Mnakaa kwenye vijiwe vyenu mnadanganyana huko na kukashifu dini za wengine halafu unaleta kwenye majadiliano ya maana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…