Hoja 8 muhimu za TEC
14. Ibara zifuatazo za Mkataba huu zina matatizo yatakayosababisha nchi kutofikia uhuru wa kiuchumi (economic independence):
14.1. Ibara ya 2 (1): inayohusu lengo la Mkataba huu ambalo ni kuweka utaratibu unaoibana Tanzania kisheria katika kuendeleza, kuboresha na kuendesha bandari zote za bahari na maziwa, maeneo maalum ya uwekezaji, maeneo ya usafirishaji wa mizigo, na maeneo mengine ya kiuchumi.
14.2. Ibaraya 4: inayohusu wigo wa Mahusiano na Utekelezaji unaoitaka Serikali ya Tanzania kuwajibika kuijulisha Dubai kila fursa ya uwekezaji inapojitokeza.Hiiinakinzana na baadhi ya sheria za nchi yetu, kwa mfanosheria ya ushindani na ile ya manunuzi.
14.3. Ibaraya 5: ambapo DPWorldimepewa haki ya kuendeleza, kusimamia na kuendesha miradi pekee yake, wakati Tanzania inabaki na wajibu wa kumwezesha kufurahia haki hiyo.
14.4. Ibaraya 6:inayoitaka Tanzania kuwajibika kuipatia DP World vibali na vivutio vya kutekeleza miradi yake kama Serikali. Hii inapingana na baadhi ya sheria za kiutaratibu.
14.5. Ibaraya 7: inayoitaka Serikali kuwajibika kutoa mamlaka yanayotakiwa na mwekezaji bila ucheleweshaji.
14.6. Ibaraya 8: Haki ya kutumia ardhi ambapo Mkataba unasababisha uvunjifu wa sheria za ardhi na sheria zinazohusu masuala ya ardhi.
14.7. Ibaraya 10: Usiri wa Mkataba ambapo Mkataba unazuia mamlaka nyingine kama TAKUKURU /BUNGE kufuatilia mikataba.
14.8. Ibara za 23 na 24: zenye ugumu wa kujitoa kwenye Mkataba
Hizo hoja ni za kuungaunga hazina mashiko yote yote
MAJIBU
Ibara ya 2(1).
Kutoendeleza bandari zozote sehem ya eneo la uwekezaji hii naunga mkono ni mwendawazimu pekee atakaekubali kuipa faida serikal huku serikal ikimpa upinzani mwekezaji. Mwekezaji awekeze mwanza north port kisha aipelekee serikali faida wakat huo huo serikal inawekeza Mwanza south port kile kilichowekezwa na mwekezaji north port. HUKU NI KUMFUKUZA MWEKEZAJI NA HAKUNA MWEKEZAJI ATAKAEKUJA KUWEKEZA SEHEM YENYE SHERIA ZA KIJINGA KAMA HIZO.
HAO TEC SI NDO WALISAINI MoU na serikal. SERIKAL IMESHINDWA KUJENGA HOSPITAL KUBWA KAMA BUGANDO HUKU MWANZA SABAB NI KULINDA MTAJI WA MUWEKEZAJI HUYO TEC KWENYE KICHAKA CHA PPP
Ibara ya 4.
Hii ni nchi ACHENI hisia za kidini.Kama hii ni kweli basi hao maaskofu ni watu wa kupuuzwa. Kuwataarifu Dubai juu ya fursa zilizopo Kuna ubaya gani. Dunia itajuaje fursa zilizoko Tanzania pasina kutaarifiwa. DUBAI ATAPEWA TAARIFA KAMA AMBAVYO MABALOZI WETU NA OFISI ZETU ZITAKAVYOTOA TAARIFA KWA NCHI NYINGINE
DUBAI WAKIVUTIWA NA FURSA ILIYOPO WATAFATA SHERIA ILI KUWEKEZA.
Ibara ya 5.
Wew na hao maaskofu acheni upotoshaji na muwe wazalendo kwa taifa lenu. Serikal imesema namna itakavyoshiriki kweny huo uwekezaji. Usalama utakua ni jukumu la serikal, TPA na TRA watakua pale,kama serikal itamonitor usalama ,TPA watakuepo ,TRA watakuepo nyiny mlitak ushiriki upi wa serikali?
Ibara ya 6.
Hapa mmeamua kutumia kiswahili kuwachanganya watu.
NANUKUU" Tanzania kuwajibika kuipatia DP World vibali na vivutio vya kutekeleza miradi yake kama Serikali. Hii inapingana na baadhi ya sheria za kiutaratibu."
Kutekeleza miradi yake kama serikal kiaje yani?
Inapingana na SHERIA za kiutaratibu kama zipi?
Ibara ya 7.
Mshazoea ukilitimba sas wew na hao maaskofu mlitaka mwekezaji acheleweshewe anachohitaji.
Ibara ya 8.
Haki ya kutumia ardhi kumbe ,kwaio mlitak asiwe na haki ya kutumia ardhi. TOFAITISHENI KATI YA HAKI YA KUTUMIA ARDHI NA KUMILIKISHWA ARDHI.
UNAPOPANGA SEHEM UNAHAKI YA KUTUMIA HIO SEHEM NA SIO KUMILIKI HIO SEHEM PERIOD !!
Ibara ya 10.
Siri gani tena jamani kwan bunge si limeujadiri huu tunaouita mkataba sas usiri gani tena bunge halitakiwi kujua [emoji23][emoji23]
Ibara ya 23$24.
Incase ingekua zinasema hauwez kujitoa hapo mngekua na hoja ila kusema kuna ugumu wa kujitoa ni swala la ajabu.Mkataba lazima uwe na vipengele vigumu kujitoa ili asije mtu mmoja kaamka asubui tu akavunja mkataba.
Mkataba umesema zitatumika SHERIA za kimataifa kama kutatokea shida.HAPO VIPI