Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC): Hatuungi mkono Mkataba wa Bandari. Sauti ya Watu ni sauti ya Mungu
Correct me if I'm wrong
As far I know this was the first stages of the actual contract which was signed but not the full contract of what we have been discussing here.
Kumbe unakiri kuna saini wameweka si ndio?
 
Kwani wao waliposema inchi haitatawalika walikua na maana gani? Uliwahoji?
Unajua wakristo hawAapendi muislam aongoze so wanaanzisha chokocho then wanakimbia sasa kwa hili ndio na sie tumepata sababu
Kwani SSH ni muislam wa kwanza kuongoza Tanzania? Mbona hayo hayakutokea wakati wa Mwinyi na Kikwete? Msitafute sababu za kijinga
 
Hata kwny Mauaji ya Kimbari walishiriki mstari wa mbele kukusanya watutsi kwny Makanisa kama vile wanawaokoa lakini wakishajaa wanawaita Wahutu waje wawanalize, halafu cha kushangaza hao Watutsi waliowakusanya na kuwateketeza makanisani walikuwa Wakristo wenzao
Kwa hiyo mnataka tufike huko?

Kama mnataka tufike huko, basi chanzo itakuwa sio hawa watakaofanya haya. Chanzo kitakuwa ni maamuzi mabaya ya serikali ya CCM na Rais Samia kuwapa Tanganyika yetu waarabu wa Dubai kwa njia ya walichokiita "mkataba wa kiuchumi kuboresha bandari..!!"

Kwa hiyo wewe Pohamba ni kwanini sasa usizuie maafa hayo (kama unayaona yanakuja) kwa kumwambia Rais Samia Suluhu Hassan na CCM yake kuachana na hii kitu na badala yake umshauri aje na namna bora, na shirikishi na ya wazi kwa mujibu wa sheria na katiba kwa manufaa ya wananchi wote ili kuboresha hicho wanachosema uendeshaji na usimamizi wa bandari zetu?

Ndugu yangu Pohamba hebu tuwe wakweli tu. Hivi ni sahihi kweli kudhani tunahitaji Mzungu wa Ulaya au mwaarabu wa Asia kuja kuwekeza kwenye usimamizi na uendeshaji wa taasisi zetu za umma kama bandari au TANESCO au TANROAD??

Kama ni hivyo, basi tunakosea target. Uwekezaji wa mitaji, utaalamu na kiteknolojia wa wazungu au waarabu hawa unatakiwa kuelekezwa kwenye taasisi hizi: Ikulu, Bunge, mahakama, polisi na TISS..!

Hizi zimesha prove failure ktk utendaji wake na ndiyo maana wanaibuka na mauchafu haya ya mkataba wa DP World. Zinahitaji kubinafsishwa Kwa wazungu au waarabu..!
 
WARAKA WA MAASKOFU SIO ITHIBATI ZA MAONI YA WATANZANIA.

Na Thadei Ole Mushi

Niseme kwa kifupi sana kuhusu ujumbe wa baraza la Maaskofu kuhusu Bandari. Kwanza nisema wazi kuwa nawaheshimu sana vingozi wangu hawa wa Dini. Cha pili nisema tamko lao naliheshimu kwa kuwa wametumia haki yao ya kikatiba kutoa Maoni. Cha tatu niseme ni TEC ni moja ya vyombo imara sana kijamii hivyo wanatakiwa kila kitu wanachokisema hawaangalia zaidi maslah ya taifa.

Niwakumbushe vitu viwili kabla ya kuendelea. Cha kwanza ni kisa cha kuuwawa kwa mtu anayeitwa Galileo Galilei 1633. Nafahamu kisa hiki mnakijua, kwa manufaa ya wote ni kwamba Galileo kama mwanasayansi aligundua nadharia ya “Copernican” kwamba alithibitisha kisayansi kuwa “Dunia ndio huzunguka jua” nadharia hii ilienda kinyume kabisa na mafundisho ya kanisa kuwa “Jua ndio lililokua linaizunguka Dunia”. Kwenda huko kinyume na mafundisho ya Kanisa alitiwa hatiani na kuteswa vikali hadi kufa. Maandiko ya Roma yameandika kuwa alihojiwa vikali “Italo Mereu” wataalamu wa lugha wanasema Italo Mereu ni mateso makali hadi kufa.

Kwenye hili kanisa lilikuwa limefanya Makosa pasipokutafiti na kujiridhisha.

Kisa cha pili ni tukio la 1992 la Jaji Fransis Nyalali alipowasilisha ripoti ya Tume kuhusu mapendekezo ya watanzania ya uanzishwaji wa vyama vingi vya Siasa. Asilimia 80 walikuwa hawataki vyama vingi vya Siasa, ni Asilimia 20 tu waliyotaka vyama vingi vya siasa. Asilimia ndogo ilishinda na kuanzishwa vyama vingi vya Siasa.

Hoja yangu.

Kwenye waraka wa Maaskofa wamesimamia misingi mikubwa miwili kujenga hoja zao. Moja ni kwa nini taifa Moja la Kiarabu kupewa kandarasi yote, na hoja ya pili ni kwamba kwa vipimo vyao wenyewe wanadai watanzania wangi wanalalamika kuhusu huo mkataba. Maelezo mengine yalijazilizia nyama tu kwenye hoja hizi mbili.

Kwa kutumia kisa cha Galileo hapo hapo juu Baraza la Maaskofu halijapewa athibati (certification) kwamba mawazo yao na mitazamo yao itakuwa sahihi kwa asilimia 100. Lakini kuna hoja inajengwa hapa kuwa watanzania wengi sijui wametumia kipimo gani kupata hao wengi lakini hata kama ni wengi kuna hoja za Msingi zimeelezwa kila kukicha faida ya kuwekeza pale Bandarini. Watu wachache waliona vyama vingi vya siasa vina tija wakavipitisha.!!!

Ok

Maaskofu wanasema walitaka wazawa zaidi kuwekeza pale bandarini. Ni jambo jema sana…. Dunia ya Sasa rasilimali zake huwezi kuzifaidi mwenyewe. Hata kwa mataifa yaliyoelendea wanafika mahali wanabidi waite wawekezaji. Hakuna Nchi Duniani haina wawekezaji toka kwenye mipaka ya nchi zao.

Dunia inahama kwa haraka sana hasa mataifa yanayoendelea. Sera kubwa ni kuwekeza kwenye Teknolojia na ku Negleti raw materials za Africa. Kwa leo unaweza ukawa na Pamba usipate pa kuiuza, Kahawa ukakosa, tumbaku ukakosa nk. Lakina wao toleo jipya la I Phone tu watu wanapangana madukani kununua kwa bei wanayotaka wao. Hata haya Madini, Wanyama pori, Bandari nk watafika mahali wata-Neglet ni busara sana kuzitumia kipindi hiki maana muda unakuja itabaki historia.

Bado mifumo ya Dunia inatulazimisha kuwekeza, Kenya na Tanzania zikipigana uchumi wa Dunia hautaathirika lakini Urusi na Ukreni athari zake tunaziona.

Leo mmerekani ameamua kubana dola yake kila mtu anahangaika, akizidi kubana tutauziana nyanya moja elfu moja. Katika mazingira kama hayo unatokaje kwenye huo mnyonyoro?

Tatizo la Tanzania hatupendi fact ndio maana Prof Mhongo alivyosema hakuna mtanzania wa kuwekeza kwenye Gas na Mafuta tulimshangaa.

Nafikiri.

1. Baraza la Maaskofu lingeona kwanza dhamira njema iliyopo kwa Rais kwenye kuwekeza pale Bandarini bila kuangalia ni taifa gani limepewa hiyo Kandarasi.

2. Baraza la Maaskofu lingeona ufisadi, Urasimu, na wizi uliopo pale Bandarini washauri kwa umakini zaidi.

3. Baraza la Maakofu lisifikiri kuwa ni Tanzania tu ina Bandari. Majirani zetu wanazo na hii ni vita ya kukamata Soko la nchi za Congo, Malawi, Zambia, Uganda, Rwanda na Burundi.

4. Nchi tajwa hapo juu ambazo hazina Bandari mizigo yao kwa Mwaka ni tani milioni 60 kwa pamoja. Bandari ya Daresalam Mwaka jana na Juzi ni tani milioni 8 tu ilipitishwa. Jambo la Msingi la kujiuliza tani 58 milioni zilipitishiwa wapi? Tusifikiri ni sasa wenyewe tuna bandari.

5. Baraza la Maaskofu limerudia kosa lile lile la baadhi ya watu wa kawaida. Kutaja Dubai kama nchi pakee iliyopewa Bandari sijui wana nia gani ndani ila wamerudia pale pale kitu ambacho kinatoa Mwanya kwa ndugu zetu waislamu wanawaza kuja na waraka wao na ndio wataligawa taifa kabisa.

6. Kama waraka huu utaenda makanisani kama ulivyo ni waumini kulishwa Propaganda na Interest za watu wachache. Nafikiri ni Busara kujikita kwenye vifungu vilivyokosewa zaidi na kushauri virekebeshweje.

Anyway…

Baraza la maaskofu lingeweza kujikita kwenye vifungu vinavyoonekana vina kasoro kuliko kubeba makando kando mengine yanayoharibu ujumbe na nia njema ndani yake. Tujitahidi kuliunganisha Taifa

C&P from👇
Ole Mushi
0712702602
Huyu ameshalewa mbege na kitimoto ni mlevi sawa na walevi wengine tu.

Huyu hafikii hata level za Malisa GJ sembuse baraza la maaskofu?

Hii ni takataka ya Lumumba tu, hakuna hata mmoja mwenye akili huko kazi yao ni uchawa tu.

Hoja 8 muhimu za TEC

14. Ibara zifuatazo za Mkataba huu zina matatizo yatakayosababisha nchi kutofikia uhuru wa kiuchumi (economic independence):

14.1. Ibara ya 2 (1): inayohusu lengo la Mkataba huu ambalo ni kuweka utaratibu unaoibana Tanzania kisheria katika kuendeleza, kuboresha na kuendesha bandari zote za bahari na maziwa, maeneo maalum ya uwekezaji, maeneo ya usafirishaji wa mizigo, na maeneo mengine ya kiuchumi.

14.2. Ibaraya 4: inayohusu wigo wa Mahusiano na Utekelezaji unaoitaka Serikali ya Tanzania kuwajibika kuijulisha Dubai kila fursa ya uwekezaji inapojitokeza.Hiiinakinzana na baadhi ya sheria za nchi yetu, kwa mfanosheria ya ushindani na ile ya manunuzi.

14.3. Ibaraya 5: ambapo DPWorldimepewa haki ya kuendeleza, kusimamia na kuendesha miradi pekee yake, wakati Tanzania inabaki na wajibu wa kumwezesha kufurahia haki hiyo.

14.4. Ibaraya 6:inayoitaka Tanzania kuwajibika kuipatia DP World vibali na vivutio vya kutekeleza miradi yake kama Serikali. Hii inapingana na baadhi ya sheria za kiutaratibu.

14.5. Ibaraya 7: inayoitaka Serikali kuwajibika kutoa mamlaka yanayotakiwa na mwekezaji bila ucheleweshaji.

14.6. Ibaraya 8: Haki ya kutumia ardhi ambapo Mkataba unasababisha uvunjifu wa sheria za ardhi na sheria zinazohusu masuala ya ardhi.

14.7. Ibaraya 10: Usiri wa Mkataba ambapo Mkataba unazuia mamlaka nyingine kama TAKUKURU /BUNGE kufuatilia mikataba.

14.8. Ibara za 23 na 24: zenye ugumu wa kujitoa kwenye Mkataba
 
Waraka umesomwa leo hapa kwenye Jumia ya Mt. Marcelino. Kila muumini moyo umesuuzika. Napita bar nipate kabisa
Ni jambo zuri kuwa umesomwa na pia ni jambo zuri sana kuwa kama muumini umesikiliza na pia ni sawa kabisa kuwa na umedhihirisha kuwa ni wazi kuwa haukoreligious kwa kuwa yaliyosemwa umeyasikia lakini unarudi mtaani unaenda bar na pia unaendelea na shughuli zako kule umeenda tu kama routine ila yanayosemwa huyazingatii laiti ungekuwa ni wa kuzingatia wala usingetoka kule na kwenda zako bar na hii ndio uhalisia wa hali ilivyo jamii yetu ya kitanzania iko less religious kwa sasa ktk kufanya mambo yake ya kila siku tuna ile identity tu kwa ajili ya masuala ya kijamii kama mazishi basi na masuala ya ndoa ila sio haya mengine.
 
Hajui kama hata Majesuits (The most Intelligence secrety Agency society) ni la Roma catholic anasahau ndo wanaongoza uchumi wa dunia for almost 90% anasahau hata nchi zq arabuni zilipogoma kuingia mikataba nao wengi walikipta cha moto na viongozi wao waliishia kuuliwa Hadharani ......

Ngoja nimkumbushe kama aa umri mkubwa lakini anakumbuka alivyokuja Papa John Paul 2 anajua ulizi wake ulivyikuwa ulinzi wke na intellijense yake ni zaid ya RAIS yyte duniani....
MIMI ni Muslim ila kwa ROMA huwa navua kofia
Mie si mromani lakini nadhani huwajui waromani. Ni kanisa lililo na wataalamu wa kila namna. Wao mbali na kusomea teologia na falsafa za dini, pia usoma elimu dunia katika nyanja mbalimbali.
Kuna wachumi, wanasheria, wahasibu, wahandisi, madakitari, marubani, manesi na walimu pia.

Unavyo sema ukute hawajasoma usiwalinganishe na aina nyingine hawa jamaa uwa hawakurupuki. Na wana wataalamu wabobezi ktk intelijensia.
 
Hajui kama hata Majesuits (The most Intelligence secrety Agency society) ni la Roma catholic anasahau ndo wanaongoza uchumi wa dunia for almost 90% anasahau hata nchi zq arabuni zilipogoma kuingia mikataba nao wengi walikipta cha moto na viongozi wao waliishia kuuliwa Hadharani ......

Ngoja nimkumbushe kama aa umri mkubwa lakini anakumbuka alivyokuja Papa John Paul 2 anajua ulizi wake ulivyikuwa ulinzi wke na intellijense yake ni zaid ya RAIS yyte duniani....
MIMI ni Muslim ila kwa ROMA huwa navua kofia
Kwa kifupi Vatican ndio walioanzisha dini ya kiislamu ili kuwa na influence middle east.
 
Jiulize Kwanini Maaskofu Katoliki huteuliwa na Baba Mtakatifu wa Dunia

😂😂😂😂🔥🔥
Huu ndo utumwa wa fikra Waafrika tuliorithishwa tena ni sumu mbaya Sana huyo Papa ana utakatifu gani? Daah Binadamu tunashida unajua Asili na Historia ya Roman Catholic? Hizi ni biashara za Watu huyo kitima kakosea Sana kujifanya anatetea rasilimali zetu uku ana joho la wezi wanaotuibia kwa mgongo wa Dini dini gani chini ya jua? Mbona zil3 ruzuku 600B wanazopokea kila mwaka huku shule na hospitali zao zikitoza gharama Kubwa kwa Raia hawalizungumzii kama unyonyaji hatari zaidi kwa Taifa letu huu upumbavu Sana yaani kikundi Cha watu wenye maslahi yao wanataka kuleta machafuko nchini kwa kisingizio cha Dini flani nyonyaji Bora wangesimama Kama Watanzania na siyo kujivika joho la ukoloni wa tangu na tangu hao RC ndiyo hatari zaidi ya DpW.
 
Wakatoliki ndo hawataki mkataba na Dpworld kisa ni waarabu waislam...
Hakuna cha kasoro za mkataba zirekebishwe wala Mahakama imesema mkataba hauna shida...

Wako very very clear....
Only watu wajinga ndo watajifanya hawajaelewa
Vipi kuhusu vipengele kama hivi kwenye mkataba, wewe unavikubali?

14.7. Ibaraya 10: Usiri wa Mkataba ambapo Mkataba unazuia mamlaka nyingine kama TAKUKURU /BUNGE kufuatilia mikataba.
 
Hoja 8 muhimu za TEC

14. Ibara zifuatazo za Mkataba huu zina matatizo yatakayosababisha nchi kutofikia uhuru wa kiuchumi (economic independence):

14.1. Ibara ya 2 (1): inayohusu lengo la Mkataba huu ambalo ni kuweka utaratibu unaoibana Tanzania kisheria katika kuendeleza, kuboresha na kuendesha bandari zote za bahari na maziwa, maeneo maalum ya uwekezaji, maeneo ya usafirishaji wa mizigo, na maeneo mengine ya kiuchumi.

14.2. Ibaraya 4: inayohusu wigo wa Mahusiano na Utekelezaji unaoitaka Serikali ya Tanzania kuwajibika kuijulisha Dubai kila fursa ya uwekezaji inapojitokeza.Hiiinakinzana na baadhi ya sheria za nchi yetu, kwa mfanosheria ya ushindani na ile ya manunuzi.

14.3. Ibaraya 5: ambapo DPWorldimepewa haki ya kuendeleza, kusimamia na kuendesha miradi pekee yake, wakati Tanzania inabaki na wajibu wa kumwezesha kufurahia haki hiyo.

14.4. Ibaraya 6:inayoitaka Tanzania kuwajibika kuipatia DP World vibali na vivutio vya kutekeleza miradi yake kama Serikali. Hii inapingana na baadhi ya sheria za kiutaratibu.

14.5. Ibaraya 7: inayoitaka Serikali kuwajibika kutoa mamlaka yanayotakiwa na mwekezaji bila ucheleweshaji.

14.6. Ibaraya 8: Haki ya kutumia ardhi ambapo Mkataba unasababisha uvunjifu wa sheria za ardhi na sheria zinazohusu masuala ya ardhi.

14.7. Ibaraya 10: Usiri wa Mkataba ambapo Mkataba unazuia mamlaka nyingine kama TAKUKURU /BUNGE kufuatilia mikataba.

14.8. Ibara za 23 na 24: zenye ugumu wa kujitoa kwenye Mkataba

Hizo hoja ni za kuungaunga hazina mashiko yote yote

MAJIBU

Ibara ya 2(1).
Kutoendeleza bandari zozote sehem ya eneo la uwekezaji hii naunga mkono ni mwendawazimu pekee atakaekubali kuipa faida serikal huku serikal ikimpa upinzani mwekezaji. Mwekezaji awekeze mwanza north port kisha aipelekee serikali faida wakat huo huo serikal inawekeza Mwanza south port kile kilichowekezwa na mwekezaji north port. HUKU NI KUMFUKUZA MWEKEZAJI NA HAKUNA MWEKEZAJI ATAKAEKUJA KUWEKEZA SEHEM YENYE SHERIA ZA KIJINGA KAMA HIZO.

HAO TEC SI NDO WALISAINI MoU na serikal. SERIKAL IMESHINDWA KUJENGA HOSPITAL KUBWA KAMA BUGANDO HUKU MWANZA SABAB NI KULINDA MTAJI WA MUWEKEZAJI HUYO TEC KWENYE KICHAKA CHA PPP

Ibara ya 4.

Hii ni nchi ACHENI hisia za kidini.Kama hii ni kweli basi hao maaskofu ni watu wa kupuuzwa. Kuwataarifu Dubai juu ya fursa zilizopo Kuna ubaya gani. Dunia itajuaje fursa zilizoko Tanzania pasina kutaarifiwa. DUBAI ATAPEWA TAARIFA KAMA AMBAVYO MABALOZI WETU NA OFISI ZETU ZITAKAVYOTOA TAARIFA KWA NCHI NYINGINE

DUBAI WAKIVUTIWA NA FURSA ILIYOPO WATAFATA SHERIA ILI KUWEKEZA.

Ibara ya 5.

Wew na hao maaskofu acheni upotoshaji na muwe wazalendo kwa taifa lenu. Serikal imesema namna itakavyoshiriki kweny huo uwekezaji. Usalama utakua ni jukumu la serikal, TPA na TRA watakua pale,kama serikal itamonitor usalama ,TPA watakuepo ,TRA watakuepo nyiny mlitak ushiriki upi wa serikali?

Ibara ya 6.
Hapa mmeamua kutumia kiswahili kuwachanganya watu.

NANUKUU" Tanzania kuwajibika kuipatia DP World vibali na vivutio vya kutekeleza miradi yake kama Serikali. Hii inapingana na baadhi ya sheria za kiutaratibu."

Kutekeleza miradi yake kama serikal kiaje yani?

Inapingana na SHERIA za kiutaratibu kama zipi?

Ibara ya 7.
Mshazoea ukilitimba sas wew na hao maaskofu mlitaka mwekezaji acheleweshewe anachohitaji.

Ibara ya 8.
Haki ya kutumia ardhi kumbe ,kwaio mlitak asiwe na haki ya kutumia ardhi. TOFAITISHENI KATI YA HAKI YA KUTUMIA ARDHI NA KUMILIKISHWA ARDHI.

UNAPOPANGA SEHEM UNAHAKI YA KUTUMIA HIO SEHEM NA SIO KUMILIKI HIO SEHEM PERIOD !!

Ibara ya 10.

Siri gani tena jamani kwan bunge si limeujadiri huu tunaouita mkataba sas usiri gani tena bunge halitakiwi kujua [emoji23][emoji23]

Ibara ya 23$24.
Incase ingekua zinasema hauwez kujitoa hapo mngekua na hoja ila kusema kuna ugumu wa kujitoa ni swala la ajabu.Mkataba lazima uwe na vipengele vigumu kujitoa ili asije mtu mmoja kaamka asubui tu akavunja mkataba.

Mkataba umesema zitatumika SHERIA za kimataifa kama kutatokea shida.HAPO VIPI
 
Nichoamini ni kuwa hao maaskofu wametumia diplomasia sana kutoa huo msimamo wao lakini ukapuuzwa. Hawa maaskofu hawapendi kabisa kuja hadharani kutoa msimamo kama waliotoa leo lakini inaonekana kuna watu watakuwa walishupaza shingo. Kwa asieijua TEC ina wataalamu wa kutosha na huwa haikurupuki na watakuwa wamefanya utafiti wa kutosha na kutafuta taarifa za kutosha kuhusiana na huo mkataba halafu wakalinganisha faida zake na hasara zake mwisho ndio wakaja na hilo hitimisho la kuukataa huo mkataba.
Utakuta hata wanaoukubali mkataba hadharani wamewafata kisiri kuwaambia watoe tamka...Kwa jinsi hali ilivyo kun akitu nakiona huenda wale wanaosuport mktaba hadharani wanaupinga Kimya kimya na wanatumia sauti za watu wengine
 
TEC inayo nguvu kikatiba.... Nayo ni kutoa maoni.
Una lingine?
Tec ni kukundi cha watanzania wana haki yyte katika katiba kama watanzania wengine. Akuna mkenya wala mganda pale wote ni watanzania. Wana haki zote kwa sababu ni watanzania. Wana haki kikatiba maana ni watanzania
 
Hebu tuwekee hapa CV ya Profesa Lipumba.
We dokta wa mchongo hao wenzio wamesoma theology yaani kwa akili timamu kwamba hawajui hata kwamba TICTS wameoperate pale miaka zaidi ya 20.

Wanakuja kusema eti tangu uhuru hakuna muwekezaji alikuja kuendesha bandari😅😅😅huoni kama ni "vilaza pro" means wanaongelea kitu hawana elimu nacho.


Huoni kwamba weny akili za miujiza hawaweza kujenga hoja na elimu yao ni takataka .!!
 
Back
Top Bottom