Toka uhuru wamekamatwa wezi wangapi? Nini kimeshindikana kuzuia huo wizi?
Wakati na elimu unabadili jamii
sengobad
Leo wazungu wakitaka kuleta ule utumwa wao uliokuwa hapa wataweza?
Nimejaaliwa umri na Mungu wa kuanza kuona Nyerere anaapishwa kuwa Rais
Nimepanga foleni ya kununua Unga wanaokula Farasi ili na sisi tule .
Nimeishi wakati ule nyerere alipiga marufuku maduka yote binafsi akatuwekea maduka ya ushirika ya serikali . Sukari unaruhusiwa kununua robo kilo tu kwa siku na kibiriti cha njiti kimoja
Na tumewekwa Rumande kwa kosa la kunukia sabuni za kenya wakati huo nyerere kagombana na Kenya.
Na nimemwaga mafuta ya kupikia na sukari kwenye mashimo ya choo kuogopa migambo wakati wa uhujumu uchumi wa yule maluuni sokoine .
na mwananchi yyt aliyepinga kelele alikuwa anawekwa jela miaka isio na idadi bila kupitia mahakamani.
Leo vijana wanataka waruhusiwe kuoa wanamme wenzao na wako tayari kumtukana mpk Rais.
Kwahio Jibu lako ni WAKATI umebadilika.
Ule WIZI wa zamani jamii imechoka nao. Na japo bado upo lkn Mapambano pia yataendelea kwa kasi vile vile.