Nchi yetu inaendeshwa kwa utawala wa sheria na serikali yetu ni ya kidemokrasia inayotokana na watu wenyewe kwa mujibu wa Katiba yetu.
Nchi Ina mihimili 3 ya serikali, bunge (wananchi) na mahakama. Kati ya mihimili hii 3 wananchi bila kujali umri, jinsia na dini zao wanawakilishwa na wabunge wao wa majimbo katika kufanya maamuzi kuhusu wao.
Baraza la Maaskofu limesika likitoa matamko na maazimio kuhusu uwwkezaji kwenye bandari, Huku likisema wananchi wengi hawaupendi mkataba wa ubinafsishaji wa bandari. Hao wananchi ni akina nani, wako wangapi na wamekutana wapi kuwauliza maoni Yao? Nchi Haina dini, tukutane kwenye kampeni za uchaguzi na kisanduku chakula kama Kuna mwenye njia/sera mbala ya namna ya kuindesha nchi badala ya kikundi Cha watu kutaka kuwasemea wananchi wote nchini kitapeli.
Jambo lolote na hoja yoyote haiwi na nia njema kama ikichanga maneno kama Tanganyika, Zanzibar, watanganyika, wazanzibar, waisilamu, wakristo, wazayuni, Wazungu, au Waarabu. Maneno haya ni hatari sana kusikika majumbani, mtaani, kazini na kwenye taasisi mbalimbali. Ukiyasikia yaepuke na yazimwe kwa gharama yoyote ile ili yasiote, kumea na kuzaa mbegu.
Tutailinda Katiba
Tatizo mnajibu hoja bila hata ya kusoma na kuelewa kilichoandikwa.
Kwanza ufute maneno yako kuwa eti wananchi wote wanawakilishwa na wabunge. Hoja yako ingekuwa sahihi kama hao wanaoitwa wabunge kama kweli wangekuwa walichaguliwa na wananchi. Hawa wanaoitwa wabunge, ni majizi ya kura, na wengine hawakuchaguliwa wala hata kuwa na kura hata moja ya mtu yeyote, tena miongoni mwao akiwemo Waziri Mkuu. Kiuhalisia wananchi hawana mwakilishi yeyote.
Jambo la pili unatakiwa kufahamu kuwa, hata kama tungekuwa na bunge, bado kuna taasisi mbalimbali ambazo kupitia kwazo, watu wa makundi mbalimbali wanawakilishwa. Taasisi hizo ni pamoja na taasisi za kidini, taasisi za kiweledi (kama vile vyama vya madaktari, wahasibu, wanasheria, wahandisi, wakulima), vyama vya makundi maalum, vyama vya wafanyakazi, n.k. Hizi taasisi zote ni taasisi ambazo zipo karibu zaidi na wanachama wao kuliko hata mbunge. Ndiyo maana taasisi hizi, zina uwezo wa kushauri, kutetea, kuonya, kukosoa na hata kupinga, japo hawana mamlaka ya kufanya maamuzi ambayo serikali inalazimika kutimiza.
Tumeona, wakati wa utawala wa Mwinyi, kupitia BAKWATA, waislam waliitaka Serikali iwaruhusu wanafunzi wasichana kuvaa mashuleni mavazi yanayoendana na imani yao. Baadaye Serikali ikaridhia. Kama kungekuwa na wajinga, wanaofikiria kwa namna kama yako, wangesema kuwa BAKWATA haina mamlaka ya kufanya maamuzi na kisha kupeleka matakwa ya waislam Serikalini.
TEC wamesema wazi kuwa wana mfumo wao wa kupata maoni ya waumini wao toka ngazi ya kaya mpaka Taifa, na kwa utafiti wao, wananchi walio wengi hawataki huo mkataba wa hovyo uliosainiwa na Serikali na kisha kupitishwa na bunge haramu. Nasema ni bunge haramu kwa sababu ni zao la uovu.
UTAMBUE
Wananchi wote, mmoja mmoja au kwa kupitia taasisi zao wana haki ya kukosoa, kupinga, kukataa, kushauri au hata kulaani au kupongeza maamuzi ya Serikali. Ambaye halijui hili, ni dhahiri itakuwa ni kwa sababu ya ujinga wake.