Ila kwa upande wangu ama maoni yangu siku hizi bora mtoto alelewe tu na single mothers ama apelekwe tu kwa bibi na babu yake huko kuliko kulelewa kwenye ndoa na baba na mama. Kwasababu mtoto atakua akiona vituko. Ndoa siku hizi zina vituko sana. Halafu ni full maigizo. Ndoa ni tamu miaka miwili ya mwanzo baada ya hapo ni sarakasi na maigizo. Chunguza tu vizuri madogo waliolelewa na kukua kwenye ndoa na baba na mama toka miaka ya 2005 yaani tabia zao hovyo bladikengez kabisa.
 
Ukishaona mtu analia lia kuhusu single mother jua hajiamini ila anatamani kuwa na uwezo wa kumtuliza single mother.

Mwanaume anayejiamini si mlalamishi. Kama hataki mwanamke mwenye mtoto atachukua asiye na mtoto, huwezi kuta anataka mwanamke asiye na mtoto huku analalamika kuhusu mwenye mtoto.

Ukiona analalamika kuhusu mwenye mtoto huyo amependa mwenye mtoto ila hamuwezi au kamshindwa sababu ya either hana kipato, au ana hofu ya kugongewa au hajiamini tu.
 
Wanaharakati wanawake ndio wa kulaumiwa, shetani kawatumia apendavyo kuharibu maadili ya ndoa na familia kupitia nyanja za kielimu, afya, sheria na uchumi. Wanawake haoleki tena kirahisi kama zamani. Kuzaa wanataka ila kuolewa imebaki kwenye dini tu, nako huko wanafunga ndoa za show off baada ya muda mfupi ndoa inavunjika kwa sababu za kipuuzi. Hawa wanawake wakiwa na uchumi mzuri hawaambiliki wala kushaurika kuhusu matumizi ya fedha nyumbani. Wana ubinafsi, wanajenga miradi makwao bila waume zao kujua. Ni jeuri huwafanyi kitu sheria wanajua fasta wanadai talaka hata kama ndoa ilifungwa kwa imani isiyotambua talaka ni kitu gani. Wanapenda kuishi peke yao bila mume kwa kuwa wanajiweza kifedha za kutunza watoto
 
Binafsi naunga mkono hoja haitokaa itokeee kamwe kuwa na single mother ever😃
 
Wanaume tumesusa kuoa,wanawake wanafika umri WA kuolewa hawaoni mtu wanaona umri unawapita muda ,wanaona Bora wawe tu single maza,na kina junior wao😀😀
 
Kabila gani?

Kuna makabila mengi Sana msichana akifikisha miaka 20 hajaolewa anaambiwa japo azae...
Miaka 20 Akiwa hajaolewa wala Hana mtoto anaonekana kachelewa sana

Ni suala la culture hasa pwani na baadhi ya mikoa
Upo sahihi pwani visichana vidogo vinazazaa tu,Kisha vinajifanya vijitu vizima,vinataka vipewe shikamoo na watu wazima
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…