Tumeshuhudia malumbano makali sana ya wananchi, baada ya Spika Ndugai "kumsummon" CAG, Profesa Assad afike kwenye Kamati yake ya maadili hapo tarehe 21/01/2019
Katika tathmini yangu nimeona kuwa watu wengi sana wanampinga Spika Ndugai, hususani pale aliposema hata kwa pingu atahakikisha Prefesa Assad anafika kwenye kamati yake kwa ajili ya kuhojiwa kwa ambacho Spika Ndugai amekiita, eti amelivunjia heshima Bunge kwa kuliita dhaifu!
Swali la kumuuliza Spika Ndugai, hivi anadhani ni mtanzania gani ambaye hajui kuwa Bunge lake ni dhaifu na liko "controlled" na mhimili mwingine wa Executive??
Kama mhimili wake anaamini kuwa upo huru, ilikuwaje matakwa ya mamilioni ya watanzania kuwaangalia wawakilishi wao LIVE kwenye Bunge wakiwasilisha matatizo yao ya majimboni yalipuuzwa na badala yake yakatekelezwa "maagizo" ya Mheshimiwa Rais ambaye peke yake ndiye ambaye hakutaka Bunge lionekane LIVE??
Kama Spika Ndugai anaamini kuwa mhimili wake haupaswi kuingiliwa, ilikuwaje Mheshimiwa Rais alimsifu kwa namna anavyowatimua wabunge wa upinzani na yeye akamhakikishia kuwa atakapomaliza kuwatimua wabunge hao "wakorofi" ndani ya Bunge, amwachie yeye huku "uraiani" ambako ata-deal nao??
Kwa maoni yangu yeye Ndugai ndiye amayestahili kutiwa pingu na kuburuzwa mahakamani kutokana na mhimili wake wa Bunge kuwa dhaifu na kushindwa kufanya kazi wanayotakiwa kikatiba ya kuisimamia serikali na badala yake yeye amekuwa "akiikingia" kifua serikali hiyo
Na wala Profesa Assad hakufanya kosa lolote na ametimiza wajibu wake wa kuusema ukweli mchungu kuwa Bunge ni dhaifu kutokana na kitendo chake cha kuwakumbatia wezi wa Mali ya Umma