Tatizo ni kuwa tuna wabunge wengi wa CCM
 
Hakuna bahati mbaya katika hili maana umuhimu wa Bunge tunaujua na Spika Ndugai hatukushushiwa mawinguni tunamjua na akachaguliwa. Kwa nini hili lilitokea?

Bunge sasa linaitwa (hata wenyewe wanajiita) dhaifu, visa vya ajabu ni vingi, Wabunge wanaovuruga kama Mlinga ndio tunawaona, kufukuzana ndio fasheni, yote chini ya uongozi mbovu wa Ndugai.

Mbunge kapigwa risasi badala ya yeye kuongoza mapambano ya kuwapata wahusika yeye anaongoza ya kumshambulia aliyepigwa risasi!
Huyu ni 'adui' wa Bunge iweje anaendelea kuwa spika?

Na hata hao wapinzani mbona Hakuna jaribio la kumtoa hata kama litashindwa? Jaribio la kumng'oa kiongozi huwa linampa wasaa wa kujitafakari.

Fanyeni sasa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
watanzania vilaza kwel...
ko we unadhani mambo anayofanya ndugai kajiamulia mwenyew..??
yupo mkulu nyuma yake bob, yy anatumika kama kijakazi tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mleta mada umetoa dukuduku lako lakini hujashauri nini kifanyike,Nchi hii ni yetu zote na hatuna pa kukimbilia kwa hiyo lazima tutetee haki yetu kama Rais wetu anavyosema kuwa lazima kuwa mzalendo na nchi yako na kuwa mzalendo ni kutetea maslahi yote ya kuendeleza taifa lako siyo kukaa kimya tu.
Tunaomba wawakilishi wetu mtupe mrejesho wa malalamiko ya wananchi kwa ujumla wake msisubiri mpaka hali ikiwa mbaya ndy tuanze yale ya Venezuela
 

Kweli kusoma na kuelewa ni tofauti. Mleta mada hanashauri nini kifanyike?

kwa nilivyomuelewa ni kwamba zifanyike juhudi za kumtoa Ndugai hata ikitokea hazitafanikuwa basi ztamsaidia kujitafakari.
 
kumbuka tafsiri na maana ya neno mzalendo imebadilika kwa awamu hii ya uongozi wa nchi yetu pendwa
 
Ndugai hawezi kujitafakari, aliwalichapa bakora ccm wenzake lakini bado anajisifia hadharani kama vile ni sifa na anawalinganisha na wanafunzi
 
"Wanaounga mkono waseme ""ndiyo"" NDIYOOOOOOOO! Wasiounga mkono waseme ""siyo"" SIYOOO!"

Walisema ndiyo wameshinda! Unategemea nini?!

Juzi kati hapa habari ya kikokotoo ilitawala vyombo vya habari. Ni yale yale maamuzi ya wengi, japo wapo wachache waliouona muswaada huo kuwa butu tangu awali akina Mh. Bulaya, na walipozungumza bungeni walizomewa lakini Leo kikao wapi? Hadi Rais kaamua. Ujinga wetu wengi bado tunathamini misemo ya wahenga kwa zama hizi. Usemi wa wengi wape ulikuwa na thamani kipindi ambacho dunia yetu ilikuwa haijaelimika. Lakini hadi leo wapo walioganda huko. "Ndiyoooooooo"!
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mfumo wa Spika kupatikana kutoka kwa wabunge hao hao tutaendelea kupata Spika wenye akili kama za Ndugai miaka nenda miaka rudi...Spika ilitakiwa asitoke chama chochote na waombe kazi kwa kuonyesha CV zao na kiwepo chombo maalumu Spika na Katibu wa Bunge waombe kazi, hapo zitatungwa sheria zinazoendana na wakati uliopo kwa Maendeleo ya Wananchi sio kama sasa zinatungwa sheria kwa maendeleo ya viongozi...Spika anamchukia mkaguzi na mdhibiti wa fedha za Umma bado anajiita mzalendo?
 
Si amesema hapo, wabunge wa upinzani wafanye jaribio la kamtoa yaani kutokuwa na imani na spika, hata kama jaribio litafeli ila kuna kitu atajifunza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hayo ni mambo ya kikatiba zaidi kitu ambacho hakitakuwepo kwasababu kazi za watu zitakuwa ngumu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maajabu yaliyomfanya Ndugai kuwa spika ndiyo hayo hayo yaliyotuwekea rais wa sasa, maendeleo yatobaki kuwa ndoto za mchana
 
HIVI KWANINI SIKU HIZI ANANYOA KIPARA KAMA J MAKAMBA??

KUNA NINI? MWENYE TAARIFA PLEASE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…