Hakuna Bahati mbaya katika hili maana umuhimu wa bunge tunaujua na Spika Ndugai hatukushushiwa mawinguni tunamjua na akachaguliwa, Kwa nini hili lilitokea?
Bunge sasa linaitwa (hata wenyewe wanajiita) dhaifu, visa vya ajabu ni vingi, wabunge wanaovuruga kama Mlinga ndio tunawaona, kufukuzana ndio fasheni nk , yote chini ya uongozi mbovu wa Ndugai.
Mbunge kapigwa risasi badala ya yeye kuongoza mapambano ya kuwapata wahusika yeye anaongoza ya kumshambulia aliyepigwa risasi!
Huyu ni adui wa bunge iweje anaendelea kuwa spika?'
Na hata hao wapinzani mbona Hakuna jaribio la kumtoa hata kama litashindwa?
Jaribio la kumng'oa kiongozi huwa linampa wasaa wa kujitafakari.
Fanyeni sasa!
Sent using
Jamii Forums mobile app