Aisee 🤔🤔
 
kwanini ndugai anampaka mama yetu kipenzi matope ya makusudi?

Hivi ni kweli ndugai hajui katiba yetu inasema nini kwa wabunge wasio na chama?

Lengo la ndugai kwa mama yetu ni nini?

Ndugai haoni ni muda wa mama kuzungumza mambo makubwa ya kujenga nchi kuliko kupoteza muda kwa vitu vidogovidogo kama hivi vya kushindania katiba inasema nini kwa wabunge wasio na chama?

Kwanini kama taifa tunalotaka maendeleo

Tunashindana vitu viko wazi namna hii?

Hivi hatuoni kama tunalichafua taifa bila sababu yoyote ya msingi?

Mama ongea neno moja kuhusu hili kwenye vikao vya sirini
 
Mama analijua hilo sakata Ila amechagua kukaa kimya ingali mengine mengi anayakemea waziwazi, hapo ndipo napimuangalia Ndugai kama mtu anayejua kabisa kwamba anatekeleza maelekezo ya boss wake.
 
Kubabaika huku si kwa kawaida na nahisi kuna jambo kubwa ambalo hatulijui.
Kwa mtu anayemwamini Mungu na aliyekuwa na uelewa wa kutosha ni wazi Job Ndugai amepotoka na anaendelea kupotoka katika suala la wabunge 19 wa viti maalum wanaodaiwa kuwa wa Chadema.
Ushahidi wa Chadema umewekwa wazi,maamuzi yaliyofanywa katika matukio kama hayo miaka ya nyuma yamewekwa wazi na kwa ushahidi usio na shaka.
Huku kubabaika kunatokana na nini?
Sasa ni wakati wa kuulizana,kubabaika huku knamnufaisha nani?
Uvurugaji wa uchaguzi 2020 haukufanyika kitaalamu na ulikuwa wa kibabe sasa inakuwa kama hadithi ya mbwa mwitu na mwana kondoo ("mwaka jana ulinichafulia maji ya kunywa na mwana kondoo alipojibu "mbona mwaka jana nilikuwa sijazaliwa"..)
 
HUKO CHADEMA NAKO KUNA SHIDA, AKINA MDEE WALIKATA RUFAA, HADI LEO CHADEMA WAMEKAA KIMYA!
 
Kwa hiyo Spika hana katiba ya CDM? Alikubalije mwakilishi wa CDM kuwa kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni na hajui kilichoandikwa kwenye katiba yao?

Kwanini alipopokea barua na akaona vigezo na masharti hayajatimizwa kwa nini hakuirudisha kuomba viambatanisho?
 
Ndugai anazidi kujianika kuonyesha kuwa Kiti cha Spika siyo size yake. Yaani yeye anavaa kiatu no 6 wakati cha Spika ni no 11. Kutembelea lazima iwe vichekesho kama siyo majanga.
 
Hua ofisi ya Spika haina utaratibu ya kujibu barua anazoletewa? kwanini ofisi yake inashindwa kuwajibu CHADEMA kwa barua kama alivyoandikiwa.
 
kunatokana na kuwa covid 19 waliingizwa na marehemu. kama unavyojua waafrika hawavunji maagizo ya marehemu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…