Ndugai ni Spika asiye na sifa za kuwa spika
Ndugai hasira ake mara nyingi huwa ina mwingiza choo cha kike kwakwelii..
 
'Nyakati za mababu,waliopewa madaraka walipakwa mafuta kama ishara ya kutakatifuzwa na kuondolewa katika maisha ya kawaida ili wavalishwe hulka za kiungozi' - hii sikufahamu hii elezea hapa kidogo walipakwa mafuta gani?
Yalikusaidia kuwabadilisha ili waongoze kwa haki?
 
Ndungai naona ni mtu poa kwa wastani, ila sema ana hasira za karibu sanaaa
Ndungai anauma na kupuliza. Ndumilakuwili. Hana nia njema na upinzani hata kidogo. Kamati ya maadili ya nini aache kupoteza muda wa kupokezana vikombe vya chai kisa kamati ya maadili. Futa kauli yako Mnyika arudi bungeni Lusinde aombe radhi kwa Bunge la Tz nukta. Amesahau kuugua kwake. Kupona kwake ilikuwa ni huruma na Neema ya Mungu. Wabunge wa vyama vyote walimuombea, Leo amepatwa na ujasiri wa kusahau yote. Mungu halali usingizi Ndungai
 
Kiti cha Spika ndio muamuzi wa mwisho katika mtanziko wa mambo ndani ya jengo la bunge, anapaswa kuongoza kwa busara kuliko jazba na hisia za kichama.

Spika anapaswa kuamua kwa kufuata kanuni na taratibu za kibunge,pale ambapo kanuni zimekaa kimya,hapo "busara" za Spika hupaswa kutumika. Lakini Ndugai ameanza kutumia "busara za spika" hata katika maamuzi ambayo kanuni zipo wazi. Katika mazingira haya,kwanini watu wasikuone m'baya

Kuna siku aliamua kubetua kanuni, kuondoa kipindi cha maswali ya moja kwa moja kwa Waziri Mkuu eti kisa "usomaji wa bajeti". Lakini ilijulikana amemkimbiza PM asijibu maswali magumu juu ya serikali kuingilia uchaguzi wa EALA na Katibu wa bunge "kusajili" vyama viwili vya CUF, ile CUF A na CUF B wakati katika kumbukumbu ya vyama vyenye wawakilishi vilivyopo bungeni hakuna vyama hivyo.

Yeye Ndugai, bila aibu na kwa kushirikiana na katibu wa bunge, waliamua kuunda vyama vyao, kimoja wakakiita CUF-A na kimoja wakakiita CUF-B. Hata Spika alipokuwa akimuita Habibu Mnyaa, alitambulisha kwa kusema "Habibu Mnyaa wa CUF-B karibu umwage sera zako". Hili ndio bunge la Ndugai.

Spika Ndugai siku hiyo alimuuliza Mbowe kwenye uchaguzi wa EALA,kati ya Masha na Wenje,nani ni mwanamke? haikuwa kauli nzuri na ya heshima kwa wenzake na wanaume wenye familia. Alivumiliwa kwasababu yeye ndio mwenyekiti. Lakini kusema Wenje au Masha, watu aliokaa nao bungeni kwa miaka mitano, kwamba kati yao nani ni mwanamke na nani ni mwanaume, yalikuwa ni matusi ya wazi.Kama kuitwa fa-*la ilikuwa ni jambo la kuudhi, kwanini kumuona mwanaume kama mwanamke lisiwe jambo la kuudhi?

Serukamba aliwahi kutoa tusi kubwa sana lakini "alibebwa",Nkamia aliwahi mtukana Sugu kwa kumuita mbwa, ikapotezewa, Lusinde hutukana sana bungeni na wabunge hushangilia. Kati ya wabunge wenye rekodi nzuri ya matusi, wabunge wanaostahili tuzo ya matusi, basi Livingstone Lusinde ni hodari. Aliwahi mwambia Lema alikuwa anapumuliwa gereza la Kisongo na hakuchukuliwa hatua. Kwenye hili la Mnyika,Spika Ndugai kampongeza Lusinde kwa kuwakomesha wapinzani.

Halima Mdee na Bulaya wataadhibiwa, lakini aliyemuita Mnyika mwizi hataadhibiwa wala kutafutwa. Sauti ya kumuita Spika fal--a ilisikika,ila ile ya kumuita Mnyika mwizi haikusikika . Yule aliyemwambia Mdee wakati ule "kikalishe chini utulie",hakutiwa nguvuni, wala huyu aliyetamka mwizi kwa Mnyika hatajulikana.

Ndugai anaona makosa ya utovu wa nidhamu kwa wenzake tu, yeye mbona kwenye kura za maoni alimpiga mwenzake Chilongani na "sungururu" ya kichwa mpaka akazimia? Ule ulikuwa ni mfano mzuri? Tena naibu Spika na mbunge anayetetea nafasi yake? Jazba na ubabe, si hulka ya kiti kinachohitaji hakima kama cha spika.

Neno fa*la,linalingana na lile alilotamka Mkapa kuwa watu ni malofa na wapumbavu, huyu naye alikuwa mfano mzuri kwa matamshi yale pale Jangwani? Lofa na kilaza ni maneno yenye uwiano, kilaza na fala yanashabihiana...Moja lilitamkwa na mkuu wa nchi, moja na Mkuu wa nchi mstaafu na moja ni la Mbunge wa Kawe.

Huu mfano wa lugha nzuri, uwe kwa viongozi wote,waliopo madarakani na waliotoka madarakani. Hii itajenga uhalali wa kukemea kila kiongozi anapovunja taratibu.
Tunaishi na kurudi katika zama za mhimili mmoja uliojichimbia kuliko mihimili mingine...Dhana ya bunge huru,zuri na lenye ushindani wa hoja inapotea.

Mlinga mbunge wa Ulanga anafahamika kwa lugha za kashfa na kuudhi,ndani ya bunge aliwahi kutamka kuwa wabunge wanawake wa UKAWA hawawezi kupata hizo nafasi bila "kuvua chu**pi. Alishangiliwa na wabunge wote wa CCM, wake kwa waume, hata hao kina Stella Manyanya, Jenista Mhagama, Ummy Mwalimu wanaojifanya wanaharakati wa "gender" kwenye bunge hawakukemea kauli ile. Walishangilia na kugonga meza.

Katika kipindi ambacho Ndugai alipaswa kuacha vihasira vya kijinga na ajabu ajabu ni kipindi hiki. Miezi minne ya kukaa juu ya mashine India ilipaswa kubadili muelekeo wa maisha na mfumo wake wa kiuongozi. Alipaswa kutambua kuwa,Mungu wake mwenye fadhila na rehema,amempa tena zawadi ya uhai ili kuja kuwatukimia watu wake kwa haki na amani, hekima na busara. Ili siku ya kurudisha hesabu mbele za Mungu wake, ahesabiwe yale aliyoyafanya kwa zawadi ya uongozi aliyopewa na Mungu.

Lakini sbb madaraka hulevya,basi naye amelewa na kulewa!!Thawabu na malipo ya uhai alioongezewa na Mungu, ni utumishi wenye haki na usawa kwa Watanzania na wabunge waliokupa nafasi ya kuwaongoza. Hii ndio nafasi nyingine uliyopewa na Mungu, itumie kuongeza marafiki na sifa njema itayakayobaki katika kumbukumbu na mioyo ya Watanzania.

Kila mtu alimtakia heri na afya njema,watu walimtumia meseji na kumpigia simu bila kujali itikadi zao. Watu walipenda arudi haraka ili kuja kuleta busara,mtangamano na ushirikiano katika bunge. Watu walihitaji uwepo wako ili kurudisha radha ya bunge la ushindani wa hoja lilioanza kupotea. Badala ya kuibua chombo kinachozama mwambao,sasa unakididimiza kwa mawe na majabali.

Inahitajika HEKIMA, ndio maana mfalme Suleiman licha ya machaguo mengi ya kifahari aliyopewa na Mungu wake achague ili kuwaongoza watu wake,mfalme aliomba HEKIMA. Hii ni kwa sababu Uongozi bila HEKIMA ni sawa na ndoano bila boya .Kila uitupiapo kilindini,huzama na mawimbi.

Mfalme Suleiman aliomba akasema "Eee Mungu wangu,unijalie HEKIMA,ili niwaongoze watu wangu kwa haki na amani".Na hakika tunda la haki ni amani.
Amani katika bunge,haiwezi kutamalaki kama haki,usawa,uweledi havitachukua nafasi.

Hii ndio bahati mbaya ya ulevi wa madaraka,heri ya ulevi wa mvinyo au bia.Huondoka kwa "supu na maji baridi".Ulevi wa madaraka hudumu,ulevi wa madaraka huleta majivuno,kibri na majigambo.Ulevi wa madaraka hupumbaza.

Nyakati za mababu,waliopewa madaraka walipakwa mafuta kama ishara ya kutakatifuzwa na kuondolewa katika maisha ya kawaida ili wavalishwe hulka za kiungozi.Kwetu tunawapa katiba na vitabu vya dini.Tutahoji kimyakimya..."Ni kweli vitabu vile vya dini huwasaidia hawa viongozi wetu?"
Mwache alinde ugali jina lisije kukatwa na Grim Ripper ndani ya chama chake.
 
Nikikumbuka alivyokuwa anaombewa dua na makundi yote bila ubaguzi akiwa hoi India nashindwa kuelewa ni vipi Leo anaweza kuwa mbaguzi wa namna hii na kuonyesha chuki za kiasi kile kwa baadhi ya watu.
Ni kweli kabisa Ndugai kapona kwa Neema ili arudi aionyeshe jamii (hasa Bunge) juu ya ukuu wa Mungu, lakini yeye kaamua kutuonyesha mamlaka ya shetani. Matendo afanyayo hakika ni ya kishetani
 
Anachofanya Ndugai ni kujaribu kujipendekeza kwa Magufuli ukuachilia mbali hulka na ukosefu wa busara wake.
Ndugai sio na wala hajakuwa chaguo la Magufuli,na hataweza kuzui kwa njia yoyote Tulia kuchukua nafasi ya. Uspika msimu ujao
Mahaba ya Magufuli kwa Tulia pamoja na "usomi" anaouhusudu sana vinafanya Ndugai kutwanga maji kwenye kinu
 
Anachofanya Ndugai ni kujaribu kujipendekeza kwa Magufuli ukuachilia mbali hulka na ukosefu wa busara wake.
Ndugai sio na wala hajakuwa chaguo la Magufuli,na hataweza kuzui kwa njia yoyote Tulia kuchukua nafasi ya. Uspika msimu ujao
Mahaba ya Magufuli kwa Tulia pamoja na "usomi" anaouhusudu sana vinafanya Ndugai kutwanga maji kwenye kinu
Bandiko lako kuna kitu umenifundisha...Nimekuelewa mkuu
 
Ndugai ana upendeleo mkubwa sana bungeni lakini Mungu anaona mwisho utafika hutakuwa spika milele
 
Back
Top Bottom