Ramani ya Makao Makuu CHADEMA yanayotarajiwa kujengwa hivi karibuni
Mwenyekiti wa kudumu ni wa kwetu, ninyi kinachowawasha ni nini? Mungu mbariki Mbowe

Hapo umenena. Hawa jamaa. Kinawawasha Nini. Embu ongeza Volume. Chama chadema. Yeye sijui CCM. Why azungumzie mambo Ya CHadema. Kwanini wasiige mfano Wa wanachadema huwezi kuwakuta wanaongelea CCM wala Mwenyekiti Wao.
 
Mmeshindwa kunenga nyakat zile mnapata mamilion ya ruzuku, mtajenga sasa wabunge weng wamewakimbia na kupunguza ruzuku? Jitahidin mjenge angalau choo maana next election mnamalizika
Mhuuuu,watu bana wanawachuria wenzao eti ' next election watamalizika? WAO JE MA CCM,WANADHANI watakuwa salama?maana hali ya hewa ni chafu mno humo ndanina huku nje watu wnawasubiri kwenye kisanduku ha kura wawamalize,maisha yamewazindua wengi,uhalisia si maneno yenu matupu na mijisifa isiyokuwa na kipimo,.Binadamu hali maneno wala haishi kwa press release zenu za kisanii za kurudishiwa dhahabu kutoka kenya,au kusifiwa kumkamata mtendaji wa Takukuru,.Mimi mtu wa kawaida inanisaidia nini hii wakati nikihihitai tiba nilazima nitowe noti mfukoni? Kula yangu ya kila siku ni kukimbizana na Manispaa,na Uchumi ulivyo fubaa hata hizo biashara zime pwaya mno ,kwani umasikini umekithiri kiasi cha kuwa kila mtu amekuwa mchuuzi wa bidhaa za kichina,na akina mama wamekuwa mama ntilie,na wengine wanauza uji kila kona ya taifa,matumaini yamebakia ijini tuu,kubangaiza angalau upate kula ya leo,kesho Mungu yupo,tunaishi kwa imani zaidi.kama alivyoagiza Nabii issa,.😎
 
Kama walishindwa kujenga Jengo walipomchukua Lowasa wasahau.Ila Pwani nwwapongeza walitumia pesa za Sumaye kikamilifu Wana Jengo zuri Sana.Sumaye alipoingia chadema hawakumkawiza wakamkwapulia pesa zake chap chap na kumpa cheo Cha mwenyekiti wa chadema Kanda ya Pwani akawajengea Jengo.Lowasa alikwenda na matajiri Akina Rostam Aziz nk na matajiri wengi walikuwa nyumma Yake wangewatumia ilikuwa kazi ndogo tu.Chadema walikuwa na matajiri wengi Sana kuondoka kwa Lowasa na kufariki ndesamburo kumebomoa daraja linalounganisha chadema na matajiri.Sasa hivi Sio rahisi.Chadema mitandaoni hawatoi hela kwanza hawana Ni porojo tu.Ruzuku inakatika muda mfupi tu miezi michache ijayo .Hata waseme ruzuku yote iliyobaki watatumia kujenga hela haitoshi na uchaguzi mkuu watakuwa pesa hawana na mishahara ya wafanyakazi pesa itakuwa hamna.Kiujimla hiki kinachosemekana mchoro wa jengo la makao makui Ni ramani hewa iliyoletwa kuwa lagjai wanachadema kwa lengo analolijua Mbowe na genge lake la Akina Godbless lema tu

Wanaweza kujenga sasa. Tangu mabeberu Wa uchumi kubanwa na JPM wanawatumia kwa namna moja au nyingine kuleta fujo. Usione mauzi yatungwa hapa kila kukicha ukadhani ni bure. Ni mkakati Wa kutumia mitandao ya kijamii. Sema wengi Hawajaelimika. Na utawajua ukiongeza Volume utaoga matusi ndo unajua akili sio zao wamejiuza. Huwezi ona hoja ya vitu vya maendeleo. Wao Kazi yao kuvizia viclip na kuchomeka maneno ili kuponda. So usiseme hela watapata wapi. Mtumikie kafiri.
 
Hatimaye iitwayo saccoss imeamua kuwa na ofisi zake? Wanajengea makao makuu au kwenye mji wa biashara?
Wanajenga kwenye kiwanja cha Mwasisi wa chama kilichopo Dsm ili wawe wanatozwa kodi ya kiwanja kila mwezi.
 
Kampeni hewa ya mbowe hiyo kutaka aendelee kupewa uenyekiti chadema.Uchaguzi mkuu wa chadema uko njiani.Sasa hivi utasikia kila Aina ya propaganda za chadema sijui kufanya hiki sijui kufanya kile vyote hewa hewa tu kuwalaghai Wana chadema
Mbowe hana haja ya kufanya jambo lolote ili apitishwe. Kupita atapita tu na hata asipopita hilo jengo litajengwa tu.

Acha wivu!
 
Sikatai CCM kulikuwa na mafisi Lakini majengo ya CCM kibao mazuri sanacya ofisi na vitega uchumi yalijengwa .Haya chadema mnakosema hakuna mafisi jengo la makao makuu mbona liko kama Banda la kufugia kuku na hakuna kitega uchumi hata kimoja.
Unasifia majengo ya ccm ilhali unaishi chumba kirefu
 
Mbona jengo limekaa kizamani kabla halijajengwa?

Tafuteni wabunifu wa majengo ya kisasa, achaneni na ushamba huo. Madirisha utafikiri jengo lote ni la vyoo.

Mwaka 2019 huu. Mko wapi? '60s?
Wivu ni kitu kibaya sana....,
 
Hii ramani kiboko, kila chumba kina choo yake, But any way, ramani sio ujenzi, ramani ni njozi tu. Ingalikuwa ramani ni ujenzi hata timu ya Yanga wangalikuwa na uwanja wa kimataifa maana wanatuonyesha ramani mpya kila mwaka.
 
Labda wataijenga baada ya mzee wa roho mbaya kuondoka madarakani aka Kagame wa TZ
 
Back
Top Bottom