Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC): Hatuungi mkono Mkataba wa Bandari. Sauti ya Watu ni sauti ya Mungu
Hapa sasa ndio tutajua, .
Serikali na baraza la maaskofu wa Roman Catholic nani mkubwa, maana kwa mujibu wa wadau hapa inavyoonekana baraza la maaskofu ndio linaloendesha nchi ya wadanganyika.
Vipi BAKWATA nao watatoa waraka wao?
Pia madhehebu mengine ya dini wakitoa nyaraka zao itakuwaje?
Ipi nafasi ya wasio na dini nao katika nyaraka?
Vipi kama nyaraka zitatofautiana serikali itafanya nini?
Kama vipi tuchapane tu, ili kila mtu arejee kijijini kwao, nadhani baada ya mnyukano tutaheshimiana.

Kama wanautaratibu huo ama wakaanza itakuwa vema. Mwisho wa siku tutajua chuyu ni zipi, pumba zipi.

Kila kitu kitakuwa hadharani, binafsi natamani na wao watoe matamko haraka sana.
 
Kama wanautaratibu huo ama wakaanza itakuwa vema. Mwisho wa siku tutajua chuyu ni zipi, pumba zipi.

Kila kitu kitakuwa hadharani, binafsi natamani na wao watoe matamko haraka sana.
Sasa kwa mfano BAKWATA wakija na waraka wa kuunga mkono mkataba wa serikali na DP world itakuwaje
 
Ni bora waje na mkataba huo ili watanzania tukubaliane kuwa TANZANIA SI TAIFA LA KIDINI....

Hatutaki udini....

Watuache na amani yetu....

#KataaUbaguzi[emoji120]
JK atuambie 👉🏽 Hapa ilikuwa mambo ya kiroho au siasa? 👇🏾Walienda kufanya nini Vatican? 😄

Eti tusichanganye dini na siasa 🤨 hivi unatuonaje hawa?
Kama mlikaa kimya mpk sasa na kushindwa kusimama upande sahihi - ajue imeenda hiyoo 😂
#OkoaBandariZetu #TutaelewanaTu
 

Attachments

  • IMG-20230820-WA0030.jpg
    IMG-20230820-WA0030.jpg
    43.1 KB · Views: 2
Hapa sasa ndio tutajua, .
Serikali na baraza la maaskofu wa Roman Catholic nani mkubwa, maana kwa mujibu wa wadau hapa inavyoonekana baraza la maaskofu ndio linaloendesha nchi ya wadanganyika.
Vipi BAKWATA nao watatoa waraka wao?
Pia madhehebu mengine ya dini wakitoa nyaraka zao itakuwaje?
Ipi nafasi ya wasio na dini nao katika nyaraka?
Vipi kama nyaraka zitatofautiana serikali itafanya nini?
Kama vipi tuchapane tu, ili kila mtu arejee kijijini kwao, nadhani baada ya mnyukano tutaheshimiana.
Nyaraka za madhehebu ya wakristo hazitatofautiana. Nyaraka za mashehe ndio zutaunga mkono. Kwa hili wao ni kama Fisiemu tu maadamu mwarabu yupo.
 
Usikute hata mkataba wenyewe hawajausoma wala hawahujui cha ajabu eti nao wanatoa tamko. ila dini hizi...mmmh!! Basi tu
Mimi ni mwislamu hao watu wapo vizuri wamewekeza kwenye resilimali watu, wa fans zote hapo hawajakurupuku wamechambua kipengele kwa kipengela ndugu
 
Mama katuuza, nilimsikiliza Prof Shivji jana akiuchambua huu mkataba kwakweli inasikitisha, unajiuliza hawa walioingia mkataba na DP World ni Watz wenzetu kweli au mamluki?!.
Ndo ujue ma CCM kuna mazwazwa, hata ule wa bandari ya Bagamoyo Kikwete alikuwa ameshaa Sain, kama sio JPM, sasa Kikwete na huyu MAMa ni kama uji na mgonjwa
 
Mie si mromani lakini nadhani huwajui waromani. Ni kanisa lililo na wataalamu wa kila namna. Wao mbali na kusomea teologia na falsafa za dini, pia usoma elimu dunia katika nyanja mbalimbali.
Kuna wachumi, wanasheria, wahasibu, wahandisi, madakitari, marubani, manesi na walimu pia.

Unavyo sema ukute hawajasoma usiwalinganishe na aina nyingine hawa jamaa uwa hawakurupuki. Na wana wataalamu wabobezi ktk intelijensia.
Mimi ni pia nikiri ni mwislam, ukisoma hilo andiko limenyooka na inaonyesha kabisa limechambuliwa na watu waliosom wakaelimika sio wale wakushamgilia kuwa mama ametuletea neema ukiwaambia kwenye mkataba imeandikwa wapi hawawezi kukuambia
 
Sisi wavaa kobazi tunasubiri waraka wa BAKWATA tufate, maana yule mungu wa katoliki sie hatumtambui kabisa
 
My friend hawa siyo akinaMwaipopo, Hapo kuna PHD za kutosha na kama kawaida Genuine PHD holder yoyote (siyo kama ile Msukuma) huwa ni wapenzi wa maandishi na hawasomi tu bali ni kusoma na ku-analyse.
Wambie bana sio wa kwetu inatoa rais siyewze kuandika kwa usahihi intrumet of ful power kwa waziri wake
 
Ishu sio waarabu. Hakuna mwenye chuki na waarabu. Ishu ni aina ya mkataba na vipengele vyake. Ccm ni ileile na watu walewale wapiga dili. Hata mwendazake alikua ni mpigaji aliyejificha kwenye kivuli cha unyonge. Ni vile kila mmoja hujaribu eneo la kucheza na akili za wadanganyika ili waweze kuwapumbaza na kuwin majorities huku wakitimiza dili zao za upigaji.
Mtu mpigaji haukuchukui muda kumgundua, usilete chuki zako binafsi huku.
 
Afrika inaangamia kwa ukosefu mkubwa wa maarifa. Samia na serikali yake wanaingia huo mkataba kwa sababu ambazo walizieleza kwa kina na zikaeleweka.

Hata mkatoliki mwenzangu hayati JPM aliijenga reli ya SGR kwa trilioni 17 ili ibebe mizigo mikubwa zaidi yenye kulipiwa kodi kubwa zaidi itakayokwenda kuongeza pato la TRA.

Hao maaskofu wanayo haki ya kukataa kuunga mkono azimio lakini maamuzi yao hayawezi kuiyumbisha serikali ishindwe kutekeleza matakwa ya ilani yake ya uchaguzi.
Nilipoona 17 trillion nikajua amna kitu kichwani
 
ILa saa100 anawapa ccm wakati mgumu SANa yaana mtu unawataalam wa kila aina badala uwatumie unapanda ndege hapa kwa kodi zetu unaenda kusain hiyo takataka kama vile mtu amekatwa kichwa
 
Tumeshasikia msimamo wa katoliki juu ya bandari na wameunga mkono waumini wao.
Sasa na sisi tunasubiri BAKWATA itupe maelekezo kupitia tamko rasmi tufaate.
Binafsi sikuwa nimesoma huu waraka na nilikuwa mfuasi wa kuupinga huu waraka ila leo nikasema niutafute.

Nilichojifunza na sasa nauunga mkono huo waraka na Hakuna baya wala jambo la kidini lililoandikwa humo kama baadhi ya waislam wenye upeo mdogo wanavyodai. Jamaa wameandika facts tu na sio hiki msemacho nyie. Hawajataja Ukristo wala uislam. Sasa hili la kusema udini sijui limetokea wapi? Mapendekezo yao yametokana na kuupitia mkataba na kuonesha vifungu vyenye mapungufu ndani ya mkataba ambapo pia wadau wengi waliyasema.

Bro, ebu acheni blah blah.
 
Back
Top Bottom